Vurugu za wachimba kokoto zafunga barabara kigamboni

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,320
33,125
Baadhi ya vijana waliotiwa nguvuni na polisi katika vurugu hizo. ..Vijana hao wakiwa kwenye Difenda tayari kuelekea kituo cha polisi.]
Eneo linalochimbwa kokoto lililosababisha vurugu hizo.

WACHIMBA kokoto eneo la Kigamboni Maweni, leo wamezua vurugu baada ya kufunga barabara na kuchoma mataili kutokana na kuzuiliwa kuendelea kuchimba kokoto eneo hilo wakati wananchi wenye asili ya Kihindi wakiruhusiwa kuchimba. Polisi walilazimika kuingilia kati huku wakitumia mabomu ya machozi ili kutuliza ghasia hizo.

Global Publishers

==========
UPDATE
==========
MziziMkavu! Nashukuru kwa picha za tukio hili. Suala nimelifikisha katika taasisi husika. Natumai hatua za haraka zitachukuliwa katika kuhakikisha wananchi wanapata fursa ya kuuza mizigo yao iliyopo machimboni na pia utaratibu mzuri kuwekwa ili wachimbaji hawa wadogo waendelee kupata kipato cha kujikimu wao na familia zao.
UPDATE: Wananchi wameruhusiwa kuendelea na shughuli zao za uchimbaji kokoto na mchanga katika eneo la Mjimwema.
 
Attachments

  • WACHIMBAKOKOTO1.JPG
    WACHIMBAKOKOTO1.JPG
    61.1 KB · Views: 86
  • WACHIMBAKOKOTO2.JPG
    WACHIMBAKOKOTO2.JPG
    51 KB · Views: 96
  • WACHIMBAKOKOTO3.JPG
    WACHIMBAKOKOTO3.JPG
    49.2 KB · Views: 77
  • WACHIMBAKOKOTO4.JPG
    WACHIMBAKOKOTO4.JPG
    43.9 KB · Views: 487
  • WACHIMBAKOKOTO9.JPG
    WACHIMBAKOKOTO9.JPG
    31.6 KB · Views: 85
  • WACHIMBAKOKOTO17.JPG
    WACHIMBAKOKOTO17.JPG
    68.3 KB · Views: 91
  • WACHIMBAKOKOTO15.JPG
    WACHIMBAKOKOTO15.JPG
    62 KB · Views: 72
  • WACHIMBAKOKOTO14.JPG
    WACHIMBAKOKOTO14.JPG
    43.8 KB · Views: 79
  • WACHIMBAKOKOTO13.JPG
    WACHIMBAKOKOTO13.JPG
    63.7 KB · Views: 62
  • WACHIMBAKOKOTO12.JPG
    WACHIMBAKOKOTO12.JPG
    53.4 KB · Views: 64
  • WACHIMBAKOKOTO10.JPG
    WACHIMBAKOKOTO10.JPG
    46.2 KB · Views: 70
MziziMkavu! Nashukuru kwa picha za tukio hili. Suala nimelifikisha katika taasisi husika. Natumai hatua za haraka zitachukuliwa katika kuhakikisha wananchi wanapata fursa ya kuuza mizigo yao iliyopo machimboni na pia utaratibu mzuri kuwekwa ili wachimbaji hawa wadogo waendelee kupata kipato cha kujikimu wao na familia zao.
 
Kigamboni kuna laana gani!!?
Ardhi imeuzwa kwa wamarekani.
Machimbo ya kokoto yameuzwa kwa wahindi.
Tanzania ni nchi pekee inayothamini wageni na kuwatesa raia wake.
Waliosema bora kuzaliwa mbwa Somalia kuliko binadamu Tanzania hawakukosea
 
MziziMkavu! Nashukuru kwa picha za tukio hili. Suala nimelifikisha katika taasisi husika. Natumai hatua za haraka zitachukuliwa katika kuhakikisha wananchi wanapata fursa ya kuuza mizigo yao iliyopo machimboni na pia utaratibu mzuri kuwekwa ili wachimbaji hawa wadogo waendelee kupata kipato cha kujikimu wao na familia zao.
huna lolote bwana mlikuwa wapi mpaka haya yote yanatokea mnaturaharibia nchi na uchu wenu kama sio wa wenzenu.
 
MziziMkavu! Nashukuru kwa picha za tukio hili. Suala nimelifikisha katika taasisi husika. Natumai hatua za haraka zitachukuliwa ...
Mheshimiwa Mbunge, tufikishie ujumbe kwa Prof Tiba, ikiwa hao wachimbaji 3,000
tu wamewatoa jasho Polisi, siku Wana Kigamboni ambao tumezuiwa kuendeleza maeneo yetu kwa miaka 4 tukiinuka kusema enough is enough wataweza wapi?
Jirani zangu wameshaanza kuendeleza maeneo yao wamechoka, siku sote tukichoka itakuwaje?
 
Wimana,
Nadhani hilo wanalijua kwamba Wananchi wa Kigamboni ni wastaarabu lakini ni wakali pale wanapodai haki yao ya msingi.
Kuendeleza eneo lako ni haki yako ya msingi na unalindwa na sheria. Endeleza kama una uwezo. Kisheria, zuio la kutoendeleza halipaswi kuzidi miaka miwili. zuio la kisheria liliisha 2010.

Ni Vyema mkaisoma na kuielewa vizuri sheria ya Mipango Miji na.8 ya 2007. Bila hivyo haki zenu za msingi zinaweza kupokwa.
 
Wimana,
...

Mbunge wangu asante kwa ushauri, fursa zilizuiliwa muda mrefu sana.
Nasikitika umekuwa Mbunge kwenye kipindi kigumu kuliko Magoba na Mwichumu.
 
Back
Top Bottom