ibanezafrica
JF-Expert Member
- Oct 23, 2014
- 7,261
- 6,543
Tukiwa tunaendelea na maombolezo tuviombe baadhi ya vyombo vyetu vya habari mjitahidi kutuletea matangazo ya moja kwa moja kwa muda wote wa tukio lengwa kwa wakati huo kulikoni ilivyo sasa ambapo baadhi ya vyombo hivi wakati tukio likiendelea au msafara unapopita barabarani wao wanafanya uchambuzi studio!
Hii kwa kweli mnatunyima na kututoa kwenye mood sisi wengine tunaoshiriki kupitia runinga, mjue tupo mamilioni tunaofuatilia nchi nzima.
Ningeshauri mtupe matukio yote Live kama yanavyoendelea katika muda husika ikiwa ni pamoja na msafara unapopita barabarani tunahitaji tuone njia, walimosimama waombolezaji na inapendeza tuzisikie na sauti zao za kuimba, kuaga na kulia, jambo hili linaleta hisia na msisimko kuliko kutuwekea nyimbo ya background toka studio wakati msafara ukipita!
Nina imani mtarekebisha kidogo katika hili naelewa kama ni uchambuzi bado tuna zaidi ya wiki mbili za maombolezo kipindi hicho tutahitaji sana uchambuzi na shuhuda mbali mbali.
Mwisho niwapongeze kwa jitihada zenu kujitahidi kutupa mrejesho wa yote yanayoendelea tokea Dar, Dodoma, Unguja na hatimaye Mwanza na Chato.