Vyeti vyangu vina gundu mnirudishie

Vyeti vyangu vina gundu mnirudishie

mwalidebe

JF-Expert Member
Joined
Mar 27, 2016
Posts
426
Reaction score
251
Kama kuna kosa ambalo wengi wamelifanya nipale mnapo tangaza nafasi za kazi na ajira kwa wananchi na kulazimika kuleta barua kopi za vyeti na utambulisho wao,halafu mwisho wa siku hamuwaajiri wala kuwapa kazi.

Sasa jambo la busara ninyi maafisa wa rasilimali watu (HR) katika kampuni zenu au mashirika yenu au taasisi zenu kwanini msiwaite kuwapigia simu wahusika ambao hamkuwaajiri waje wachukue vyeti vyao?

Badala ya ninyi kukaa navyo mwaka mzima! Mnakaaa na document za watu ambao si wafanyakazi wenu hamujawaajiri kwa malengo yapi?

Sasa niwape siri wengine kabla hawajaleta vyeti kwenu walitambika sasa kuweni makini mizimu itawatafuna ninyi hapo hadi mshike adabu

Lakini pia wale watu wakikumbuka mateso waliyopata wakati wa kuhangaika kuja kuleta vyeti soli zilivyoisha manyanyaso waliyopata inakuwa laana kwenu

Wengine ni vijukuu vya mtume sasa mnakaa na vyeti vyao mwaka watano sasa kwa malengo gani wakati kumwajiri hamna mpango naye!

Nije kwa upande wangu naombeni kila shirika au taasisi kampuni yenye kopi za vyeti vyangu mnipigie simu mnirudishie la sivyo mikosi itaawandama mpaka mshike adabu.

Nimejaribu kufuatilia wale wote wenye kopi za vyeti vyangu ambao bado mmekumbatia mnapitia changamoto kubwa rudisheni vyeti kwa wahusika kama hamjawaajili.
 
Hasira za kukosa kazi[emoji41]

tapatalk_1537519263712.jpeg
 
Hahahha nimecheka mkuu ni kopi tu we una og zako bana achana nazo shukuru umekosa usikate tamaa ya kuomba tena na tena ndio changamoto kuna siku utatoka tu
 
Back
Top Bottom