Unawapa neno ma agent wa ibilisi mkuuIvi vyama vya wafanyakazi havina tofauti na wabunge wa ccm kwa sababu sheria inatungwa na ccm.na inapitishwa na ccm.
Hapa hata wapinzani wagalegale bungeni wengi watapitisha baada ya kugundua hakuna hela ishaliwa na serikali ya ccm.
Mifuko karibuni yote kuna mashimo baada ya kuikopesha serikali na serikali hailipi pesa kwa wakati ni serikali ya mikopo na madeni.
Kwa ufupi PPF ishajifia, Pspf ilikuwa inaelekea ICU, lapf ilibaki kidogo kuelekea huko pia na mwenzake NSSF ndio alibaki kidogo anapumua.
Kuona ivyo wakaanza hakuna fao la kujitoa wameenda weee wakagundua sio suluhu ya matatizo yao kwa sababu hawana hela za kurejesha hata wakikaa hadi miaka 55 au 60 hawataweza kuwalipa watumishi.
La maana wakaona kwanza wapunguze mafao mbali mbali kama ya afya, uzazi nk kwa mchangiaji.
Then wakaona wakikupa 100% ya mafao watafilisika maana serikali hailipi madeni wakaona waje na sheria ya kutoa 25% ili wabaki na 3/4 ya mafao wakulipe waonavyo wenyewe yaani hela ulikuwa unakatwa kwa ziaidi ya miaka 30 bado hawakupi yote na kukaa nayo wao.
Yaani sawa benki wakukopeshe ukae nayo miaka 30 na wewe unaamua namna ya kurejesha utakavyo.
Haya maviongozi ya wafanyakazi ni makada ya ccm ndio maana huyasikii yakisema lolote maana bwana mkubwa wao kawaweka kutimiza matakwa yake.
Wangekuwa ni kinyume chake ungeshasikia wanahitwa kuhojiwa ila kwa kuwa nao wanasubiri uteuzi huwezi wasikia.
Kuna haja ya kujitoa kwenye vyama vya wafanyakazi kila mmoja ajifie kivyake.
Ila CCM NI MUUWAJI