Vyombo vya habari havitimizi majukumu yao

emalau

JF-Expert Member
Apr 25, 2009
2,775
3,100
Wadau, toka rais Magufuli aiengie madarakani kumekuwa na mabadiliko makubwa, mengine chanya mengine hasi, ukifuatilia vyombo vya habari vya nje kama CNN, BBC, CBS news na vinginevyo kiongozi wa nchi anapoingia madarakani mara nyingi vinaomba vimfanyie interview ili pamoja na mabo mengine wajue msimamo wake katika mambo mbalimbali.

Kwa sasa hivi kuna ukiukwaji mkubwa wa sheria za nchi na ukanyagaji wa katiba ya nchi, mambo mengi ambayo tumeyaweka kwenye katiba yetu kama mwongozo na sheria mama yanakanyagiwa chini, kwa mfano sasa hivi kuna kamata kamata ya viongozi wa vyama vya siasa na uvunjaji wa mikutano halali kana kwamba nchi hii si ya vyama vingi.

Pamoja na uvunjaji huu wa sheria sijaona TV wala radio imemuita rais wa nchi, waziri wa sheria na katiba wala mkuu wa jeshi la polisi kumuuliza maswali magumu juu ya uvunjaji huu wa sheria. Vyombo vimebaki kuongelea vitu vidogovidogo - trivials.

Ni wakati muafaka vyombo hivi vikaanza kutimiza majukumu yake na si kubaki tu vinajiita eti ni muhimili wa nne wa dola.

Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom