Vyombo vya habari kutokurusha bunge LIVE

Vyombo vya habari kutokurusha bunge LIVE

Mtoa mada, mimi mbona nimeona bunge live asubuhi hii . kuna shida? Au mnapenda kuona wakizitwanga muone live. Mimi najua kamera za vituo vyengine vipo watakuonyesha kama recorded
 
Habari za asubuhi wadau,

Ni muda mrefu sana nimekuwa nikifuatlia mwenendo wa serikali mpya ya awamu ya 5 Tanzania hususani katika kusimamia haki za watanzania ikiwemo ya kupata taarifa na uhuru wa vyombo vya habari.

Kiukweli naona hoja zinapishana na sioni nguvu za wasomi wetu katika kuishauri serikali hii na kama ipo basi si ya kuzalisha matokeo chanya miaka 5 ijayo hii ni hatari sana.

Nimezipokea kwa masikitiko taarifa za kutorusha live bunge kutoka vyombo mbalimbali vya habari ambvyo vinaoperate binafsi. Na sasa watatakiwa kuchukua signals kutoka TBC ambao kwa mujibu wa taarifa nilizonazo wameanzisha studio maalum ya kurusha matangzo inayopatikana bungeni dodoma.

Lakini pia hiyo studio itarusha live sehemu/kipindi cha maswali na majibu sana. Hoja ya msingi mwanzoni ilikuwa pesa nyingi zinapotea kurusha live matangazo lakini zipo taasisi zilizotaka kufund hzo broadcasting costs still serikali inaonekna haiko interested???? Labda wanataka hizo pesa wapewe watengeneze barabara[emoji2] [emoji2] [emoji2]

Maoni yangu Rais magu anaonekna ni mpenda haki kwa watanzania je haoni watu kutopata taarifa za bungeni yanayojili kunadumiza haki? Na je uhuru wa vyombo vya habari ambavyo vilitumika kiasi kikubwa kumcampaign na kumfanya aingie madarakani vitakuwaje? TBC ni shirika la umma ambalo kamwe haliwezi kuuma serikali kwa kufuata editoral policy walizonazo.
Mazuri yote ya JPM yanaweza kupotea kwa hatua hii ya kuwanyima wananchi walipa kodi fursa ya kupata taarifa muhimu ...
 
HIVI SAA HIZI ZA ASUBUHI BADALA YA KUHANGAIKIA RIZIKI UNATAKA KUANGALIA VIPINDI VYA BUNGE????
AU HUNA KAZI ZA KUFANYA SAA HIZI????
Any person who is alright upstairs wouldn't post such a thing. Hata kama unalipwa kwa kufanya hivyo ni kwamba unadhalilisha utu wako.
 
Naunga mkono hoja, wananchi tushikamane tuwe na msimamo mmoja
 
Hii ni zaidi ya kubana matumizi. Ni kuwanyima wanachi haki yao ya kujua kile wawakilishi wao wanachokiongea. Mbona vituo binafsi navyo vimezuiliwa?

Eti wanadai wanataka watu wengi wafanye kazi badala ya kuangalia bunge, mara ooh tunabana matumizi , lakini ukweli unajulikana.
 
Nakerwa sana na chama changu CCM kutokana na hii tabia ya udikteta ya kuminya haki yetu ya msingi ya kuhabarishwa.

Ningependa upinzani bungeni wagome kabisa kuudhuria vikao vya Bunge Hadi CCM iachie. CCM wenyewe hatuwezi kupitisha miswaada bila kujadili na wapinzani. Tutakuwa tunajikaanga wenyewe. Dawa hapa itakuwa ni kila mtu aitwaye mpinzani kususia Bunge Hadi Matangazo Ya Moja Kwa Moja yarudishwe.

Hii itakuwa ni aibu kubwa sana kwa CCM kuiendesha nchi kiubabe, na ukitizama kule Zanzibar ambako nao ni wenyewe, basi CCM tutakuwa tumejimaliza wenyewe
Hama chama kwani hata Kingunge alihama wewe unasubiri nini?
 
Hii ni zaidi ya kubana matumizi. Ni kuwanyima wanachi haki yao ya kujua kile wawakilishi wao wanachokiongea. Mbona vituo binafsi navyo vimezuiliwa?
Huu ni upunguani wa hali ya juu sana magufuli hawezi kushindwa kutimiza malengo yake kwa kubania wananchi kuangalia bunge.
Atafute mbinu nyingine ya kutumiza malengo yake hicho ni kitu kidogo sana na hakiwezi kumfikisha popote.
Huwezi ukawabana watoto wako ukawapa chai bila vitafunio harafu ukajiona ni mjanja.
Eti unaba matumizi.
 
Habari za asubuhi wadau,

Ni muda mrefu sana nimekuwa nikifuatlia mwenendo wa serikali mpya ya awamu ya 5 Tanzania hususani katika kusimamia haki za watanzania ikiwemo ya kupata taarifa na uhuru wa vyombo vya habari.

Kiukweli naona hoja zinapishana na sioni nguvu za wasomi wetu katika kuishauri serikali hii na kama ipo basi si ya kuzalisha matokeo chanya miaka 5 ijayo hii ni hatari sana.

Nimezipokea kwa masikitiko taarifa za kutorusha live bunge kutoka vyombo mbalimbali vya habari ambvyo vinaoperate binafsi. Na sasa watatakiwa kuchukua signals kutoka TBC ambao kwa mujibu wa taarifa nilizonazo wameanzisha studio maalum ya kurusha matangzo inayopatikana bungeni dodoma.

Lakini pia hiyo studio itarusha live sehemu/kipindi cha maswali na majibu sana. Hoja ya msingi mwanzoni ilikuwa pesa nyingi zinapotea kurusha live matangazo lakini zipo taasisi zilizotaka kufund hzo broadcasting costs still serikali inaonekna haiko interested???? Labda wanataka hizo pesa wapewe watengeneze barabara[emoji2] [emoji2] [emoji2]

Maoni yangu Rais magu anaonekna ni mpenda haki kwa watanzania je haoni watu kutopata taarifa za bungeni yanayojili kunadumiza haki? Na je uhuru wa vyombo vya habari ambavyo vilitumika kiasi kikubwa kumcampaign na kumfanya aingie madarakani vitakuwaje? TBC ni shirika la umma ambalo kamwe haliwezi kuuma serikali kwa kufuata editoral policy walizonazo.

!
!
Magufuli hapendi haki, hajawahi kuipenda na hana dalili ya kuipenda. Hii one man show inampa sifa za udikteta, ubabe na nyingine kama hizo. Binafsi naona taratiiiibuu tunaanza kufanana na Korea ya Kaskazini. Long live Magufuli. Hapa ni kazi tu katika Selikali ya viwanda.
 
unaposema magu ni mpenda haki...asingechekelea uozo wa zanzibar..
Tanzania inahitaji mabadiliko ya kweli ambayo ni ngumu kuyapata ndani ya CCM..ambako huko ni kutengeneza mfumo wa madhalimu kuitawala tanzania milele..
 
Kwani uhuru wa kupata habari ni lazima habari hiyo iwe live? Kama ni hivyo watu wasingekuwa wanachapisha magazeti na wala kusingekuwa na taarifa za habari. Wewe ukitaka bunge live nenda Dodoma ukahudhurie maana kuna jukwaa la wageni mle ndani.
 
Jana Bunge la bajeti ndio limeanza, lakini jambo la ajabu hakukuwa na msisimko wa upashaji habari wa TV stations wala radios kwa siku ya jana na Leo hata magazeti yamepotezea habari za ndani za bunge, jee wamesusia?
Hata hivyo kuna habari kuwa waandishi walikatazwa kuchukua hata picha mnato, sauti wala picha za video kwa wanahabari wakati hizo ndio nyenzo za upashanaji habari.
Hili la kuzuia aina zote za kupasha habari za bunge ni style mpya na ya aina yake Afrika, jee inakusudia nini hasa?
 
Ni vyema wakawapotezea kama hawataki wananchi wawe wanapata habari sahihi
 
Mimi ninapendekeza kama bunge limegoma wananchi tusione bunge live basi na habari zao tusiletewe na jao wanahabari watafute habari zingine watuletee habari ziko nyingi.

Wabahabari kwa pamoja waungane waache kushirikiana na Bunge.
 
Back
Top Bottom