Aliyoyasema Rais Samia alipokuwa kwenye ziara maalum katika shule ya Sekondari Benjamin William Mkapa

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,863
930


ALIYOYASEMA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHESHIMIWA SAMIA SULUHU HASSAN ALIPOKUWA KWENYE ZIARA MAALUM KATIKA SHULE YA SEKONDARI BENJAMIN WILLIAM MKAPA, DAR ES SALAAM.

MACHI 7, 2022.

Nichukue nafasi hii kuwashukuru uongozi wa Mkoa, Wizara na Shule kwa shughuli ya kunishtukiza mlioifanya Januari mwaka huu, wakati naadhimisha siku yangu ya kuzaliwa. Shughuli ile ilinipa faraja kubwa na kujua kwamba Walimu na Watoto wangu, wananikumbuka na wapo tayari kunienzi.

Nimefurahi sana kuwaona wanangu, na nashukuru sana kwa mapokezi makubwa mliyonipa. Ujio wangu hapa ni utekelezaji wa ahadi niliyoitoa wakati nilipozungumza nanyi kwa njia ya simu, kwamba ningefika kukusalimieni, nimekuja kutimiza ahadi yangu.

Nawapongeza sana walimu kwa kazi kubwa mnayoifanya ya kutoa elimu na kwalea watoto wetu katika maadili mema. Nafahamu katika shule hii ya Sekondari Benjamin Mkapa na Shule jirani ya Sekondari Uhuru Mchanganyiko pamoja na Shule ya Msingi Uhuru kuna wanafunzi wenye mahitaji maalum kutokana na changamoto za kimaumbile walizonazo.

Serikali inatambua changamoto wanazokabiliana nazo, watoto wenye mahitaji maalum nchini kote ndio sababu Serikali inahakikisha inaweka mazingira mazuri ya kujifunzia na kufundishia ili kila Mtanzania anufaike na fursa za Elimu kwa manufaa yake binafsi na taifa kwa ujumla.

Serikali imeendelea na mkakati wa kitaifa wa elimu jumuishi wa 2021/22 hadi 2025/26 ambao utazingatia elimu jumuishi kwa ngazi zote za elimu kuanzia elimu ya Awali, Msingi, Sekondari, Walimu, Vyuo vya Ufundi na Maendeleo ya Jamii, Elimu ya Watu wazima na Elimu ya juu lengo ni kutoa elimu bora kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum.

Serikali inafanya hivyo kwa sababu inatekeleza Azimio la Kimataifa, Azimio Namba nne (4) katika maazimio ya maendeleo endelevu linalozungumzia elimu. Azimio hilo limetutaka tutoe Elimu kwa wote, watoto wa kike na wa kiume, Elimu isiyolipiwa na yenye hadhi.

Serikali imeandaa miongozo kwa ajili ya kurahisisha utoaji Elimu maalum na jumuishi Nchini: Mwongozo wa Usimamizi wa Uendeshaji wa Taasisi zinazotoa Elimu maalum na jumuishi kwa watoto wenye mahitaji maalum wa mwaka2021, Mwongozo wa majengo ya Serikali yanayozingatia wanafunzi wenye mahitaji maalum wa mwaka 2020 na mwongozo wa lishe shuleni wa mwaka 2021.

Serikali imeshatumia zaidi ya shilingi Bil.5.9 kununua vifaa kwaajili ya wanafunzi wenye mahitaji maalum katika Elimu Msingi, Sekondari na Vyuo.

Mwaka 2021 Serikali imechapa na kusambaza vitabu vya maandishi yaliyokuzwa vya masomo yote kuanzia darasa la kwanza hadi la saba kwaajili ya wanafunzi wenye uoni hafifu au wasioona kabisa.

Serikali pia imetoa shilingi milioni 704 kwa ajili ya uchapaji wa vitabu vya aina hiyo kwa masomo ya Sanaa, Sayansi na Biashara kuanzia kidato cha kwanza hadi kidato cha nne, hatua inayofuata ni kitado cha tano na cha sita.

Serikali imetoa mafunzo ya aina tofauti kwa walimu 3980 wenye taaluma ya elimu maalum katika ngazi za Msingi, Sekondari na Walimu.

Mafunzo yametolewa kwa wadhibiti ubora ili waweze kukagua madarasa maalum na jumuishi pamoja na miundombinu kwa ajili ya wanafunzi wenye mahitaji maalum.

Serikali ilifanya ubainishaji wa watoto wenye mahitaji maalum ambao wamefikisha umri wa kuanza shule, zoezi hilo lilifanyika katika kata 3785 sawa na asilimia 95.7 ya kata zote nchini.

Serikali ilifanya ubainishaji wa watoto wenye mahitaji maalum ambao wamefikisha umri wa kuanza shule, zoezi hilo lilifanyika katika kata 3785 sawa na asilimia 95.7 ya kata zote nchini na kubaini watoto elfu 28968 wenye mahitaji maalum kati ya watoto elfu 59784 waliochunguzwa, tayari watoto hao wote wameandikishwa.

Hatutakubali, mtoto wa Kitanzania akose fursa za elimu kwa sababu ya changamoto za kimaumbile, tutafanya kila tunaloweza kujenga mazingira wezeshi ili watoto wote waweze kwenda shule.

Tumeendelea kujenga uwelewa kwa jamii, kuhusu utambuzi, uandikishaji na uchukuaji wa hatua stahiki kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu wa ngazi zote za elimu kupitia vyombo vya habari, makongamano na majukwaa mbalimbali ya Kitaifa na Kimataifa.

Ndugu wanafunzi, mliwasilisha maombi maalumu kupitia Waziri wa Elimu, Prof. Adolf Mkenda aliyafikisha nami nilimpa jukumu hilo la kuhakikisha yote yanatekelezwa.

Kuhusu suala la chumba cha Saundproof nimeona haja ya kuwa na chumba hicho hapa shuleni nalibeba swala hilo mwenyewe, nitatafuta mtu wa kufanya kazi hiyo.

Mliomba pia kujengewa Hostel, nakuagiza Prof. Mkenda (Waziri wa Elimu) mnapojenga hostel hizo jengeni pia na nyumba mbili za matron na patron ili wawe karibu na wanafunzi hapa.

Kuhusu ombi la Maktaba na Ukumbi, nalielekeza TAMISEMI kupitia Jiji la Dar es Salaam, ombi la gari kwaajili ya kusaidia wanafunzi wenye mahitaji maalum wanaopata changamoto wanapokuwa shuleni, tayari limeanza kufanyiwa kazi, gari hilo likipatikana lihudumie pia na Shule jirani ya Uhuru Mchanganyiko watakapokuwa na uhitaji mpaka hapo watakapopata gari lao.

Kulikuwa na maombi ya vifaa vya michezo, nawashukuru sana Bank ya NMB ambayo imetusaidia, na pia leo nimepokea ahadi kutoka kwenye Foundation ya Mhe. Wanu Hafidh Ameir ambaye ameahidi ataleta jezi 76 pamoja na mipira yake kwa ajili ya shule zote tatu.

Changamoto ni nyingi, zilizobaki tutakwenda kuzifanyia kazi na tutarejesha majibu. Namshukuru Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB kwa kutuletea Komputa lakini ni chache, namuomba mnapotenga tena fedha kwaajili ya msaada mtuongezee kwa idadi kama hii.

Shule ya Sekondari ya Uhuru Mchanganyiko wanazo pia changamoto mbalimbali ikiwemo upungufu wa vyumba vya madarasa, nawataka Mawaziri wa TAMUSEMI na Elimu kaangalieni uhitaji uliopo kwa shule hizi na zote nchini, tupate gharama zake ili tunaweza kupunguza kwa kiasi kikubwa.

Shule ya Sekondari Uhuru pia walileta changamoto ya umeme kukatika katika, nami nalichukua. Hizi ni changamoto kwa shule zote zenye mahitaji maalum kote nchini, nawahakikishia, Serikali imejipanga kuzishughulikia kadri bajeti itakavyoruhusu.

Natambua pia baadhi ya changamoto zenu zinahitaji utatuzi wa haraka, Mawaziri husika wakitoka hapa watakwenda kuzishughulikia.

Nawapa moyo wanangu wenye mahitaji maalum, pamoja na changamoto za kimaumbile mlizonazo tambueni kwamba mnao uwezo wa kufanya mambo makubwa kwa ajili yenu.

Kila mmoja Mungu amempa kitu ambacho anaweza kufanya, nawaomba msome kwa bidii, mpate elimu baadae kila mmoja achague anachoweza kufanya, Serikali yenu ipo, itawaunga mkono kwa yale ambayo mtakuja kufanya. Nawaombea kila la kheri katika masomo yenu pamoja na walimu wenu, Mungu awaongoze.


Imeandaliwa na Idara ya Habari-MAELEZO

IMG-20220307-WA0059.jpg


IMG-20220307-WA0064.jpg


IMG-20220307-WA0063.jpg
 
Pamoja na hizo garama za kununua, kuprint, kubandika nk hazitolewi na serikali but hizi serikali zetu za kiafrika kuna haja ya kubadirika kwa matumizi aina hii.

Yaani kwenda kuonana na kuongea inatumika for instant 200mil nje ya miradi inayokusudiwa au vitu vilivyotolewa.

Yap siyo pesa ya wananchi but moja kwa moja inatokana na wananchi. This is Afrika.
 
kwa shule ya Benjamini viongozi wengi wanajitahidi kwa sehem kuitembelea, lakini sijui Pugu sekondari kuna mzimu gani.. hata viongozi waliosoma pale hawana mzuka nayo kabisa.
Kama serikali haina mpango na hiyo shule si bora irudishe kwa waseminari wenyewe kama ilivyokuwa kwa Forodhani?
 
Back
Top Bottom