Voices from within: Nimesikia sauti, Dr. Tulia Ackson ndiye Spika ajaye! Sauti hiyo imenieleza Ndugai, japo atatamani aendelee lakini...

Mkuu mdukuzi, kwanza asante kwa bandiko hili Pasco Mayalla ana vielement vya unabii afungue kanisa

Naomba tulitumie bandiko hili Voices From Within: Japo 2025 Tumepanga Twende na Mwanamke, 2025 Mama Akabidhi Kwanza Mwanamume, Kisha 2030 Ndipo Aje Mwanamke kama a litmus paper to test kama sauti hizi ni za ma pepo au ni Roho Mtakatifu!.
Angalia baadhi ya kauli umba zangu ziliumba nini na baadhi ya tabiri zangu, nilisema nini na kikatokea nini?. "Ombeni Mtapewa", "Tafuteni Mtapata", "Bisheni Hodi Mtafunguliwa" Je, Wajua Kuna "Kauli" na "Kauli Umba" Ambazo Huumba? Shuhudia
P.
 
Sauti ya ndani haijasema chochote khs spika 2025?..
Sauti hazijasema ila trends zinanieleza Kama CCM imedhamiria kwa mgombea urais wa JMT mwaka 2025 ni lazima awe Mwanamke, then Mwanamke huyo ni Dr. Tulia, hivyo the next speaker automatically atakuwa Zungu, ila kwa my honest opinion, Zungu hafai kabisa kuwa Spika!. Vicky Kamata Anastahili Pongezi! Asimama Kidete Kupinga Uonevu, Ubabe na Double Standards za Zungu! na hapa Zungu akiuka Kanuni za Bunge kuiokoa Serikali!. Pareso ang'ang'ania Shilingi! Almanusura!
P
 
Binafsi nakuelewa sana ila wasiokuelewa ni wale wanaosoma maandiko yako kama wanasoma gazeti,barikiwa mkuu
 
, lakini pia kwa vile Spika ajae kwa mujibu wa maono haya ni Dr. Tulia Akson, hata rais akikiuka katiba, Bunge la Dr. Tulia, tena kwa kuzingatia litakuwa ni Bunge la chama kimoja CCM, litaweza kumwajibisha rais?.

Alhamisi Njema.
Paskali
Bunge letu Tukufu limefanya kosa kubwa sana kuptisha sheria mpya ya uchaguzi yenye ubatili ndani yake!.

Ukiondoa udhaifu huo, Spika did her best
Spika Tulia kaiva sana kwenye suala kutafiri Sheria, naangalia hapa Bunge live wanapitisha muswada wa tume ya uchaguzi naona anamtoa knout mpaka AG huyu dada ni balaa wabunge wote wanampigia makofi.

Mbeya tunasema Tulia mitano tena.
Naunga mkono hoja Hongera Spika Dkt. Tulia Ackson. Kuna haja MaSpika wetu iwe lazima kuwa Wanasheria?

Tena sio Tulia mitano tena bali 2025 could be ni Dr. Tulia!.
Angalia tulikotoka nae
1. Hivyo japo ni mimi niliyemtabiria Dr. Tulia uspika, Voices from within: Nimesikia sauti, Dr. Tulia Ackson ndiye Spika ajaye! Sauti hiyo imenieleza Ndugai, japo atatamani aendelee lakini...

2. Fursa ya Spika mpya ilipojitokeza, niliwaomba CCM Kujiuzulu kwa Ndugai ni mpango wa Mungu kwa Tanzania ili tupate Spika Bora. CCM itateua Spika Bora au Bora Spika kama kawa?

3. Hivyo Dr Tulia aliposhinda nikamshauri Je, Wajua, Naibu Spika, Chini ya "Bora Spika", Anaweza Kuwa "Spika Bora?". Dr. Tulia, "Ukitulia, Una Fursa ya Kuwa Spika Bora Sana!" Hongera Sana!

4. Kwa vile Rais Samia amesisitiza 2025 twende na Mwanamke Watanzania, tuunge mkono 2025 ni zamu ya Mwanamke, ila sio lazima awe yeye bali yule aliyepangiwa na 'YEYE', kama ni yeye aliyepangiwa, then ni yeye! wengi wanadhani Mwanamke wa 2025 ni lazima awe Rais Samia, anaweza kuwa ni Dr. Tulia!.
5. Sababu ya kwanini 2025 anaweza kuwa ni Dr. Tulia ni HII

P
 
Acha kudanganya watu.
Tangu Magufuli amtoe tulia kutoka alikokua na kufanya michongo awe naibu spika, kila mwenyemacho alikua Tulia anaandaliwa kua spika.
 
Acha kudanganya watu.
Tangu Magufuli amtoe tulia kutoka alikokua na kufanya michongo awe naibu spika, kila mwenyemacho alikua Tulia anaandaliwa kua spika.
Naomba usichanganye mambo kati ya Dr. Tulia kuwa Naibu Spika na kuwa Spika, kwenye Unaibu Spika, ni kweli JPM alihusika ila kwenye Uspika, its just a fate, JPM had nothing to do with this kwasababu he was long gone!.

Kaka umesahau kwamba hakuna mtu wa CCM ambaye angejitokeza kugombea na naibu aliye madarakani, kwani umekua utaratibu wa CCM kwamba spika akiondoka naibu anachukua.
 
Hakuna utabiri wowote uliofanya hapo, ilikuwa wazi kuwa kama Ndugai angemaliza muda wake, basi Tulia alishaandaliwa kuwa spika, ni utamataduni wetu CCM.
 
Hakuna utabiri wowote uliofanya hapo, ilikuwa wazi kuwa kama Ndugai angemaliza muda wake, basi Tulia alishaandaliwa kuwa spika, ni utamataduni wetu CCM.
There you are!, jee JYN alimaliza muda wake?. Soma tenda bandiko hili huki ukishirikisha critical thinking. Anza na heading tuu
P
 
Kaka umesahau kwamba hakuna mtu wa CCM ambaye angejitokeza kugombea na naibu aliye madarakani, kwani umekua utaratibu wa CCM kwamba spika akiondoka naibu anachukua.
Kiukweli baadhi yetu humu hamna kumbukumbu, enzi za Spika Sitta, mzee wa Speed and Standards,SS, yeye alichukua fomu na naibu wake Anna Makinda akachukua.

Jee baada ya JYN kuchukua fomu, Tulia alichukua?. Angalia tena heading yangu nimesema nini?.

Hivi kweli huamini huu ni utabiri?.
Vipi huu

Na huu

Na huu

Na huu

P
 
Mzee mwenzangu Sasa unaniangusha. Kipindi kile Six angeshinda Ila Makamba ndie aliyetamka hadharani kwamba safari hii tunataka spika mwanamke, kwa bahati mbaya six hakua mwanamke.
Kumbuka mabifu ya Hawa wazee.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…