Ng'wamapalala
JF-Expert Member
- Jun 9, 2011
- 6,811
- 6,506
Kwenye swala la Muungano, sera ya CCM inabidi ife kama mtu anayekufa na tai shingoni.
Hata Mwenyekiti wa Taifa wa CCM analifahamu hili na ndiyo maana akawaambia wanachama wajiandae kwa lolote litakalotokea katika mchakato wa Katiba.
Serikali mbili zimeshindwa kuuvusha muungano nje ya kero za muungano na kwa maana hiyo, kinachotakiwa ni serikali tatu ambazo kwa uharisia ni njia kuelekea kuvunjika kwa muungano kwa vile Zanzibar hawawezi kuchangia gharama zake.
Haya matatizo yangemalizwa kama serikali ya CCM ingeruhusu kuwepo kwa kura ya maoni kitaifa kuhusu muungano.
Ninafahamu wabunge wa bunge maalum wanaweza kubadilisha kilichoko kwenye Rasimu hii ya Katiba lakini vile vile wakumbuke kuwa wananchi pia wana sauti yao kupitia kura ya maoni kuhusiana na Rasimu hii ya Katiba.
Njia bado ni ndefu!