Wakuu naomba niulize na nielimishwe hivi vunja jungu lina umuhimu gani tunapokuwa tunakaribia mfungo wa ramadhani?au maana yake hasa ni nini?
Na kama halina maana kwa nini wanamziki na wanaoandaa makongamano wanaandaa sherehe mahususi na kuiita vunja jungu hivi Bakwata haliwezi kuingia kati na kusitisha matangazo yanalenga kuleta maana potofu tafauti na yatendway kipindi cha vunja jungu.
Wakuu nisaidieni.
Ni makosa, makubwa, na ni dhambi Muislamu kuukaribisha mwezi wa Ramadhaan kwa maasi badala ya vitendo vyema. Tunaona kwamba Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Ametuwekea mwezi mtukufu wa Rajab, kisha mwezi wa Sha'abaan ambayo yote ni faida kwetu kujitayarisha na vitendo vyema kuupokea mwezi wa Ramadhaan.
Lakini ni jambo la kusitikisha sana kuona kwamba ndugu zetu wengine hufanya kinyume chake; wengine kuukaribisha kwa kama inavyojulikana 'vunja jungu', na humo wengine ima huingia katika mambo ya munkaraat kama michanganyiko wa wanawake na wanaume kwenda mandarini (picnics), wengine kufanya maparty ya muziki na wengine hufika hadi kutenda maasi ya kulewa au kuzini....!
Mkumbuke Malakul-Mawt (Kikata Ladha) ambaye atayakatisha maisha ghafla moja, bila ya mtu kutaraji, bila ya wakati maalum na bila ya kuletewa barua. Huyo si mwengine, ila mwenye kumpatia jina jipya mtu kuwa ni Marehemu, anayeligeuza jina la mke kuwa Kizuka na kumfanya kuwa Mjane. Anayempatia jina jipya mtoto kuwa ni Yatima. Anayegeuza mali iliyoachwa kuwa ni mirathi. Hiyo ni amri ya Mola wetu kuzichukua roho za wanaadamu, mmoja baada ya mmoja. Na ujira wa matendo yote yatalipwa kamili Siku ya Qiyaama.
Uislamu haumuamrishi mfuasi wake kujiingiza kwenye shughuli zisizo na manufaa. Haya yote yanatokana na kukosa khofu, hata ibada zetu tunaziingiza mambo ya fedheha na kashfa kubwa. Wakati kama wa Ramadhaan unahitaji matayarisho ya kutenda mema na kuazimia kuingia kwenye khayr nyingi ndani ya mwezi huu. Badala yake Waislam wanajitayarisha kuupokea kwa vunja jungu na kuumizana kichwa kwa kufanya shopping pamoja na kupandisha vyakula bei za juu kabisa.
Ni vyema tukaelewa ya kwamba Uislam unaharamisha yale ambayo yanaleta ufisadi na kuyawacha yale ambayo watu hawana budi nayo, na kuyachukia yale yasiyofaa na kuyapenda yale yenye maslaha zaidi. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Taala):
"
Sema (uwaambie): "
Mola wangu Ameharamisha mambo machafu, yaliyodhihirika na yaliyofichika
"
Q 7:33
Gonga Hapa kwa Habari Zaidi kuhusu: Vunja Jungu