Serikali ya Tanzania yasema polisi bado wanachunguza kupotea kwa Mwandishi wa habari Azory Gwanda

Jerlamarel

JF-Expert Member
Sep 14, 2021
843
2,517
Polisi bado wanachunguza kutoweka kwa mwandishi wa habari maarufu wa Tanzania Azory Gwanda ambaye alitoweka mwaka 2017, amesema Msemaji Mkuu wa Serikali ya Tanzania, Gerson Msigwa katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Jumapili mjini Mwanza.Msigwa amesema hakuna taarifa mpya ya kiuchunguzi bali polisi wanaendelea na kazi hiyo pamoja na watu wengine na si juu Azory Gwanda pekee.Gwanda alitoweka Novemba 21, 2017 baada ya kuripoti kwa kina juu ya mauaji yasioeleweka na kupotea kwa watu katika wilaya ya Kibiti, mkoani Pwani.

Miongoni mwa waliouawa huko ni askari polisi nane waliovamiwa wakiwa kazini. Wazari ya Mambo ya Ndani ya Nchi wakati huo, Mwigulu Nchemba alisema wahusika wa mauaji walikuwa ni wahalifu. Kutoweka kwa mwandishi wa kujitegemea, Azory Gwanda ni mkasa ulioitikisa tasnia ya habari Tanzania tangu 2017. Mwaka 2019, Kamati ya kuwalinda waandishi habari CPJ ilielezea kwamba tangu kutoweka kwa mwandishi huyo wa kujitegemea, serikali ya Tanzania ilikuwa haijatoa taarifa zaidi ya kuahidi kuchunguza mkasa wa kupotea kwake.

Kauli ya leo Jumapili ya Bw. Msigwa ni ya karibuni zaidi kutolewa na serikali ya Tanzania kuhusu kutoweka kwa Bw. Azory Gwanda, baada ya kuwa kimya kwa muda mrefu. Tangu mwaka 2019 miito imeendelea kutolewa kwa serikali ya Tanzania kutoa ufafanuzi kamili kuhusu hatma ya mwandishi habari Azory Gwanda baada ya waziri ya Mambo ya Nje wa wakati huo nchini humo, Prof. Palamagamba Kabudi, kusema katika mahojiano na BBC kuwa 'sio Azory Gwanda pekee aliyetoweka na kufariki katika eneo la Rufiji'.

Tangu kupotea kwa Azory kumekuwa na shinikizo kutoka kwa makundi ya haki za kibinaadamu, waandishi wa habari na mashirika ya habari ambayo yamekuwa yakitoa wito kwa mamlaka Tanzania kutoa kipaumbele kwa suala la Gwanda na kutoa majibu kuhusu hatma yake kupitia kampeni mbali mbali katika mitandao kama vile #WhereIsAzory na #MrudisheniAzory zikisambazwa kwa kiwango kikubwa hapo awali kwenye mitandao ya kijamii.

Mwandishi huyo wa Tanzania alikuwa akiifanyia kazi kampuni ya Mwananchi wakati alipotekwa katika mazingira ya kutatanisha. Alikuwa akiripoti matukio ya mauaji katika eneo la Kibiti katika mwezi ambao alipotea. Serikali ya Tanzania imekuwa ikisema kuwa inachunguza suala lake na watu wengine waliotoweka lakini hakuna kilichoafikiwa hadi sasa.

Kwa upande mwingine akijibu swali kutoka kwa mwandishi wa habari katika kikao cha leo, Msemaji Mkuu wa Serikali ya Tanzania Bw. Gerson Msigwa amesema, Serikali haijazuia mikutano ya vyama vya siasa iwe ya hadhara au ya ndani bali kinachofanyika ni utaratibu tu wa kisheria kupitia Polisi wanaosimamia sheria juu ya uhakika wa kuwa na usalama.

Vyama vya ssiasa vya upinzani nchini humo vimekuwa vikilalamika kuzuiwa kufanya mikutano ya kisiasa na wanachama wake wakiwemo viongozi kukamatwa. Kadhalika, Bw Msigwa amesema Serikali inafanyia kazi rufaa dhidi ya uamuzi wa Mahakama ya Afrika Mashariki iliyoamua kuwa vifungu 12 vya sheria ya Huduma ya Habari ya mwaka 2016 vifutwe au virekebishwe kwa kukiuka misingi ya mkataba ulioanzisha Jumuiya hiyo. Hatahivyo hakufafanua zaidi kwa kauli kuwa hilo ni jambo la kisheria.

BBC.​
 
Ahh makonda ajitazame huko alipo, ingekuwa mm ni Makonda chap kwa haraka ningeenda kwa Taliban.
 
Serikali itoe dau kwa watakaotoa taarifa nzuri za waliopetea kama Azory na Ben Saanane. Likiwa dau kubwa wapo watu watakuja na hiyo taarifa.
 
Yaani watanzania mnaonwa kama vilaza sana hivi kweli watu wenye akili zao timamu wataamini eti miaka serikali ilishindwa kuchunguza hilo tukio?
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Hawa jamaa hawa !!.

Kwamba hawajazuia vyama vya upinzani kukutana na wananchi !! . Nakumbuka hata KAMATI KUU YA NCCR ilizuiwa kutumia msimbazi center . Lakini kesho yake Ccm waliutumia ukumbi huo huo !! .
 
Inaelekea unazo taarifa zao na unachosubiri ni kutangazwa kwa dau kubwa kwa atakayetoa taarifa sahihi
 
Polisi bado wanachunguza kutoweka kwa mwandishi wa habari maarufu wa Tanzania Azory Gwanda ambaye alitoweka mwaka 2017, amesema Msemaji Mkuu wa Serikali ya Tanzania, Gerson Msigwa katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Jumapili mjini Mwanza.Msigwa amesema hakuna taarifa mpya ya kiuchunguzi bali polisi wanaendelea na kazi hiyo pamoja na watu wengine na si juu Azory Gwanda pekee.Gwanda alitoweka Novemba 21, 2017 baada ya kuripoti kwa kina juu ya mauaji yasioeleweka na kupotea kwa watu katika wilaya ya Kibiti, mkoani Pwani.

Miongoni mwa waliouawa huko ni askari polisi nane waliovamiwa wakiwa kazini. Wazari ya Mambo ya Ndani ya Nchi wakati huo, Mwigulu Nchemba alisema wahusika wa mauaji walikuwa ni wahalifu. Kutoweka kwa mwandishi wa kujitegemea, Azory Gwanda ni mkasa ulioitikisa tasnia ya habari Tanzania tangu 2017. Mwaka 2019, Kamati ya kuwalinda waandishi habari CPJ ilielezea kwamba tangu kutoweka kwa mwandishi huyo wa kujitegemea, serikali ya Tanzania ilikuwa haijatoa taarifa zaidi ya kuahidi kuchunguza mkasa wa kupotea kwake.

Kauli ya leo Jumapili ya Bw. Msigwa ni ya karibuni zaidi kutolewa na serikali ya Tanzania kuhusu kutoweka kwa Bw. Azory Gwanda, baada ya kuwa kimya kwa muda mrefu. Tangu mwaka 2019 miito imeendelea kutolewa kwa serikali ya Tanzania kutoa ufafanuzi kamili kuhusu hatma ya mwandishi habari Azory Gwanda baada ya waziri ya Mambo ya Nje wa wakati huo nchini humo, Prof. Palamagamba Kabudi, kusema katika mahojiano na BBC kuwa 'sio Azory Gwanda pekee aliyetoweka na kufariki katika eneo la Rufiji'.

Tangu kupotea kwa Azory kumekuwa na shinikizo kutoka kwa makundi ya haki za kibinaadamu, waandishi wa habari na mashirika ya habari ambayo yamekuwa yakitoa wito kwa mamlaka Tanzania kutoa kipaumbele kwa suala la Gwanda na kutoa majibu kuhusu hatma yake kupitia kampeni mbali mbali katika mitandao kama vile #WhereIsAzory na #MrudisheniAzory zikisambazwa kwa kiwango kikubwa hapo awali kwenye mitandao ya kijamii.

Mwandishi huyo wa Tanzania alikuwa akiifanyia kazi kampuni ya Mwananchi wakati alipotekwa katika mazingira ya kutatanisha. Alikuwa akiripoti matukio ya mauaji katika eneo la Kibiti katika mwezi ambao alipotea. Serikali ya Tanzania imekuwa ikisema kuwa inachunguza suala lake na watu wengine waliotoweka lakini hakuna kilichoafikiwa hadi sasa.

Kwa upande mwingine akijibu swali kutoka kwa mwandishi wa habari katika kikao cha leo, Msemaji Mkuu wa Serikali ya Tanzania Bw. Gerson Msigwa amesema, Serikali haijazuia mikutano ya vyama vya siasa iwe ya hadhara au ya ndani bali kinachofanyika ni utaratibu tu wa kisheria kupitia Polisi wanaosimamia sheria juu ya uhakika wa kuwa na usalama.

Vyama vya ssiasa vya upinzani nchini humo vimekuwa vikilalamika kuzuiwa kufanya mikutano ya kisiasa na wanachama wake wakiwemo viongozi kukamatwa. Kadhalika, Bw Msigwa amesema Serikali inafanyia kazi rufaa dhidi ya uamuzi wa Mahakama ya Afrika Mashariki iliyoamua kuwa vifungu 12 vya sheria ya Huduma ya Habari ya mwaka 2016 vifutwe au virekebishwe kwa kukiuka misingi ya mkataba ulioanzisha Jumuiya hiyo. Hatahivyo hakufafanua zaidi kwa kauli kuwa hilo ni jambo la kisheria.

BBC.​
Msigwa unastahili nini sijui. Kuna siku utajuta na kusema ukweli. Usione watu ni wajinga, muda ukifika utaona kuwa watu wanakuzidi akili mbali
 
Nyie MASHETANI ni bora mkae kimya. Mkae mkijua Azory ana ndugu, jamaa na marafiki.

Halafu mwendazake alipenda sana kukaa mbele kanisani. Huyu mwenzie anajifanya swala tano. Tunawazoom tu, mkae mkijua Mungu hadhihakiwi.
 
Taarifa zipo ila serikali ndio kikwazo maana wanajua chanzo cha huo uovu. Iko siku uovu wote huo utakuwa hadharani. Si unaona Sabaya ameanza kukiri kuwa alikuwa anapokea maagizo toka juu kutekeleza uhalifu? Huko huko alikosema Sabaya ndio unyama wote ulikokuwa unapangwa. Hata shambulio la Lisu linaeleweka vizuri ni maagizo ya nani na akina nani walitekeleza shambulio lile. Lisu anasema siku ya shambulio lake walinzi wanaolinda geti lile waliondolewa. Hapo unataka ushahidi gani tena.
aelekea unazo taarifa zao na unachosubiri ni kutangazwa kwa dau kubwa kwa atakayetoa taarifa sahihi
 
Yaani watanzanis mnaonwa kama vilaza sana hivi kweli watu wenye akili zao timamu wataamini eti miaka serikali ilishindwa kuchunguza hilo tukio?
Maswala mengi sana yanayoulizwa humu kuhusu Azori ben Tundu tayari polisi wanafanya kazi kwa weledi.Majibu yote wanayo na naamini wahusika wanajulikana.Sasa nani aanze.hapo ndo kuna............ makengeza.
 
Back
Top Bottom