Vuta picha vyama vyote vya upinzani vifutwe ibaki CCM pekee

trust me maisha yataenda ka kawaida maana hata huko CCM upinzania utaibuka na kutakuwa na vita ka tuvionavyoleo maana hata kabla ya vyama vingi kulikuwa na maisha ka hayo
 
Kwani kabla ya upinzani Nchi ilikuwaje?
Huko China kuna vyama vya upinzani?

Ni heri upinzani huu wa kutetea matumbo yao,kujimilikisha Ardhi,kutetea ufisadi ,kussuport ushoga na utegemezi wa misaada ...Ni bora ufe kabisa ili tupate vyama mbadala vyenye Sera zinazoeleweka.
Usifananishe China na takataka zingine.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Anaandika #GODBLESS_LEMA (MB) Arusha

Vuta Picha Vyama vyote vikafutwa katika kipindi hiki kikabaki CCM tu chama ulichonacho wewe.

Then hao uliokua unawaona hawafai akina Mbowe, Mdee, Heche, Nassary, Lema n.k wakaona ni UJINGA KUFA unatetea watu wasiojua kujisaidia wenyewe. Wakajiuliza Kwani tunakwama wapi? Acha na sisi tukaungane na CCM mtesi wao na sisi tuishi vizuri tu.

Then Wabunge wote katika Majimbo yote wakatokea CCM kila kitu kikaamuliwa ndani ya Chama.

Mbowe akasaidiwa kujenga Bilcanas mpya maisha yakaendelea kama tunavyoona watu wanasamehewa kubomolewa nyumba zao wakijiunga na CCM.

Mbowe, Mnyika, Lijualikali tayari wanatambulika na system ya Uongozi hapa nchini. Kama DC wa Dodoma anaejitambua kama karai amepata vipi hawa wenye makarai yao watakosa?

Then fikiria wewe Mtanzania wa kawaida utaishije na atakusaidia nani tena kuhoja kuhusu pesa yako?

Kama walipokuwepo watu wa kuhoji pesa yako bado walikua watu wanakula kwa kujificha japo kweli zinaliwa. Vipi wakikosekana?

Hivi mshawahi kufikiria madhara ya hizi Juhudi za Kudhoofisha Upinzani au huwa mnashangilia tu?

Mtaishi kama "Mbwa Koko" na hutatambulika tena kama mfuasi wa CCM watatambuana viongozi kwa viongozi. Who is going to deal with you?

Leo Viongozi wa CCM wanawanyenyekea kidogo wananchi ni kwa sababu wanajua kuna Uchaguzi awamu ijayo.... Na Pengine Jimbo likaenda Upinzani. Ikibaki CCM pekeake nani atakunyenyekea wewe? Nani atakuja kujua hata unaishije?

Mshafikiria?

Hamtamuona Polepole tena! Anakuja kueneza nini? Watakua ofisini tu wakilipana mishahara. Watawachagulia kila kitu na hakuna cha kuwafanya.

Mshafikiria?

Ni ngumu kuelewa kwa kuwa haijatokea na mnaangalia leo tu.

Huwa natamani hii hali itokee hata kwa muda wa mwezi mmoja tu.

Mtakopwa hadi mishahara mtasema wapi? Nani atawapigania kipindi hicho hata kina Lissu wanakula mema ya nchi tu.

Hicho ndo kipindi hata ajira mpya kuna zingine itabidi wapate kwanza watoto wa viongozi na wengine mtapata zitakazobakia.

Hicho ndo kipindi mtapigwa hadi fimbo makazini, nadhani Dalili za Makofi zimeanza na hakuna wa kuwatetea.... Ukienda kushtaki makahamani unawakuta wale wale. Unapeleka kesi na unafungwa wewe. Wa kupiga kelele itakua ni familia yako tu wengine wote wanaogopa.

Akina Mbowe kipindi hicho watakua wanakula kuku kwa mirija tu.

Mtawaita na hawataitika tena. Ipo sababu kubwa sana ya Kuilinda Demokrasia na vyama Vya Upinzani. Walioianzisha na Kuitetea kwa Damu hawakua wajinga they focused on their future.

Hatubembelezani hapa kuilinda demokrasia ya kweli maana kesho ni yetu sote.

Kila Unachotaka kukishabikia kipime kwanza madhara yake ya baadae.

Watu mnatamani vyama vya Upinzani vyote vife au vifutwe ila ipo siku mtavililia na hamtavipata.

Tafakari

Siku njema

Sent using Jamii Forums mobile app
Mlikuwa Wapinzani, mkaingia kwenye uanaharakati na sasa mko kwenye matusi..!
Namna hii hatujui baada ya matusi upinzani utaelekea wapi kama sio kulaumiana na mwisho kufutika kabisa..!
Upinzani ulikuwa ule wa Dr Slaa, wa kujenga hoja na kutumia akili sio huu wa Lema, Heche na watu wa aina hiyo.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom