Vyama vya upinzani vina siasa za maji machafu - hawataiweza CCM mpaka CCM yenyewe iamue

Shocker

JF-Expert Member
Sep 15, 2012
734
1,000
Kila nikizipima siasa za vyama vya upinzani naona, siasa zao hazina tofauti na michirizi ya maji machafu, inajipitia tu, mpaka itengenezewe misingi ndio utaona inafuata njia na hizi njia huwa zinatengezwa na CCM, yaani kama ndege basi CCM wakimwaga machicha huku utaviona vyama hivi vinaelekea huko CCM wakibadilisha na kumwaga mtama upande mwengine utaviona vyama hivyo vyote vinaelekea huko,vimegeuzwa mwanasesere.

Kwa mtindo huu CCM mpaka watake wenyewe na kuwaonea huruma ndipo wanaweza kidoogo kupata vijinafasi vya ubunge na tumeona miaka iliyopita CCM waliachia na kuwapa sehemu kubwa ya viti vya ubunge matokeo yake vikanogewa na kujiona vina nguvu saaaaaaaanaa, CCM bila ya kuchelewa wakabana, matokeo tumeyaona jamaa hawajaambulia kitu.

Huo ndio ukweli msidanganye wananchi kama mna nguvu ya kisiasa.
 
JOHNKEKE

JF-Expert Member
Mar 30, 2011
1,131
2,000
Tatizo kubwa kwa vyama vya upinzani ni kukosa demokrasia ya ndani na uongozi mbovu. Kiongozi anakuwa na tamaa ya kung'ang'ania uongozi. Anatengeneza 'kundi' lake na kulitumia kuinfluence maamuzi yeyote anayotaka.
 
Mromboo

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
2,495
2,000
Upinzani upi? Si mlikubaliana muue kabisa jamani?
Acha kutubemenda aliki aisee.
 
maIang0

Member
Jan 30, 2021
72
125
Hovyo sana ninyi CCM hamna kitu tegemeo lenu ni Nec ccm na Polisi ccm ndiyo mpate ushindi wa hila, kama mnataka levol wekeni Tume huru muone, mnajivunia ushindi wa mezani uwanjani unakwapua mpira? Mizizi gani mliyonayo viongozi mnakwapua Chadema kina Slaa, Siinde, Katambi, Gekul, Mwita, wengi tuu ni zao la chadema na Mwenyekiti Mbowe.
 
maIang0

Member
Jan 30, 2021
72
125
Tatizo siyo demokrasia ni kupata watu makini wasiopandikizi ndani ya vyama, angalia Cecil Mwambe au Sumaye wakepata uenyekiti chadema leo ingekuwepo. Fikiria watu kama Halima Mdee alikuwa Mwenyekiti wa Bawacha leo kawa Yuda Iskrariote, unadhani usipokuwa makini utapata vyama kama cha Shibuda Ada-Tadea alafub tuite tuna wapinzania. CCM hawajalala ukifanya mchezo unapandikiziwa watu na chama kinakufa, NCCR-Mageuzi wapo wapi, TLP ya Mrema mbona hauangalii kwa jicho la pili.
Tatizo kubwa kwa vyama vya upinzani ni kukosa demokrasia ya ndani na uongozi mbovu. Kiongozi anakuwa na tamaa ya kung'ang'ania uongozi. Anatengeneza 'kundi' lake na kulitumia kuinfluence maamuzi yeyote anayotaka.
 
ndomyana

JF-Expert Member
Jan 24, 2012
4,920
2,000
Kijani ushajifiàga kitambo sana sijuia kilichobaki mpaka sasa sijui ni chama au nini. Kipigo cha 2020 ilikua aibu mpaka wakamue watangazo watakacho.
 
ndomyana

JF-Expert Member
Jan 24, 2012
4,920
2,000
Tatizo siyo demokrasia ni kupata watu makini wasiopandikizi ndani ya vyama, angalia Cecil Mwambe au Sumaye wakepata uenyekiti chadema leo ingekuwepo. Fikiria watu kama Halima Mdee alikuwa Mwenyekiti wa Bawacha leo kawa Yuda Iskrariote, unadhani usipokuwa makini utapata vyama kama cha Shibuda Ada-Tadea alafub tuite tuna wapinzania. CCM hawajalala ukifanya mchezo unapandikiziwa watu na chama kinakufa, NCCR-Mageuzi wapo wapi, TLP ya Mrema mbona hauangalii kwa jicho la pili.
Apo ndio napo ikubali Chadema nahisi inawatu wengi sana ndanj ya kijani make wanastukiwa Mapema sana.
 
Kinoamiguu

JF-Expert Member
Nov 29, 2018
4,158
2,000
Kweli mpaka Ccm iamue yenyewe kuacha kuingia na mabegi mweusi yenye kura zilizopitwa tayar na TISS
 
FUSO

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
22,331
2,000
unasemea hawa hawa CCM wanaovizia na wanaopiga mitama watu wakati wa kurudisha form za uteuzi, hawa hawa wanaofunga ofisi za umma na kupotea kusikojulikana ama wengine? hawa hawa wanaotumia mapolice kuwapa kesi wagombea zisizo na dhamana hadi uchaguzi upite?

CCM ipi hasa unayoisema weye ambayo i safi ??
 
Lugatamva

Member
Feb 16, 2021
26
45
Kila nikizipima siasa za vyama vya upinzani naona, siasa zao hazina tofauti na michirizi ya maji machafu, inajipitia tu, mpaka itengenezewe misingi ndio utaona inafuata njia na hizi njia huwa zinatengezwa na CCM, yaani kama ndege basi CCM wakimwaga machicha huku utaviona vyama hivi vinaelekea huko CCM wakibadilisha na kumwaga mtama upande mwengine utaviona vyama hivyo vyote vinaelekea huko,vimegeuzwa mwanasesere.

Kwa mtindo huu CCM mpaka watake wenyewe na kuwaonea huruma ndipo wanaweza kidoogo kupata vijinafasi vya ubunge na tumeona miaka iliyopita CCM waliachia na kuwapa sehemu kubwa ya viti vya ubunge matokeo yake vikanogewa na kujiona vina nguvu saaaaaaaanaa, CCM bila ya kuchelewa wakabana, matokeo tumeyaona jamaa hawajaambulia kitu.

Huo ndio ukweli msidanganye wananchi kama mna nguvu ya kisiasa.
Ccm bila kulindwa nadola ni wepesi mno hata ukiwashindanisha na jiwe jiwe linashinda nadhani na wewe unajua ila unajipendekeza tu
 
Shocker

JF-Expert Member
Sep 15, 2012
734
1,000
Niwambie ukweli na ukweli ni kitu kinachoanika kila kitu,mmeona Uganda ? Ni sawa na hapa Tz,kiufupi CCM ina nguvu kubwa za ajabu na uzuri ni kuwa imejikita kila kona na kuna intelijensia zisizojuana,mtaiweza wapi ?

Moyo wa kuishinda CCM haujapatikana katika vyama vinavyojiita vya upinzani kidogo sana CUF ya wakati ule walijaribu na walifanikiwa ndio hadi leo as ACT wametia mguu ndani ya Serikali,wale jamaa ni wapigananji, kuliko huku kwetu kwa dizaini za akina Slaa na Mrema.

Wanabaki kukamata masanduku ya kura ambayo sie wengine tukiyaita maboya ya kuwapoteza na kuwakeep bize hivyo vyama vinavyojiita vya upinzani.

Leo eti wale wale waliokamata masanduku wameingia kwenye ubunge kimagumashi,kwa njia hizo bado sana kuishinda CCM .
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom