Wadau pamoja na UDSM kuwa na sifa kubwa kimataifa na kuwa chuo kikongwe TZ lakini mazingira ya kusomea yanasikitisha hususani sehemu kama vyoo (mfano vyoo wa SR, CoET, TATAKI, PESS office, Old DARUSO offices & Halls of Residence hasa Main Campus) ninachojiuliza hakuna watu wanaoangalia masuala ya usafi hapa chuoni. Fikiria unaenda chooni unakuta mikojo imetapakaa mpaka sakafuni kinyesi kila mahali halafu mnapishana na prof. katoka kukata gogo humo humo huyooo anaelekea class kukata nyanga. AIBU. hebu jifunzeni kwa taasisi nyingine usafi unazingatiwa sana. Iweje MLIMANI CITY waweze nyie mshindwe? viongoz wa UDSM kuanzia VC, DVC, Directors, Deans mnatembelea magari ya gharama sana lakini usafi wa choo unawashinda?