Vyeti vya kuzaliwa - Not proof of Citizenship

Vyeti vya kuzaliwa - Not proof of Citizenship

Ghost

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2010
Posts
428
Reaction score
53
Habari zenu wakuu,

Naomba nijuze, kwanini vyeti vya kuzaliwa vinavyotolewa sasa hivi vina kipengele kinachosema: N.B: This Certificate is not proof of Citizenship?
 
Mbona watu wanapenda watoto wao wazaliwe US? Au huko ni automatic citizenship?
 
Na uthibitisho wa uraia wa Tanzania ni nini hasa?
That's the million dollar question.
Kama kweli wamekata birth certificate, cjui ni kipi sasa kinatumika kujitambulisha kama ww ni raia wa tz.
 
Na uthibitisho wa uraia wa Tanzania ni nini hasa?

1.Historical background ya ukoo,wazazi,babu,bibi n.k
2.historical background ya maisha yake na ushuhuda wa wanaoishi naye na kumzunguka kuhusu maisha yake na mahusiano yake na watanzania ni mzuri au mbaya
3.Tabia ya huyo mtu je ni ya kitanzania au ya nchi fulani
4.Uwezo wa kumudu lugha vizuri.Zamani walikuwa wakihoji hadi kilugha cha eneo analodai kazaliwa na kakulia
5.Muda alioishi Tanzania
6.Faida ambayo nchi itapata kwa kumpa huyo mtu uraia
7.Uhiari wa huyo mtu kupenda kuwa raia

Hivyo ni baadhi tu ya vinavyoangaliwa kuna mambo zingine zilizoandikwa na ambazo hazijaandikwa.Kuna vetting ambayo hufanywa na vyombo mbali mbali kabla ya kupewa huo uraia.Cheti cha kuzaliwa tu hakikupi uraia.
 
Cheti Cha kuzaliwa uthibitisha mahali ulipo zaliwa

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
1.Historical background ya ukoo,wazazi,babu,bibi n.k

Hii inakuwa corroborated kivipi?

2.historical background ya maisha yake na ushuhuda wa wanaoishi naye na kumzunguka kuhusu maisha yake na mahusiano yake na watanzania ni mzuri au mbaya

Kwa hiyo wakipatikana watu hata kitaani tu watakaosema 'aah huyu mbongo bana' inatosha kuthibitisha uraia?

3.Tabia ya huyo mtu je ni ya kitanzania au ya nchi fulani

Tabia ya Kitanzania ndo ikoje?

4.Uwezo wa kumudu lugha vizuri.Zamani walikuwa wakihoji hadi kilugha cha eneo analodai kazaliwa na kakulia

Na wale wa Kiswanglish inakuwaje sasa? Manake Kiswahili hawakimudu vizuri na Kiingereza nacho cha kuunga unga tu.

5.Muda alioishi Tanzania

Hili linathibitishwaje?

6.Faida ambayo nchi itapata kwa kumpa huyo mtu uraia

Faida inamaanisha nini hapo? Mi ni raia wa Tanzania lakini hata sijui faida yangu kwa nchi.....
 
Kuzaliwa mtoto akapewa cheti cha kuzaliwa kuna maelezo ya uraia wa wazazi wake yanawekwa kwenye cheti hicho. kwa hiyo ili awe raia ni lazima baba na/au mama awe raia ama wa kuzaliwa tz au wa kuomba kuandikishwa. Na wakati mwingine pia ili kuthibitisha kuwa baba na/au mama ni raia wa tz hutakiwa uthibitisho wa babu na/au bibi kama na wao ni raia.
 
Hii inakuwa corroborated kivipi?

Kwa hiyo wakipatikana watu hata kitaani tu watakaosema 'aah huyu mbongo bana' inatosha kuthibitisha uraia?

Tabia ya Kitanzania ndo ikoje?

Na wale wa Kiswanglish inakuwaje sasa? Manake Kiswahili hawakimudu vizuri na Kiingereza nacho cha kuunga unga tu.

Hili linathibitishwaje?

Faida inamaanisha nini hapo? Mi ni raia wa Tanzania lakini hata sijui faida yangu kwa nchi.....

anyway mwaswali unayo mengi muda wa kujibu sina naomba kawaulize uhamiaji ambao kutwa kazi yao ni kushughulikia hayo mambo.Mimi mbeba box nawahi kabla kibarua hakijaota majani
 
Mbona watu wanapenda watoto wao wazaliwe US? Au huko ni automatic citizenship?

akifika 18 years mtoto anapaswa kukana uraia wa nchi moja hvyo wengi ukana wa tz na kubaki na wausa
 
Back
Top Bottom