Vurugu Umbwe-Lyamungo: Miaka 12 baadae

Wale wa umbwe tujikumbushe kidogo shule yetu.
Screenshot_20221211-141541.jpg
 
Nakumbuka tu jina Feruzi, alikuwa mweusi na lips flan nyekundu. But alikuwa Day, kama ni huyo namkumbuka.
Kina Andrew kimboka na Buruani Mtali Mushi na Jabri Mushi uliwaacha sio

Yule Dada Matata wa Day Eutropia Mushi unamkumbuka au ndio shemeji yetu alikuwa?
 
Mwl mbise
Weeeee, mwalimu Mbise alifariki muda mrefu sana.

Alipata uvimbe tumboni ukawa sababu ya kifo chake. Alitufundisha English kuanzia form one mpaka four. Apumzike kwa amani Mwl Mbise. Mr Kapinga nae alishafatiki pia. Alikuwa anafundisha B/K na commerce
 
Weruweru na Machame girls watoto weupee 😋😋
Subiri kwanza....

Mimi ndiye Legend sasa.

Nimesoma Umbwe, nimesoma Machame...

Tukiwa Machame tulikataa kucheza disco ya Lyamungo, tukacheza na Umbwe.
Lyamungo wakatishia kutuchapa viboko tukifunga shule.

Tumefunga shule tukaogopa kuondoka shuleni maana walisema wanatusubiri pale mashine tools.

Lolest, ilibidi walimu wasindikize magari mpaka Moshi mjini.

Tulikuwa na hekaheka jamani
 
Leo nimeamka na kuwaza kwa machungu sana na maumivu moyoni nikikumbuka vurugu zilizotokea kati ya shule niliyokuwa nasoma Umbwe Sec na Lyamungo Sec 2009, vurugu zilizoacha vifo, majeraha na uharibifu. Shule mbili zilizopo katika wilaya mbili tofauti (Moshi Vijijini na Hai), zilizopo katika jamii mbili tofauti za wachaga zilizokuwa na mgogoro miaka ya nyuma (Wakibosho na Wamachame), Umbwe sec ikiwa na idadi kubwa ya vijana kutoka Arusha, Kilimanjaro, Singida, Manyara, kanda ya juu kusini, kanda ya ziwa kwa uchache ...Wakati Lyamungo ikiwa na idadi kubwa ya vijana kutoka Mara, mikoa mengine ya kanda ya ziwa, Arusha, Manyara Kilimajaro kwa uchache

Mzozo ulianza Umbwe Sec tulipoenda kucheza mechi na Lyaskika, shule ya kata iliyopo karibu na Lyamungo. Vijana wa Lyamungo walikuja kuishangilia shule ya lyaskika, wakiwa kwa uchache, kulianza mvutano wa maneno kati ya vijana Lyamungo na Umbwe. Kutokana na wingi wao, Vijana wa Umbwe waliweza kuwapelekesha vijana wa Lyamungo. Vijana wa Lyamungo waka-organize na kurudi shuleni kwao ambapo walienda kuwakusanya wenzao waliobaki shuleni na kurudi uwanjani wakiwa na mafyekeo, fimbo..etc. Walikuja kwa kwasi sana wakiwa na silaha. Hii ilwapelekea vijana wa Umbwe kukimbia hoe hae, wengine kwenye mashamba ya mahindi na coffee. Wachache waliweza kufikiana na kuanza kupigana huku vijana wa Lyamungo wakiwa na advantage kutokana na silaha zao. Katika harakati za mapigamo, kijana mmoja wa Lyamongo alizungushiwa waya ya senyenge shingoni na vijana wa Umbwe na kuivutia shingoni hadi ikatoka na nyama za shingoni.

Vijana wa Umbwe kwa kukimbia waliweza kurudi shuleni, tukiwa katika jaziba na hofu kuwa vijana wa Lyamungo wanaweza kurudi, wale ma-brother wakubwa walitupangia mawindo ya usiku kwa makundi kila kona ya shule. Na story kubwa iliyokuwepo ni kuwa ikifika asubuhi na mapema tunatakiwa kwenda kuwavamia Lyamungo shuleni kwao. Asubuhi ilifika kila mtu akiwa na silaha, tukiwa tumevalimia vitambaa vyeupe kichwani ili tutambuane na kupeane code names ili tusiweze kushambuliana kimakosa. Tukaanza safari, nakumbuka tulipita sehemu na mama mmoja alikuwa akipalilia shambani akaanza kulia na kutuomba tusiende ila vijana hatukuelewa tukazidi kwenda.

Tulipofika shuleni Lyamungo tukaingia kwa kasi sana na kuanza kuwashambulia vijana wa Lyamungo na kuharibu miundombinu yao. Nakumbuka kuna jamaa alikuwa akitumia kombeo alimlenga kichwani jamaa mmoja aiyekuwa ana piga mswaki dirishani. Tulifanya shambulizi kwa kasi sana na kurudi shuleni ambapo tulikuta polisi wameshafika shuleni Umbwe na tukakalishwa chini wote. Bila mategemeo wala kudhania, tukapata taarifa kuwa kuna mwanafunzi mwenzetu amefariki kutokana na kupigwa na wanafunzi wa Lyamungo. Maan, my whole world collapsed....baada ya siku kadhaa pia tukapata taarifa kuwa yule mwanafunzi wa Lyamungo aliyezungushiwa waya ya senyenge shingoni amefariki dunia.

Zile nyakati ni moja ya kati vitu vigumu vilivyowahi kutokea maishani mwangu. Nikikumbuka jinsi yule mama wa yule kijana aliyefariki alivyofika shuleni na kuanza kuangua kilio pale administration block, huwa naumia sana. Nikimfikiria kijana wa lyamungo aliyezungushia senyenge na baadae kufariki naumia pia. Nafikiria zaidi kuhusu familia zao, mategemeo waliyokuwa nayo juu yao.

12 years later, bado moyo wangu ni mzito, kama bado haukuwahi ku-experience vita usiombe iweze kutokea katika mazingira yako.

May the Lord grant us his Mercy.

Huwa napenda ku-reference hii ishu na nyimbo ya Dr Dre ft Snoop Dogg - Lil ghetto boy

Ilikua ni noma
 
Back
Top Bottom