Vyama vya msimu vyaleta mvua kali Igunga (storm) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vyama vya msimu vyaleta mvua kali Igunga (storm)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kinepi_nepi, Sep 20, 2011.

 1. kinepi_nepi

  kinepi_nepi JF-Expert Member

  #1
  Sep 20, 2011
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 870
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Ilitolewa kauli yenye dharau, majigambo na kujiamini sana na mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi. Alisema kuna vyama vya msimu kila mwenye uelewa alijua nini alimaanisha. Kauli hazikuishia hapo, walijifanya wana safisha chama kwa kuwatosa wote wenye kutajwa kwenye kashfa za wizi, ubadhirifu, ulaghai na ufisadi wa mali ya umma.

  Leo Igunga imeonyesha CCM sio chama cha kuaminiwa hata kidogo kimekula matapishi na kimesahau mwelekeo ulikuwa kujenga chama upya chenye maadili kikifuata misingi yake ya awali.

  Nitasema kweli daima fitina kwangu mwiko, Rushwa ni adui wa haki. Cheo ni dhamana sintotumia cheo changu kwa faidia yangu, mtu bali ya wote.
  Maneno mazuri sana na yenye mvuto mkubwa, CCM ya JK imesema yakae kwanza.

  Ninasikitika sana kwani CCM imeafanya hujuma kubwa sana ya kuwanyima watanzania wengi elimu bora ya awali hivyo kuwafanya wengi kushindwa kuunganisha dots.

  CDM wananipa matumaini makubwa sana katika harakati hizi za kidemokrasia na utawala wajibiki. Kwa zaidi ya miaka 50 Igunga imekuwa kwenye utawala wa kisiasa na kiuchumi chini ya CCM, na kwa miaka kama 15 hivi chini ya money maker, king of CCM RA. Alikuwa anashinda kirahisi sana bila kupata upinzani mkubwa. CDM ilikuwa haijawahi kuweka mgombea pale, hivyo ilikuwa haina mtandao mnzuri ukilinganisha na CCM na CUF.

  Kuonyesha kuwa kasi ya kukua na kukubalika kwa CDM na makamanda wake ni kubwa sana. Leo CCM wameungana na CUF kupamabana na CDM Igunga. Vita hii inanikumbusha Ubungo. Wanawali hawa ( CCM +CUF) walipigana na Mnyika usiku kucha.

  CDM inaungwa mkono kwa matumaini na jitahada zake za kuelimisha wananchi, kama CCM wangekuwa wana watu wanafikiri hata kama mtoto wa dara la tatu wangejua kwamba wanatumia nguvu nyingi sana baada ya kushindwa kwa miaka 50. Wanachokifanya ni sawa na mwanafunzi aliyezembea kusoma kwa miaka minne akitegemea ata-make over usiku mmoja haya ndio matokeo ya kuiba mitihani yalipoanzia kama ilivyo kwenye wizi wa kura pale CCM inapoona hawawezi ku-make up.

  Elimu ya uraia na wajibu wa kiongozi ndizo sifa zitakazo mrudisha mwanasiasa yeyote bungeni au Ikulu. CCM wakiendelea kulazimisha ushindi wa mezani watatupeleka Libya, Misri, Yemen, Tunisia, Syria nk. Ukiangalia maisha ya wapiga kura wengi ni yakukata tamaa kubwa, hayana uhakika wa kesho wala kesho kutwa, ndio maana wanageuzwa na sinia au matonge mawili au matatu ya ubwabwa huu ni udhalilishaji mkubwa sana wa utu wa mwanadamu.

  Huwezi kuwa na akili timamu na mtu mwenye maadili ya kweli, na nia ya dhati ya kusaidia wananchi leo hii ukakubali kupigiwa kampeni na RA. Pamoja na kwamba anajiuza kama mtu msafi na mwadilifu ninaamini kabisa na nina shawishika sana RA, Mkapa na Dr Kafumu wamehusika vizuri kufilisi Tanzania kila mmoja kwa sehemu yake. Mkapa alimtumia Dr Kafumu kuiba na kusaidia mikataba mingi sana mibovu ya madini. RA akimtumia mwanae Ngeleja ndio walimlinda Dr Kafumu wizara ya Nishati na madini huku, Tangia enzi za akina msabaha, Karamag Dr Kafumu alikuwepo, hawa wote waliondoka na kashfa.

  Ukiwa msomi tena mwenye weledi wa maadili huwezi kubali kutumika kama mpira. Hili ndilo tatizo kubwa na mtego mkubwa tunalopata Tanzania. Wanakutumia wanakusaidia wanakubeba kisha lazima ulipe fadhila. Leo Dr Kafumu tayari kanunuliwa kwenye mtandao wa mafisadi mapapa, lazima aje kuwalipa fadhila vyovyote vile ama akirudi kwenye kitengo chake cha madini wizarani au akisaidiwa kuiba kura na kuleta maafa Igunga ili akawasaidie kuwalinda bungeni. Kuna maana gani ya kujaza hizo elimu kichwani kama unaweza kuburuzwa hata na Tambwe Hiza? Kweli elimu kubwa tena iliyopatikana kwa fedha za wauza pamba, korosho, kahawa nk inafanywa kama sandakalawe???

  Huwa inanisikitisha sana kuona hata wale ambao wangetegemewa, hutumiwa hata na wehu na wao wakakubali. Kweli leo unasaidiwa na kundi lilochafuka lote? Huna rafiki msafi hata mmoja? wewe mtu gani? Wanaokusaidia ni wale wote wenye kashfa za ubadhirifu je wewe nawe si mbadhirifu?????

  Tell me your friend and I will tell your character..................................
   
 2. Najijua

  Najijua JF-Expert Member

  #2
  Sep 20, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 1,029
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  duuh ndefu mno makala yako,ilistahili kuwa gazetini,huku ni short,precise n clear
   
 3. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #3
  Sep 20, 2011
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  tena mvua zina upepo mkali dhoruba na sasa zinaanza radi, tunaomba kasilipuke kavolkano.
   
 4. M

  Maengo JF-Expert Member

  #4
  Sep 20, 2011
  Joined: Jul 7, 2011
  Messages: 280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hujalazimishwa kusoma!
   
 5. T

  Topical JF-Expert Member

  #5
  Sep 20, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  aisee magwanda wanahangaika kujaza server...

  mbona mtaambulia aibu mkuu..taratibu mapofu yasikutoke..hii ni siasa.
   
 6. Rugaijamu

  Rugaijamu JF-Expert Member

  #6
  Sep 20, 2011
  Joined: Jul 10, 2010
  Messages: 2,833
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  <br />
  <br />
  Acha uvivu wewe...nyie ndo huwa mnaacha kupiga kura kisa eti kuna foleni kubwa kwenye kituo cha kupigia.!
   
 7. Comrade Mpayukaji

  Comrade Mpayukaji Senior Member

  #7
  Sep 20, 2011
  Joined: Sep 26, 2007
  Messages: 192
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Wewe ni walewale! unapoteza muda wako humu jamvini! watakusikiliza wakina Nape na JK!!!!!
   
 8. Alfred Daud Pigangoma

  Alfred Daud Pigangoma Verified User

  #8
  Sep 20, 2011
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,778
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Kama unatumia sana nguvu kusoma basi nakushauri ujitoe katika jukwaa hili la siasa. Huku ni Thinkers tu ndo wanakubalika!!
   
 9. MAGEUZI KWELI

  MAGEUZI KWELI JF-Expert Member

  #9
  Sep 20, 2011
  Joined: Jul 16, 2011
  Messages: 1,943
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 145
  bila shaka wewe ni arsenal......kama siye masi chelsea....amua na imekula kwako
   
 10. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #10
  Sep 20, 2011
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Mkuu wamebanu kichiz lgungu. Wameunguna lakini wapi? Binafs mwsho wa mwez mtafika hapo kucheck dakika tisi live kama kawa kulinda kura!
   
 11. chitambikwa

  chitambikwa JF-Expert Member

  #11
  Sep 20, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 3,940
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  kila siku chadema inashinda tu
   
 12. yutong

  yutong JF-Expert Member

  #12
  Sep 20, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 1,604
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  They saw it coming! Hata sunami wakati inakuja waliiona lakini wakadharau kilichofuata ni kilio, CCM wanaviita vyama vya msimu lakini ndo vinawamaliza wanahaha sasa hivi huko igunga na watahonga mpaka wake zao huko
   
 13. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #13
  Sep 20, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  sio muda mrefu nao tutawaita wanachama wa msimu maana hii liko mbioni sio wazee ving'ang'anizi bali ni vijana wenye maono ya nini kinafanyika na nini wafanye
   
 14. m

  mwinukai JF-Expert Member

  #14
  Sep 20, 2011
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 1,448
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  HATA GADAFI aliwaita wapinzani wake panya lakini alichokipata ckinafahamika kwa hao panya.
   
 15. kinepi_nepi

  kinepi_nepi JF-Expert Member

  #15
  Sep 20, 2011
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 870
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Huo uvivu wa kusoma nusu ukurasa ndio unatupelekea kusaini mikataba mibovu kwani mnaona tabu kusoma kurasa......... Magamba wavivu kwa kila kitu
   
 16. bemg

  bemg JF-Expert Member

  #16
  Sep 20, 2011
  Joined: Apr 25, 2010
  Messages: 2,706
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  ni mvua za mafuriko CCM na siasa zao uchwara na mipasho yao wananchi wameshaamuka hakuna kulala tena hadi kieleweke
   
 17. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #17
  Sep 20, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Safi sana watabana mwisho wataachia. Mie ntaungana nanyi 30th kuja kumuangusha magamba
   
 18. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #18
  Sep 21, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  mapambano bado yanaendelea na ukombozi bado tunasafari ndefu maana tutasikia mengi sana mwaka huu
   
 19. K

  Kikwebo JF-Expert Member

  #19
  Sep 21, 2011
  Joined: Aug 25, 2006
  Messages: 352
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Hivi hawa ndio wasomi wa CDM... licha ya kulipwa kuja kuandika habari za CDM lakini hata kujenga hoja hujui. Umekiri kama CDM haikuwa na mtandao mzuri Igunga ... na hapo hapo unashutumu vyama vingine kuwa ni vya msimu. Mimi nadhani nenda kajifunze kujenga hoja kabla hujaleta uaro wako hapa..
   
 20. Lukansola

  Lukansola JF-Expert Member

  #20
  Sep 21, 2011
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 5,456
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Yeah tha' was loud and clear Quad.
   
Loading...