Ni aibu yaooo....
Kwanini CCM kwa umri wa miaka 52, inashindwa hata kuanzisha jambo wenyewe hadi wavizie Chadema wamefanya nini na wapi, kisha wao waige?
Tumeshuhudia matukio kadhaa ambapo CHADEMA imepanga kufanya mkutano wa hadhara kwa sababu fulani ya msingi, kisha wanafanya.
Kumaliza tu utasikia kina Nape wanaibuka CCM itafanya mkutano katika uwanja uleule waliotumia Chadema, bila hata ya kuwa na jambo la msingi la kuja kueleza wananchi isipokuwa kuja kutukana Chadema. Mifano iko mingi: Temeke, Jangwani, Mwanza nk, ndiyo maana najiuliza ni kuishiwa au?
Mifano mingine ni M4C, tumesikia pia CCM wataenda mikoani... sijui wataitaje, ningesema waite M4D(D=death). Kwa sababu hawawezi kubuni kitu chao, tunaweza kuwasaidia... lakini si aibu jamani kwa umri wa miaka 52 kuendelea kuigaiga vya wengine????
Kwa miaka 52 madarakani, nadhani ingependeza vyama vingine ndivyo viige vya ccm, kwa sababu ya uzoefu, badala yake vyama vya upinzani, hususan Chadema ndo imekuwa kinara wa ubunifu, na mikakati mathubuti ya kuleta maendeleo kwa mtanzania.
Mtu mzima mwenye umri wa miaka 52, kama hawezi kusimama mwenyewe, hadi aige ige wanachofanya wengine aitweje?
Ndo maana nauliza CCM umri iliyonayo... kwa kukosa dira ya kusonga mbele... hadi kusubiri kuiga tukiiteje?
.....Maana graph hiyo inakwenda chini sasa.... sijui mwisho wake..kwani ikifikia hatua ya kushindwa hata kuiga itafanyeje??? Labda itakuwa kukaa chini na kusubiri kifo..