Vodacom yakabidhi bil. 8/- kwa JK

BONGOLALA

JF-Expert Member
Sep 14, 2009
16,500
2,000
RAIS Jakaya Kikwete, jana amepokea hundi ya sh. bilioni nane kutoka Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania na kuikabidhi katika Hospitali ya CCBRT, ili kufanikisha ujenzi wa Hospitali mpya ya huduma za uzazi na watoto.

Akipokea hundi hiyo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom, Bw. Rene Meza, Rais Kikwete alisema hayo ni
matokeo ya kampeni ya kutokomeza ugonjwa wa Fistula kwa wanawake ambayo ilizinduliwa Februari 18 mwaka huu.

Alisema kutokana na Serikali kujali afya za wanawake na watoto, iliamua kushirikiana na kampuni ya Vodacom Tanzania kuhakikisha ugonjwa huo kwa wanawake unatokomezwa nchini.

Kwa upande wake, Bw. Meza alisema mchango waliotoa ni sehemu ya ahadi zilizotolewa na kampuni hiyo nchini kupitia taasisi yake ya Vodacom Foundation.

"Kati ya fedha hizo, milioni 900 zimetokana na michango ya wafanyakazi wa kampuni hii, washirika pamoja na wadau mbalimbali ambao waliguswa na tatizo hilo.

"Pesa hizi ni nusu ya ahadi yetu kwani awali tuliahidi kuchangia sh. bilioni 15 kwenye ujenzi wa hospitali hiyo ambayo inatarajiwa kukamilika mwaka 2014," alisema Bw. Meza.

Alisema kampuni hiyo kupitia taasisi yake ya Vodacom Foundation, CCBRT pamoja na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, waliungana pamoja ili kupambana na magonjwa mbalimbali ya uzazi kwa wanawake ukiwemo Fistula ambao umekuwa tishio.

Naye Ofisa Mtendaji Mkuu wa hospitali hiyo, Bw. Erwin Telemans, aliishukuru kampuni hiyo kwa kutoa fedha hizo na kuahidi kuwa, CCBRT itaendelea kutoa ushirikiano ili kuutokomeza ugonjwa huo.

Alisema ujenzi wa hospitali hiyo ukikamilika, itapewa jina la 'Baobab' na itakuwa ya fufaa kwa wanawake wajawazito ambao
wana matatizo mbalimbali.

Aliongeza kuwa, wanawake milioni mbili duniani wana tatizo la ugonjwa wa Fistula wakati Tanzania ikiwa na wanawake 31,000 wenye tatizo hilo.

Bw. Telemans alisema huduma ya M-Pesa inayotolewa na kampuni hiyo imewezesha wanawake 1,000 wenye matatizo ya Fistula kupata fedha za usafiri na matibabu kutoka mikoani ili waweze kutibiwa katika hospitali hiyo.

Alisema mpango wa kusafirisha wagonjwa kwa kuwatumia fedha kupitia huduma ya M-Pesa, umeiwezesha hospitali hiyo kupambana na ugonjwahuo kwa kuwafikia wanawake wengi hasa waishio vijijini.

"Tunao mabalozi wetu katika mikoa mbalimbali nchini, wanapopata taarifa kuhusu mwanamke mwenye Fistula wanatupa taarifa na pesa inatumwa kupitia M-Pesa na wagonjwa wanapofika Dar es salaam hupokelewa na kuletwa katika hospitali hii," alisema.
 
mpenyo

Member
Jan 6, 2011
19
20
Hata kama ni za mafisadi si zinakuja kuwasaidia watanzania hospitali,au wewe unataka wakaziweke Uswisi?
 
Rack Fikiri

Member
Oct 13, 2012
23
0
Kwa voda ni jambo la maana kwani wameamua kuwasaidia Watanzania ni siyo kwa nia ya kumwingiza Dr Slaa ktk ufisadi 2najua ni shujaa,jasiri, na mwenye maamzi ya busara 2naamini ataendelea na msimamo wake Jasiri haachi asili
 
Lambardi

JF-Expert Member
Feb 7, 2008
10,589
2,000
Nawapongeza sana Vodacom kwa moyo huo wa kusaidia wakinamama ni ugonjwa mbaya mbaya sana maana haja ndogo inatoka bila control,ni hatari sana na inadhalilisha utu wa mwanamke!Jengo litakuwa lina theathre 8 kwa ajili hiyi pia nasikia Vodacom watatoa pesa kwa miaka 3 za matibabu na nauli kwa wagonjwa wote watakaofika pale toka mikoani gharama zao zoote zitalipiwa na Vodacom/Vodafone.....makampuni mengine waanzishe Sober House/Hospital Jamani maana mateja ni janga la Vijana!!na wengi wao wako tayari kuacha wakipewa matibabu
 
Nyalotsi

JF-Expert Member
Jul 20, 2011
6,411
2,000
Hata kama ni za mafisadi si zinakuja kuwasaidia watanzania hospitali,au wewe unataka wakaziweke Uswisi?
hela zetu ni afadhali wanaturudishia kwa mlango mwingine kuliko wangenunulia mavx malaya zao mitaani. Aafu mbona arv za kina b and b foundation mnakula? Kwani biashara zote wanazofanya ni halali? Kwani hapo atakayenufaika ni slaa au wagonjwa ambao ni pamoja na dada zako watakaopata fistula. GT wamepungua sana, ungekuwa gt usingemhusisha slaa na hizohela
 
Money Stunna

JF-Expert Member
Aug 9, 2011
13,083
2,000
ninachotaka kuona mwanachi wa kawaida asa akina mama wanasaidiwa sitak kujua aliotoa ni fisadi au la,sababu sina ushaidi wa kumshtak mtu,acha akina mama wasaidiwe
 
Timtim

JF-Expert Member
Feb 9, 2008
609
250
Tusiweke siasa hapa. Hizo pesa wametoa kama msaada na si kumnunua Dr. Slaa au venginevyo.
 
nummy

JF-Expert Member
Aug 20, 2011
587
0
Sio haba, Kigogo mmoja naye amesema elimu ya secondari bureeeeeeeeeeee! sijui ana taka masifa au ni habari ya kweli
 
BONGOLALA

JF-Expert Member
Sep 14, 2009
16,500
2,000
na jee vodacom wasipokuwepo ktk list ya TOP 20 large tax payers tutalalamika?
 
R.B

JF-Expert Member
May 10, 2012
6,303
2,000
RAIS Jakaya Kikwete, jana amepokea hundi ya sh. bilioni nane kutoka Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania na kuikabidhi katika Hospitali ya CCBRT, ili kufanikisha ujenzi wa Hospitali mpya ya huduma za uzazi na watoto.

Akipokea hundi hiyo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom, Bw. Rene Meza, Rais Kikwete alisema hayo ni
matokeo ya kampeni ya kutokomeza ugonjwa wa Fistula kwa wanawake ambayo ilizinduliwa Februari 18 mwaka huu.

Alisema kutokana na Serikali kujali afya za wanawake na watoto, iliamua kushirikiana na kampuni ya Vodacom Tanzania kuhakikisha ugonjwa huo kwa wanawake unatokomezwa nchini.

Kwa upande wake, Bw. Meza alisema mchango waliotoa ni sehemu ya ahadi zilizotolewa na kampuni hiyo nchini kupitia taasisi yake ya Vodacom Foundation.

"Kati ya fedha hizo, milioni 900 zimetokana na michango ya wafanyakazi wa kampuni hii, washirika pamoja na wadau mbalimbali ambao waliguswa na tatizo hilo.

"Pesa hizi ni nusu ya ahadi yetu kwani awali tuliahidi kuchangia sh. bilioni 15 kwenye ujenzi wa hospitali hiyo ambayo inatarajiwa kukamilika mwaka 2014," alisema Bw. Meza.

Alisema kampuni hiyo kupitia taasisi yake ya Vodacom Foundation, CCBRT pamoja na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, waliungana pamoja ili kupambana na magonjwa mbalimbali ya uzazi kwa wanawake ukiwemo Fistula ambao umekuwa tishio.

Naye Ofisa Mtendaji Mkuu wa hospitali hiyo, Bw. Erwin Telemans, aliishukuru kampuni hiyo kwa kutoa fedha hizo na kuahidi kuwa, CCBRT itaendelea kutoa ushirikiano ili kuutokomeza ugonjwa huo.

Alisema ujenzi wa hospitali hiyo ukikamilika, itapewa jina la 'Baobab' na itakuwa ya fufaa kwa wanawake wajawazito ambao
wana matatizo mbalimbali.

Aliongeza kuwa, wanawake milioni mbili duniani wana tatizo la ugonjwa wa Fistula wakati Tanzania ikiwa na wanawake 31,000 wenye tatizo hilo.

Bw. Telemans alisema huduma ya M-Pesa inayotolewa na kampuni hiyo imewezesha wanawake 1,000 wenye matatizo ya Fistula kupata fedha za usafiri na matibabu kutoka mikoani ili waweze kutibiwa katika hospitali hiyo.

Alisema mpango wa kusafirisha wagonjwa kwa kuwatumia fedha kupitia huduma ya M-Pesa, umeiwezesha hospitali hiyo kupambana na ugonjwahuo kwa kuwafikia wanawake wengi hasa waishio vijijini.

"Tunao mabalozi wetu katika mikoa mbalimbali nchini, wanapopata taarifa kuhusu mwanamke mwenye Fistula wanatupa taarifa na pesa inatumwa kupitia M-Pesa na wagonjwa wanapofika Dar es salaam hupokelewa na kuletwa katika hospitali hii," alisema.
 
Tikerra

JF-Expert Member
Sep 3, 2008
1,704
0
Wajinga ndio waliwao.Kwani CCBRT ni ya nani na Vodakom ni ya nani.Kilichofanyika hapo ni kutoa mfuko wa kushoto wa suruali na kuingiza kwenye mfuko wa kulia.Hatudanganyiki.Zote hizo ni institutions za Freemasons.Hawajasaidia lolote.Ni changa la macho!
RAIS Jakaya Kikwete, jana amepokea hundi ya sh. bilioni nane kutoka Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania na kuikabidhi katika Hospitali ya CCBRT, ili kufanikisha ujenzi wa Hospitali mpya ya huduma za uzazi na watoto.

Akipokea hundi hiyo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom, Bw. Rene Meza, Rais Kikwete alisema hayo ni
matokeo ya kampeni ya kutokomeza ugonjwa wa Fistula kwa wanawake ambayo ilizinduliwa Februari 18 mwaka huu.

Alisema kutokana na Serikali kujali afya za wanawake na watoto, iliamua kushirikiana na kampuni ya Vodacom Tanzania kuhakikisha ugonjwa huo kwa wanawake unatokomezwa nchini.

Kwa upande wake, Bw. Meza alisema mchango waliotoa ni sehemu ya ahadi zilizotolewa na kampuni hiyo nchini kupitia taasisi yake ya Vodacom Foundation.

“Kati ya fedha hizo, milioni 900 zimetokana na michango ya wafanyakazi wa kampuni hii, washirika pamoja na wadau mbalimbali ambao waliguswa na tatizo hilo.

“Pesa hizi ni nusu ya ahadi yetu kwani awali tuliahidi kuchangia sh. bilioni 15 kwenye ujenzi wa hospitali hiyo ambayo inatarajiwa kukamilika mwaka 2014,” alisema Bw. Meza.

Alisema kampuni hiyo kupitia taasisi yake ya Vodacom Foundation, CCBRT pamoja na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, waliungana pamoja ili kupambana na magonjwa mbalimbali ya uzazi kwa wanawake ukiwemo Fistula ambao umekuwa tishio.

Naye Ofisa Mtendaji Mkuu wa hospitali hiyo, Bw. Erwin Telemans, aliishukuru kampuni hiyo kwa kutoa fedha hizo na kuahidi kuwa, CCBRT itaendelea kutoa ushirikiano ili kuutokomeza ugonjwa huo.

Alisema ujenzi wa hospitali hiyo ukikamilika, itapewa jina la 'Baobab' na itakuwa ya fufaa kwa wanawake wajawazito ambao
wana matatizo mbalimbali.

Aliongeza kuwa, wanawake milioni mbili duniani wana tatizo la ugonjwa wa Fistula wakati Tanzania ikiwa na wanawake 31,000 wenye tatizo hilo.

Bw. Telemans alisema huduma ya M-Pesa inayotolewa na kampuni hiyo imewezesha wanawake 1,000 wenye matatizo ya Fistula kupata fedha za usafiri na matibabu kutoka mikoani ili waweze kutibiwa katika hospitali hiyo.

Alisema mpango wa kusafirisha wagonjwa kwa kuwatumia fedha kupitia huduma ya M-Pesa, umeiwezesha hospitali hiyo kupambana na ugonjwahuo kwa kuwafikia wanawake wengi hasa waishio vijijini.

“Tunao mabalozi wetu katika mikoa mbalimbali nchini, wanapopata taarifa kuhusu mwanamke mwenye Fistula wanatupa taarifa na pesa inatumwa kupitia M-Pesa na wagonjwa wanapofika Dar es salaam hupokelewa na kuletwa katika hospitali hii,” alisema.
 
Top Bottom