Vodacom washusha bei kuongea sasa sh 1 kwa sekunde

Voda wanatuyeyusha shilingi moja kwa masaa ishirini kama hiyo sio promasheni ni nini? Tigo anakuambia shilingi moja kwa masaa ishirini na nne, Hiyo ya voda mimi naiita ni promotion.
 
kweli bongo kila kitu kipo tofauti, ulaya peak time ni 6 - 18hrs lakini bongo peak ni 17-21 du
 
Voda wezi hawajapunguza chochote wanajikosha tuu kwani Tigo tokea miaka ya nyuma wao wana huduma hiyo sasa wanavyojinadi ili iweje???
 
Vodacom Tanzania katika kushawishi matumizi zaidi ya simu za mkononi imeshusha bei ya upigaji simu ambapo sasa wateja wa Voda kwa Voda watapiga simu shilingi moja kwa sekunde.
Kwa hesabu za haraka haraka punguzo hilo ni zaidi ya asilimia 200 na wenyewe wanasema litatengeneza hasara lakini watafurahi kama watanzania wengi wataingia katika mtandao.

Huwezi kuwa na punguzo la zaidi ya asilimia 100. Ina maana pamona na kupiga simu bure unapewa pesa:)
 
kweli bongo kila kitu kipo tofauti, ulaya peak time ni 6 - 18hrs lakini bongo peak ni 17-21 du
kibongo bongo tunaenda kinyume nyume hata umeme ni hivyo hivyo peak time yao eti watu wanawasha taa na majiko ya kupikia..
 
Huwezi kuwa na punguzo la zaidi ya asilimia 100. Ina maana pamona na kupiga simu bure unapewa pesa:)
you are right mkuu, ina maana kama walikuwa wanatoza sh 6 (100%) kwa sekunde then kwenda shilingi 1 means wamepunguza sh 5 ambayo ni 5/6 ya 100% which is equal to approx 83% kwa hiyo waseme wamepunguza kwa asilimia 83 na siyo 200
 
Unatumia voda wewe? Au ushabiki tu ndugu yangu?
Si ndio hapo mtu wangu.. halafu utasikia ooh mtandao unaoongoza tanzania....lol. Tigo walipoanza jirushe nao wakatafakariiiii baada ya miezi kadhaa ndipo wakaona wanafulia wakaanzisha cheka time na kama kawaida wakatangaza ni kwa siku nzima ila kwenye utekelezaji waka-exclude 5-9 pm. Sasa wameiga mambo ya sh 1 kwa sekunde alafu tena wana-exclude 5-9pm . Swali la kipimabaridi ni hili: Je wanaongoza Tanzania au wanafuata nyayo za tiGO Tanzania?
 
Back
Top Bottom