Vyama vya upinzani vinaweza kuleta maendeleo bila kuitegemea serikali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vyama vya upinzani vinaweza kuleta maendeleo bila kuitegemea serikali

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nteko Vano, Mar 13, 2012.

 1. N

  Nteko Vano JF-Expert Member

  #1
  Mar 13, 2012
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 436
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Vyama vya upinzani vinaweza kufanya shughuli za maendeleo katika majimbo ambayo wanayashikilia bila kutegemea fedha toka serikalini. Tunaweza kupata maji ya uhakika, umeme, miradi midogo midogo katika vikundi kwa eneo husika, na kutatua kero mbalimbali zinazotupa changamoto.

  Nimejaribu kufikiria kama wananchi wameitikia kwa nguvu zote bila kinyongo kuchangia kampeni za CDM, Arumeru kumbe tunaweza kutumia mbinu hiyo na nyingine zifananazo na hiyo kufanikisha kutatua matatizo yanayotukabili. Ninajua kuna wataalam wanaweza kushauri jinsi ya kuendeleza utaratibu huo hata kama suala moja litachukua miaka mitano lakini kama litaisha itakuwa ni hatua na njia safi.

  Vyama vya upinzani vitafaidika na mpango huu kwa kuzuia CCM kwa njia moja au nyingine kutumia mbinu ya kudhoofisha maendeleo ya majimbo ambayo upinzani wanayo ili iwe tiketi ya kuombea kura mwaka 2015. Nina imani kuwa mpango huu utakuwa endelevu kwa vyama vyetu vya upinzani.

  Wana JF, naleta kwenu ili tujadili naomba kila mtu mwenye wazo lake kuhusiana na hili atoe mchango wake. Litakuwa na athari gani na tunaweza kuepuka vipi athari hasi na je, ni mikakati ipi inaweza kuwekwa ili kutimiza hili kama linawezekana.

  Nawasilisha
   
 2. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #2
  Mar 13, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,703
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  Yap! Tanx mkuu kwa kuleta post yenye akili but kama vyama vya upinzani vikendelea kuchangisha watu mpaka majimboni basi inaweza ikawa njia moja au nyingine ya kurhusu CCM kutumia mwanya huo kupandikiza propaganda chafu kuwa wananchi wasiwachague kwani eti wanawachangisha ela alafu wankula wao na familia zao, so kupitia proganda hizi zinaweza kuleta negative effects kwa upinzani Tz, so cha kufanya kwa vyama vya upinzani ni kuongeza harakati ktk kuishinikiza serkali ili iweze kutimiza ahadi, pia ni lazima ktk katiba mpya mamlaka ya munge yangeongezwa ktk swal la usimamiaji badget halmashauri ili aweze kuchochea maendeleo kwa kasi jimboni kwani yeye ndo mwenye mzigo na jimbo kuliko kiongozi yeyote yule jimboni.
   
 3. T

  Thesi JF-Expert Member

  #3
  Mar 13, 2012
  Joined: Aug 8, 2010
  Messages: 998
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Ni wazo lako lakini sikubaliani nalo hata kidogo. hatuwezi kusita kutumia fursa inayoonekana mbadala wa serikali ya kipropaganda ya ccm. Hili si wazo dogo ni wazo zito. ungesema cha muhimu ni kuhakikisha michango inayotolewa inalingana na thamani ya miradi. Lengo ni kuonyesha tofauti yetu na ccm. naomba CDM ianishe miradi inayoweza kufadhiliwa kwa njia hii kwenye majimbo ya yaliyopo sasa na majimbo ambayo mwelekeo ni mzuri kisha kuanza na vile ambavo vitakuwa vya vipaumbele wa juu. Sisi wapenda mabadiliko tutachangia pasipo kusita.
   
Loading...