Vurugu St. Mathew's Sekondari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vurugu St. Mathew's Sekondari

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Congo, Feb 18, 2010.

 1. Congo

  Congo JF-Expert Member

  #1
  Feb 18, 2010
  Joined: Mar 13, 2008
  Messages: 1,312
  Likes Received: 604
  Trophy Points: 280
  Mwishoni mwa wiki iliyopita kulitokea vurugu kubwa shule ya Sekondari St. Mathew's kule Kongowe. shule hii inamilikiwa na bwana Mtembei. Sababu ya vurugu hizi ni vijana waliomaliza kidato cha sita waliokuwa wanadai fedha zao za "caution money". Kiasi cha shilingi 30,000 kila mmoja. Walipoufuata uongozi wa shule (na hatimae mwenye shule) wakanyimwa fedha hizo. Vurugu hizo zilisababisha Polisi kupelekwa pale shuleni na mpaka leo wako pale. Pia masomo ya shule nzima yamesimama kwa maelezo kuwa walimu walichomewa vifaa, vitabu na madaftari yao ya kufundishia. baadhi ya wanafunzi wamechukuliwa na wazazi wao kwa kuwa hakuna maji na chakula kinachelewa kupikwa.
  Cha, ajabu, sikuona chombo chochote cha habari kikiripoti habari hiyo. Habari leo waliripoti Jumatano ukurasa wa tatu. Najiuliza, ilikuwaje vyombo vingine vya habari visiripoti habari hiyo?
  Suala la kurudishiwa "caution money" kwa mwanafunzi aliyemaliza shule ni haki yake ili mradi tu awe hakufanya uharibifu wowote wa vifaa vya shule kabla. Vipi hawa wanyimwe mpaka kutokee mzozo uliosababisha vurugu?
  Labda kuna mwenye habari zaidi na majibu mwafaka.
   
 2. Mgeninani

  Mgeninani Senior Member

  #2
  Feb 18, 2010
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 190
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Skuli nzuri wanaitia doa, makubaliano ni nini kama hiyo caution money ni refundable basi wanatakiwa warudishiwe kama siyo (non-refundable) basi, waangalie kwanza kwani kudai ndo mpaka vurugu? waache ushamba
   
 3. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #3
  Feb 18, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 368
  Trophy Points: 180
  Mutembei yupi; toa jina kamili kama umeamua kutaja majina bwana kutuepushia ma_uncles usumbufu!
   
 4. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #4
  Feb 18, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,831
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  cha kusikitisha ni kwamba wazazi na walezi ndio wanatoa hela lakini watoto wanapigania hiyo pesa!! mob psychology inaharibu sana watoto

  kwani zililipwa kwa vurugu? there could be a better way to claim the money
   
 5. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #5
  Feb 18, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  caution money huwa hazirudishwi hata siku moja hapa kwetu Tanzania.Sijui huwa zinapelekwa wapi?
   
 6. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #6
  Feb 18, 2010
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,476
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Hivi mnajua bora mmenikumbusha nami nenda dai yangu japo ni miaka lukuki- by that tme sie tulikuwa tunalipa tu bila hata ya kupewa maelezo zaidi ya pesa ya kinga shilingi 5,000/= Laiti ningekuwa nimeiona ile 'refundable'
   
 7. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #7
  Feb 18, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,834
  Likes Received: 249
  Trophy Points: 180
  Kama walifanya uharibifu hapo ni "bila-bila" - caution Money imepata matumizi - sidhani kama kuna kudai tena!
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...