Vodafone K-3565-Z IMEWEZESHWA SIMCARD ZOTE | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vodafone K-3565-Z IMEWEZESHWA SIMCARD ZOTE

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by gomer, Jan 12, 2011.

 1. g

  gomer Senior Member

  #1
  Jan 12, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 108
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Rejea mijadala na marumbano inayo husiana na kifaa hiki cha ZTE chenye nembo ya kibiashara ya Vodafone kwamawasiliano ya mfumo wa GSM.

  Zimeainishwa njia kuu mbalimbali, zote zikianisha kuondolewa kwa kikwazo cha kivuli kilichosimikwa ndani ya kifaa kinachoendesha uteja wa mawasiliano yanayolenga kulinda kete za Vodacom Tanzania na washikaji wao.

  Abadan si nia ya ZTE wala Vodafone kuzuia simcard nyinginezisitumike katika kifaa hiki ila program ya Vodafone imepungukiwa na nukuu katika mafaili yake ya utambulisho.
  Kunukuu utambulisho wa simcard isiyowezeshwa itakuwa ni njia mojawapo ya kuiwezesha itumike na program ya Vodafone.

  Kutotumia program kikwazo ya Vodafone itakuwa ni njia nyingine tutakayoijadili katika jalida jingine ikiwa ni kutumia Vodafone K-3565-Z bila program yake na hata viunganishi vikuu vingine inawezekana. Microsoft windows OS imekamilika.

  Natumia utambulisho wa Airtel kama mfano wa kijenga hoja ya hatua zitakazoainishwa.

  I. Tufahamu
  MCC na MNC; Sms centre number ni muhimu

  Za Airtel ni :-
  640 na 05; +255780000004.
  II. Tuchambue folder la Vodafone, Opco semaliko
  C:\Program Files\Vodafone\Vodafone Mobile Connect\Opco ,

  Kopy folder ili tulihifadhi kama rejeo endapo tutakosea,

  Tufungue Opcos na tutafute na kuubadili kiaina mstari huu kwa kutumia editing tools,
  <OpcoEntry CCMNC="23403" Opco="Airtel-Vodafone" Country="Jersey" Phone="+447829791004" />
  Tupate mstari unaosomeka hivi,
  <OpcoEntry CCMNC="64005" Opco="Airtel " Country="Tanzania" Phone="+255780000004" />
  tusave katika format ileile.
  III. Tutafute folder 23403 Jersey ndani ya folder Opco

  Tulipe jina mbadala 64005 Tanzania
  Tuingie ndani ya folder na kubadili kila namba 23403 iwe 64005 na Jersey iwe Tanzania.

  Kuna mafaili mawili muhimu aina ya .html na .xml ,

  tukifungua la .xml tubadili mstali kama tulivyofanya hatua ya II,

  <OpcoData CCMNC="23403" Opco="Airtel-Vodafone" Country="Jersey" Phone="+447829791004" />

  Tupate mstari unaosomeka hivi,

  <OpcoData CCMNC="64005" Opco="Airtel " Country="Tanzania " Phone="+255780000004" />
  .............................
  .................................
  Haya ni mababiliko muhimu ya kuiwezesha simcard ya airtel itambulike na program ya vodafone -9.4.2.14250

  Mabadiko mengine yanaweza kufanyika kuboresha matokeo na matumizi ya programu.
  Kwa wale wenye ugumu wa kucheza na madudu haya itakuwa bora kupata folder zima lililomo ndani ya opco, kupitia mlango wa uwani, kutoka kwa mtu aliye karibu na airtel. Hii itamaanisha kuongeza mstari wake kwenye opcos file.

  Programu ya Vodafone inaonyesha kuwepo kwa mawimbi ya zantel gprs; Tigo gprs na 3g; Vodacom gprs na 3g; airtel gprs na 3g, katika eneo la mbezi beach Dar es Salaam, mawimbi ya airtel yako juu na stable.
   
 2. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #2
  Jan 12, 2011
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  hongera mkuu ninayo hapa nitafata maelekezo yako na nitatoa majibu nipo njiani
   
Loading...