Vyakula na life style katika umri wa 40+

Mayu

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2010
Posts
8,674
Reaction score
14,356
Kwa uzoefu wangu mdogo nimebaini Watanzania wengi sana tunapofikisha miaka around 40 tunaanza kupata changamoto nyingi sana za kiafya zinazo weza kuzuilika kutokana na life style zetu.

Ukiachana na kutofanya mazoezi swala la ulaji na aina ya vyakula tunakula lina beba taswira kubwa sana ya changamoto za maradhi kadiri umri unavyokwenda.

Lakini pia kuna swala la kutokufanya mazoezi na mentality za kustaafu zina fanya wastaafu wengi sana kufa mapema au kwa mateso kwa changamoto za kiafya zinazo zuilika.

Naamini hapa JF wapo wataalamu lakini wapo pia ambao wanajua mambo haya kupitia uzoefu nk
Nimatarajio yangu watatujuza mambo haya muhimu tuyaepuka tufurahie uzee wetu.

Karibuni kwa madini na nondo zaidi.
 
Sukari na pressure na heart attack inaweza kuzuilika Kama tukizingatia lifestyle nzuri.

Kula kiasi kidogo usile ukashiba Sana...kwa mfano chapati mbili na bakuli la choroko inatosha kbs..nyama sio nzuri..pendelea sana maziwa mtindi.

Ugali na wali haufai...matembere na kabeji NI mboga nzuri sana..matunda mazuri kbs duniani NI tikitimaji na tango.

Kumbuka kunywa maji Lita zaidi ya nne kwa siku.mazoezi ya kukimbia na ya kutoa jasho NI mazuri...epuka pombe sio nzuri sana
 
Asanteni Mungu awabariki kwa ushauri huu mzuri
Nadhani thread hii idumu kwa ushauri na maelekezo
 
Punguza nyama ongeza mboga za majani, maharage na matunda.

Maji litre mbili kwa siku. Tembea hata kwa nusu saa kila siku.

Punguza pombe

Kama utaweza breakfast pata ndizi mbivu, papai na mayai mawili ya kuchemsha

Lunch ukiweza kupata samaki mzima na mboga mboga

Jioni vijiko viwili vya wali unajazia maharage juu.
 
Mh
Mh,ntaweza kweli hivi mimi!!
 
Daah hapo kwenye kupunguza pombe sasa , mi bila tubia tuwili kwa kweli silali. mazoezi nafaya sana na tayari nimegonga 45. Mungu atusaidie tustaafu na afya zetu
 
Mbona Babu zenu walikuwa wanakula tena nyama mbichi na waliishi miaka mingi tu-hayo ya kutokula nyama wewe umeyatoa wapi?
 
Huyu dingi ana miaka 71 ona alivyo.
Anakwambia kula mlo mmoja kwa siku, usile vyakula vya kukaanga, pendelea choma na chemsha.

usinywe soda wala juice za kopo, kula matunda natural.
 
Vijiko viwili vya wali???? Mbona ntakuwa nalala na njaa kila siku!!!
Im a big fan wa "i love to eat diet " hiyo sukari na pressure mungu tu anisaidie , natembea 3km wastani kila siku , na maji nakunywa 4 plus litters per day
 
Vijiko viwili vya wali???? Mbona ntakuwa nalala na njaa kila siku!!!
Im a big fan wa "i love to eat diet " hiyo sukari na pressure mungu tu anisaidie , natembea 3km wastani kila siku , na maji nakunywa 4 plus litters per day
Kwakweli tena ukute wali wa nazi
 
Huyu dingi ana miaka 71 ona alivyo.
Anakwambia kula mlo mmoja kwa siku, usile vyakula vya kukaanga, pendelea choma na chemsha.

usinywe soda wala juice za kopo, kula matunda natural.
Maisha hayana formula mkuu na yapo very brutal for those who plan for it.
Corona imeua sana first class pattients , hohehae wengi wame survive,

A 109 years old ww2 us veteran , alifariki akiwa na miaka 112 , a pack of 20 cigarates was his daily dose ,
 
Huyu dingi ana miaka 71 ona alivyo.
Anakwambia kula mlo mmoja kwa siku, usile vyakula vya kukaanga, pendelea choma na chemsha.

usinywe soda wala juice za kopo, kula matunda natural.
Kuna mmoja nilikutana nae kazini ni dada wa Kijamaica, anasema alianza tangu akiwa na miaka 30 aliacha pombe, vyakula vyake anakula organic tu matunda mengi, samaki na mboga mboga, aliacha kunywa chai na kahawa anakunywa chai ya mchai chai tu.
Ukimuona ni kama ame baki pale pale 30 ingawa sasa ana 60.
 
Ona huyu babu ana miaka 92 anapiga mazoezi ya kutosha.

Babu anasema hataki kuugua ugua magonjwa ya kijinga kwani hataki kua mzigo kwa watu wengine.

 

Bandiko hili la mdau nimelielewa sana [emoji116][emoji116][emoji116]

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…