Debranding Vodafone K3570-Z USB Modem | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Debranding Vodafone K3570-Z USB Modem

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Ozzie, May 26, 2011.

 1. Ozzie

  Ozzie JF-Expert Member

  #1
  May 26, 2011
  Joined: Oct 9, 2007
  Messages: 3,234
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 135
  Nilinunua Modem ya Vodacom aina ya ZTE, Vodafone K3570-Z. Nilihangaika sana kuifanya iweze kutumika kwa kila mtandao. Bahati nzuri nikatembelea mtandao fulani ambapo mtu kwa jina la Shahnawaz alikuwa amepost namna ya kuifanya modem hii kutumika katika mitandao tofauti. Mimi ni mtaalamu wa afya, bahati nzuri nimekuwa napenda mambo ya IT, hivyo nimejaribu kuchukua hatua alizozitoa huyu jamaa. Hapa ninapoandika ninatumia Airtel kwenye Modem.
  Hatua:
  1. Kwanza unatakiwa uwe na mafaili mawili ya ZTE Drivers na pia ya ZTE Connection manager. Kama huzioni link za hayo ma file basi yanapatikana kwenye address hizi mbili, ya kwanza Hotfile.com: One click file hosting: Win-ZTEDrv_V1.0.1.16.zip na pili hapa Hotfile.com: One click file hosting: Connection_Manager_generic_EN_DE.zip
  2. Ikiwa ulishawahi tumia modem hii kwa namna ya kawaida bila shaka ulishafanya installation ya Vodafone ZTE connection manager hivyo hatua itakayofuata itakuwa ku uninstall hiyo Dashboard ya Vodafone (Vodafone ZTE Connection Manager) ili baadaye nafasi yake ichukuliwe na ZTE Connection manager ambayo haiko branded na Vodafone ambayo utakuwa umeshaipakua katika hatua namba 1 tayari kwa kufanya installation katika hatua namba 3. Ukishafanya uninstallation itatakiwa uzime na kuwasha 'SIPIYU' yako.
  3. Hatua ya tatu (ambayo inaweza ikawa hatua ya pili kama hukuwahi fanya installation ya Vodafone ZTE Connection Manager) ni kufanya installation ya ZTE drivers ulizopakua hapo juu. Ukishamaliza tena install ZTE connection manager (ZTE Join Air). Hili file la pili kama lile la kwanza liko zipped, kwa hiyo uki unzip litatokea folder lililoandikwa Connection_Manager_generic_DE_EN ambapo ukilifungua utaona kuna file limeandikwa "install" ambalo itabidi u-run hilo file.
  4. Muda wote huo inatakiwa modem yako iwe haijachomekwa kwenye computer, baada ya kumaliza installation unaweza kufungua connection manager (au inaweza kufunguka automatically) na subiria kwa angalau dakika 1, kuruhusu software hizi ku unlock modem yako. Hapo itakuwa kama umeshamaliza kazi, na unaweza ukafanya configuration ya connection manager wakati SIM card imepachikwa. Kwa SIM cards za Voda na Airtel huhitaji kubadirisha settings zozote (au Dial *99# kwa hizi network za GSM). Modem yako ikishakuwa detected wewe unganisha tu. Ila kama wewe watumia cdma kama Zantel Dial *777#
  [​IMG]
   
 2. Loyal_Merchant

  Loyal_Merchant JF-Expert Member

  #2
  May 26, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 589
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  sasa hapo mfano ukitoa hiyo modem na kwenda kuinstal katika sipiyu nyngne utahitajika kurudia proces zote hzo au ndo inakuwa multiline jumla?
   
 3. Ozzie

  Ozzie JF-Expert Member

  #3
  May 26, 2011
  Joined: Oct 9, 2007
  Messages: 3,234
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 135
  Sijajaribu. Ila nahisi itabidi urudie hatua hizohizo. Maana nilijaribu ku-uninstall programme zote (zihusianazo na hii modem) kwenye laptop yangu ili nione kama naweza kutumia ile original Vodafone ZTE connection manager. Japo Vodafone ZTE Connection Manager ilikubali ku install lakini ikakataa ku connect kwenye internet. Mpaka nilipozirudisha tena program tajwa hapo juu ndipo nikaweza kupata mtandao kupitia Airtel na Vodacom.
   
 4. S

  Soki JF-Expert Member

  #4
  Jun 4, 2011
  Joined: Jan 5, 2011
  Messages: 1,308
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Mkuu umesema modem unaichomeka katika PC katika hatua gani?
   
Loading...