Vurugu South Africa tukubali sie weusi ni tatizo

ibanezafrica

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,261
6,543
Kisingizio Zhuma Kufungwa imepelekea maelfu ya watu kuvamia maduka na kupora mali,kusababisha uharibifu mkubwa wa mali za watu! Hii ni aibu kubwa sana cjui duniani wanatuchukuluaje sie waafrika.

Afrika kusini ina mchanganyiko wa matabaka tofauti ya watu waafrika,wazungu,wahindi nk lakini cha ajabu hizi video zinazosambaa duniani tunaona kabisa wengi wao kama si wote wanaofanya uporaji ni weusi, hiki kitu kinatujengea taswira mbaya waafrika wote weusi mbele ya uso wa dunia..na ndio kisa maswala ya ubaguzi wa rangi kwa weusi kudhalilishwa huko ulaya hayaishi kwa tabia mfano wa hizi.

Tumeona majuzi wachezaji wa England wenye asili ya afrika wakinyanyapaliwa kwa ule tu weusi wao na asili. Sisi weusi tuna tatizo kubwa aisee wacha tu wazungu watuone wa ajabu.

Mfano mwingine wa tabia za ajabu na kinyama ni kule Nigeria ambapo kila kukicha vikundi vya watu wanateka wanafunzi na kuwapeleka porini na serikali ipo!

Eeh Mungu hebu tusaidie waafrika.sijui nini kifanyike au wangeliona hili wangetafuta tiba.
 
Kweli ng'ombe wa masikini hazai,,

Ningekuwepo hapo south ndy kipindi kizuri cha kupiga pesa sna hicho.

Daa!!!

Natamani nipae nifike,.huko kwenye vurugu..
 
Kisingizio Zhuma Kufungwa imepelekea maelfu ya watu kuvamia maduka na kupora mali,kusababisha uharibifu mkubwa wa mali za watu! Hii ni aibu kubwa sana cjui duniani wanatuchukuluaje sie waafrika...
Wazungu wanatuita "a stain in humanity"ni doa katika ulimwengu,hata USA,blacks wakiandamana lazima wapore.

Wale washabiki wa Trump waliovamia jengo la Ikulu,walipiga Askali tu na kuharibu mali,hawakwenda kupola mali za watu.

Viongozi wa Kiafrika wameshindwa kusaidia wenzao,wamepatikana matajiri wachache kama Ramaphosa, Motsepe, lakini wazawa wengi Bado choka mbaya.
 
Mleta mada ww ndo tatizo na mbaguzi.ww Cha kwanza uliweka concentration kwa wa Africa na sio wote waliofanya vurugu!!!mbaguzi wa rangi mkubwa wewe!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom