Uchaguzi 2020 Vyama 8 vinavyoshiriki Uchaguzi vyamtaka Mbowe ajieleze kwa Msajili baada ya kuviita ni vyama bandia

Ketoka

JF-Expert Member
Sep 23, 2015
1,087
1,913
Vyama 8 vimemtaka Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe kuomba msamaha kufuatia kauli aliyotoa hivi karibuni kuwa vyama vingine ni vyama bandia.

Vyama hivyo vimesema Mbowe amevidhalilisha na amevunja sheria na huku vyama hivi vimesajiliwa kama kilivyosajiliwa CHADEMA.

Wamekitaka CHADEMA wajitoe kwenye uchaguzi kwani wamekata pumzi na watabaki vyama 14 vyenye wagombea machachari akiwemo Mwanamama Queen.

------
Muungano wa vyama vinane vya siasa vinavyoshiri Uchaguzi Mkuu, vimemtaka Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, amuite Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, ajieleze kwa madai kuwa ameviita vyama hivyo ni bandia.

Makatibu wakuu wa vyama hivyo, wametoa msimamo huo wakati wakizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Vyama vilivyokutana na kutoa tamko hilo ni ADC, NRA, DP, UMD, SAU, UPDP, Demokrasia Makini na AFP.

Makatibu hao walisema Mbowe alisema vyama hivyo ni bandia, kwa kuwa kupitia Tume ya Maadili ya Uchaguzi vilipitisha azimio la kusitisha kampeni za mgombea urais kupitia Chadema, Tundu Lissu baada ya kukiuka kanuni na taratibu.

Kiongozi wa Muungano huo ambaye ni Katibu Mkuu wa Chama cha Democratic (DP), Abdul Mluya alisema kauli hiyo ni sawa na udhalilishaji kwa vyama hivyo, vilivyoundwa kwa mujibu wa sheria na taratibu.

"Mbowe ametukosea sana adabu sisi kama viongozi wa vyama hivi lakini pia wanachama wetu, kwa kauli yake kuwa vyama vyetu ni bandia, kauli yake hiyo haivumiliki na zaidi imelenga kutuchafua mbele ya wanachama wetu na taifa kwa ujumla" alisema Mluya.

Alisema kauli hiyo na nyingine kuwa vyama hivyo vinatumika kisiasa wakati huu wa Uchaguzi Mkuu ni sawa na matusi kwa vyama hivyo. Alisema vyama hivyo vinahoji Mbowe anapata wapi kiburi cha 'kuwatukana' hadharani.

Mluya alidai kuwa Mbowe na viongozi wengine wa Chadema, wanaonekana kukosa hoja za msingi hasa wakati huu wa harakati za Uchaguzi Mkuu.

Aliomba watanzania wanasubiri kuona Msajili wa Vyama vya Siasa, anatoa adhabu kali kwa Mbowe na Chadema ili iwe fundisho kwa wenye tabia kama hiyo.

Katibu Mkuu wa Chama cha Wakulima (AFP), Rashid Rai alisema umefika wakati kwa watanzania kuipima Chadema na viongozi wake, hasa kutokana na kauli za mara kwa mara zinazoashiria uchokozi wa kisiasa.

Alidai kuwa si mara ya kwanza kwa viongozi wa chama hicho, kutoa kauli za uchochezi na kuvunja umoja. Aliwataka wananchi wakiepuke ili taifa lisipoteze amani.

Rai alisema Chadema wameona uchaguzi umekuwa mgumu kwao; na ndiyo maana wameanza kuleta chokochoko kuuharibu, kama ambavyo wamekuwa wakionekana wakinadi sera majukwaani

"Ukiangalia tabia zao, mienendo yao utaona kabisa kuwa wamepoteza dira, hivi vyama ni halali kisheria na mahali pote ambapo wao wapo hivi vyama, pia vipo na vyote vinafanya kazi kisheria. Iweje watuite kuwa sisi ni vyama bandia" alihoji.

Rai alisema vyama hivyo, vinafanya kazi kwa utaratibu wao na si kufuata yale ambayo Chadema wanayataka. Aliitaka Chadema kutambua kuwa vyama vya siasa ni mali ya wananchi na ndiyo wanaohusika kuchagua.


My take: Hivi kweli hivi vyama vidogo vina strategies yoyote katika kukuza vyama vyao au ni wasindikizaji wa siasa hapa Tanzania hasa kwenye uchaguzi?
 
Vyama 18 vimemtaka mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe kuomba msamaha kufuatia kauli aliyotoa hivi karibuni kuwa vyama vingine ni vyama bandia

Vyama hivyo vimesema Mbowe amevidhalilisha na amevunja sheria na huku vyama hivi vimesajiliwa kama kilivyosajiliwa CHADEMA...
Vyama 18? Hebu tutajie ni vyama gani mkuu!!
 
Atawatolea maelezo yao Polepole kesho maana naona siku hizi ndio amejipa jukumu hilo.
 
Mbowe haombi msamaha kwa chama chochote kile hata maccm. Waambie hao vibaraka wa maccm WARIE TU. Tusi kubwa.
Asipoomba radhi ni dhahiri CHADEMA viongozi wake waishi kwa jina la chama. Haihitaji elimu ya siasa kutabiri athari ya kauli hiyo wakati huu wa uchaguzi.

Kwamba hata wagombea wa chama badala ya kunadi Sera wanawashambulia kwa kuwadharilisha wagombea wa vyama vya siasa. Hili likuwa halali wakati wa mfumo wa chama kimoja (Sera, Itikadi na Imani na ya chama kimoja). Katika mfumo huo mshindi ni yule aliyeweza kujisifia na kumponda mwenzake.

Kwenye mfumo wa vyama vingi, pamoja na sifa za mgombea, nguvu ya chama chake (kwa maana ya Sera) ndiyo huvutia wapiga kura.

Hivyo basi, CHADEMA, inajiondoa yenyewe kwenye kuaminiwa na wapiga kura.

MWANA KULITAFUTA MWANA KULIPATA
 
Kwani ni Mbowe tu, hata CCM wanalijua hilo kuwa inawaendesha kwa vijisenti. Badala ya kumlaumu Mbowe vijitoe kwenye mifuko ya koti la CCM.
 
Back
Top Bottom