MP CHACHANDU
JF-Expert Member
- Dec 4, 2016
- 875
- 616
Baada ya zoezi la uhakiki wa watumishi hewa kuisha serikali ilitoa ahadi ya kuanza kuajiri kupitia sekretarieti ya ajira mpaka sasa hakuna ajira yeyote iliyotangazwa na sekretarieti hii tafsiri yake kuwa sekretarieti ya ajira Tanzania imekoswa kazi ya kufanya na kupelekea watumishi wake kupokea mishahara bure bila kazi maana yake kwamba kazi na majukumu makubwa ya sekretarieti ya ajira ni kutangaza kazi na kuendesha usaili kwenye taasisi za serikali ambazo zina upungufu wa watumishi malengo hayo yamekiukwa na sekretarieti ya ajira kutumia fedha za umma Bure bila kazi yeyote.
Serikali ilisema baada ya uhakiki italeta orodha ya watumishi wenye vyeti feki wote imeshindwa kuleta hayo majina inamaana hakuna ambaye alibainika na cheti feki? Kuna watumishi wa umma wengi tu wana vyeti feki na bado wanaendelea kutumikia vyeo vyao hii ni kuonyesha kuwa dhamira ya serikali ilikuwa siyo kuhakiki vyeti feki mbali kilikuwa kichaka cha kujificha ili isiajili watumishi wa umma.
Serikali Mara nyingi imekuwa ikijitokeza kusema kuwa imebaini watumishi hewa 19000, lakini imeshindwa kusema idadi ya watumishi wa umma ambao wana vyeti feki ukweli uhakiki wa vyeti feki ulifanyika kisiasa sana hakuna ukweli na umakini juu ya zoezi hilo mbali limeleta kero kwa vijana na watumishi halali wa umma mfano wa kero zilizosababishwa na zoezi hewa la uhakiki wa vyeti ,ni kusitishwa uhamisho wa watumishi ,kusitishwa kulipa madeni kwa watumishi ,kusitishwa kupanda madaraja na wale vijana 3000 walioajiriwa mwezi June 2016 kusitishiwa ajira zao wakiwemo wa mahakama nk .
Ukweli serikali imelifanya zoezi hili kuwa ni kichaka cha kujificha kutoajiri kutokana na uchumi wa nchi kuyumba moja ya dalili za uchumi kuyumba katika nchi yeyote duniani ni serikali kushindwa kutoa ajira kutoka na kufilisika.