Vurugu kubwa zatokea Kariakoo, Dar

Vurugu kubwa zatokea Kariakoo, Dar

Milindi

JF-Expert Member
Joined
Mar 3, 2009
Posts
1,478
Reaction score
757
Muda huu gari tatu,Polisi magari mawili na msd gari moja yamepita hapa kwa mwendo kasi ajabu wakiwa wamevalia full na siraha kamili.Aliyeko mtaani atujuze zaidi.

Updates
:

attachment.php

attachment.php

attachment.php

attachment.php

Taswira ndani ya viunga vya Kariakoo.

Inasemekana askari wa jiji walikuwa wanakamata biashara za wamachinga mtaa wa kongo, na wafanyabiashara hawakukubali ndipo fujo zikaanza na wafanyabiashara wakafunga barabra na kuchoma matairi, ndio Field Force wakaja kutawanya watu na mabomu ya machozi kupigwa kwa wingi na risasi za moto kupigwa hewani.

Ni hivi: ilikuwa ni operation ya kuondoa biashara holela hapa kariako hasa mitaa ya kongo na msimbazi, wamachinga wakadindisha, wakagoma kabisa! ndio vurugu za mabomu zilipoanza na watu kukimbizana kama mbwa pori.

MATOKEO: -watu wawili nasikia wamekufa kwa kugongwa na magari wakati wa mkimbizano.
- Majeruhi watatu ndio wameshushwa na taxi kwenye hospitali hapo mtaa wa lindi.., hali zao ni mbaya

BREAKING NEWS--NI VITA KARIAKOO, RISASI ZA ZARINDIMA NJENJE,MAGARI SOMA HAPA KUJUA

HABARI zilizotufikia Mda huu zinasema Vurugu kubwa imetokea mda huu maeneo ya kariakoo Jijini Dar Es Salaam na kupelekea Jeshi la polisi kurusha Risasi hovyo ili kuwatawanya Wamachinga walioanzisha Fujo hizo huku barabara za kuingia na kutoka kariakoo zikiwa zimefungwa kutokana na Matairi ya Gari yaliyochomwa moto barabarani.

Kwa Mujibu wa Shudhuda wetu aliyoko Maeneo hayo ya Kaliakoo anasema Chanzo cha vurugu hizo zinatokana na Wafanyabiashara Wadogodogo Maarufu Wamachinga kudai mfanya Biashara mwenzao kuuliwa na Mgambo wa jiji.

Shuhuda huyo alizidi kusema Mfanya Biashara huyo aliuliwa na Mgambo kwa kupigwa kipigo kikali na kumpelekea mauti, Wafanyabiashara hao wanadai hali hiyo ni ishara ya kuchoshwa na Manyanyaso hayo wanayofanyiwa na Mgambo hao na kuanzisha hali hiyo ya Fujo ambayo wanadai ni njia ya kupeleka ujumbe kwa Serikali.
 
Attachments

  • IMG-20141223-WA0139.jpg
    IMG-20141223-WA0139.jpg
    34.3 KB · Views: 12,996
  • kimenuka3.jpg
    kimenuka3.jpg
    36.8 KB · Views: 1,886
  • leo1.jpg
    leo1.jpg
    61.1 KB · Views: 11,382
  • leo2.jpg
    leo2.jpg
    67.4 KB · Views: 11,295
  • leo3.jpg
    leo3.jpg
    64.2 KB · Views: 11,301
Watu wamefunga maduka na biashara zingine baada ya kutokea askari wakifanya fujo, mabomu/risasi hakika sijajua anayeharibu amani nchi hii ni nani kati ya wananchi au serikali ya CCM?

Watu ndani ya nchi yao wakifanya shughuli zao za kihalali na mchana kweupe anapigwa mabomu, anatishiwa maisha, wakati huo huo yeye ndie mlipa kodi kwa maana kodi yake inamgeuka kumtishia maisha yake...
 
Piganeni nao ka Arusha na Mwanza
 
Uchaguz c umeshaisha waohawana faida na nyinyi had uchaguz ujao
Ss cjuihayando maisha bora tilio ahdiwa
 
Mtu una post news alert watu wanaleta utani halafu wanajiita great thinker!! Mnazidi kuishusha dhamani forum yetu!! shame on you!!.Thanks waliotujuza ni city na machinga!.Mida hii naona na zima moto linapita kwa kasi!!
 
Haiwezekani askari waanze tu kurusha risasi na kufyatua mabomu bola sababu, please tuelezee chanzo - story ipo biased
 
Watu wamefunga maduka na biashara zingine baada ya kutokea askari wakifanya fujo, mabomu/risasi hakika sijajua anaye haribu amani nchi hii ni nani kati ya wananchi au serikali ya CCM ?
Watu ndani ya nchi yao wakifanya shughuli zao za kihalali na mchana kweupe anapigwa mabomu, anatishiwa maisha, wakati huo huo yeye ndie mlipa kodi kwa maana kodi yake inamgeuka kumtishia maisha yake...
Serikali za mitaa chama gani kimeshinda hapo?
 
Watu wamefunga maduka na biashara zingine baada ya kutokea askari wakifanya fujo, mabomu/risasi hakika sijajua anaye haribu amani nchi hii ni nani kati ya wananchi au serikali ya CCM ?
Watu ndani ya nchi yao wakifanya shughuli zao za kihalali na mchana kweupe anapigwa mabomu, anatishiwa maisha, wakati huo huo yeye ndie mlipa kodi kwa maana kodi yake inamgeuka kumtishia maisha yake...

Wageuzieni na shavu la pili kama mkitaka, vinginevyo tumieni sera ya jino kwa jino. Mkitaka pepo sharti mfe kwanza
 
Tupia Taarifa Tatizo ni nini au wanawatisha wananchi ili wasahau utumbo alioongea huyo
kilaza wao?
 
Watu wamefunga maduka na biashara zingine baada ya kutokea askari wakifanya fujo, mabomu/risasi hakika sijajua anayeharibu amani nchi hii ni nani kati ya wananchi au serikali ya CCM?

Watu ndani ya nchi yao wakifanya shughuli zao za kihalali na mchana kweupe anapigwa mabomu, anatishiwa maisha, wakati huo huo yeye ndie mlipa kodi kwa maana kodi yake inamgeuka kumtishia maisha yake...

Police wanafanya fujo....????
 
Back
Top Bottom