Vyombo vya habari vimechangia kupotea kwa mwandishi Azory Gwanda?

Jana kwenye malumbano ya hoja wakizungumzia uzalendo kuna mtu alimtaja Ben Saanane, msimamizi akawa na haraka kweli kumrudurisha kwenye hoja kana kwamba ameona hamna uhusiano wa hoja ya uzalendo na Saanane.
 
Nimeangalia Jana Mke wa huyo Mwandishi akizungumzia hilo sakata iliniuma sana ilibidi nibadilishe hiyo Star TV yaani inaumiza mno...ila naamini hukumu ipo hapa hapa inaweza ikawa sio leo wala kesho...
 
Wakishafuzu huko JIHA... basi kamanda siro na deputy wake Mombasasa waanze kujiandaa maana hao watoto wataleta "fire and fury"
" fire and fury " kwa sauti ya trump!!! haaaa haaa haaaa, !! mkuu umenifurahisha! !
 
Wasiojulikana ni mtego wa panya , hakuna asiyehusika kila mtanzania atahusishwa kwa namna moja ama nyingine
 
Vyombo Vya Habari Vimechangia Kupotea Kwa Mwandishi Azory Gwanda Kwasababu Viliamua KUYAFUMBIA MACHO Matukio Ya Watu Kuokotwa Kwenye Sandarusi Coco Beach, Watoto 1300 Kupotea Kibiti, Watu Kutekwa Hovyo Kila Siku, Laiti Kama Wangekemea Vitendo Hivi Leo Mwahabari Wao Asingepotea

Kuna wakati walipotea watu wa Kawaida..Waandishi hawakuwasemea, walitekwa wengi bado walikuwa kimya. Kwasababu hii imekuwa dhambi tuliyoilea Leo ametekwa mwenzao wameona madhira yake. Sishabikii utekwaji huu. Ila natamani mjue kwanini hamkupaswa kuwa waoga wakati wakitekwa wengne

mr mkiki.
Wewe hujui usemalo, Mungu akusamehe bure
 
Back
Top Bottom