VODACOM wanatuibia Kwenye "Bureau De Change Bubu".....!!!!!!!!

Shark

JF-Expert Member
Jan 25, 2010
27,110
2,000
Wadau,

Mimi ni mteja wa Vodacom na kutokana na Biashara zangu z Hapa na pale hua nafanya pia Biashara na Kenya na mara nyingi natumiaga M-pesa kutuma hela Kenya kisha natumiwa Bidhaa. Nimefanya miamala mingi tu na Kenya ila leo nimewaza hii biashara nayoifanya nikagundua kama sio wizi wa Vodacom ningekua Mbali zaidi.

Vodacom wanachaji kiasi cha TZS 23.76 kwa kila 1KES unapokua unatuma pesa Kenya. Kiwango hiki ni kikubwa mno kulinganisha na bei ya kwenye Maduka ya fedha (Bureau de Changes). Mfano nikitaka kutuma KES 100,000 basi kwa kutumia Mpesa nitahitajika kutumia Tshs 2,376,000/= wakati kwenye maduka ya fedha ambako nanunua KES 1 kwa Tshs 21.5 ningelipa Tshs 2,150,000/= (hasara 226,000/=). Hii ni zaidi ya Faida nayoipata kwa mzigo naoulipia hizi hela.

Na serikali hapa pia inapoteza hela nyingi sana, maana ki ukweli hii ni biashara ya Bureau De Change "bubu" wanafanya hawa Vodacom. Ukiacha fact kwamba wanatuibia kwa kutukata rate kubwa, pia wanaiibia serikali kwa kufanya biashara ya Bureau de Change Bila Kibali.

Naomba mamlaka zinazohusika na mambo haya ziangalie hili swala, tulipishwe kwa rate ya Soko, pia Hawa Voda ikiwezekana wasajiliwe kama Bureau de Change nao walipe kodi pia kwenye sekta hiyo
 
Perfectz

JF-Expert Member
May 17, 2017
7,215
2,000
NDIO MAANA HUWA NA PREFER KUWEKA VISENTI VYANGU BENK,MITANDAO INA MAKATO MAKUBWA MNOOO
 
Qurie

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
3,341
2,000
Kwanini usitumie huduma za kibenki kutuma pesa huko.... Si kuna kcb bank au hujui
 
yangu macho

Member
Jun 7, 2017
28
45
Vodacom bana ebu badilikeni hata bando za internet ni shida huwezi fananisha na airtel wala tigo ebu kuweni uwiano na mitandao mingine voda kweli mko juu lakini kuweni makini zaidi
 
Shark

JF-Expert Member
Jan 25, 2010
27,110
2,000
Kwanini usitumie huduma za kibenki kutuma pesa huko.... Si kuna kcb bank au hujui
Kaka,
wajua ilivyo rahisi kwa simu kuliko kwa Benki,
Ila ahsante kwa ushauri, nitaangalia huduma za kibenki kwa transactions zangu kama itapunguza cots
 
Mr Mose

JF-Expert Member
Jun 11, 2016
348
500
Wadau,

Mimi ni mteja wa Vodacom na kutokana na Biashara zangu z Hapa na pale hua nafanya pia Biashara na Kenya na mara nyingi natumiaga M-pesa kutuma hela Kenya kisha natumiwa Bidhaa. Nimefanya miamala mingi tu na Kenya ila leo nimewaza hii biashara nayoifanya nikagundua kama sio wizi wa Vodacom ningekua Mbali zaidi.

Vodacom wanachaji kiasi cha TZS 23.76 kwa kila 1KES unapokua unatuma pesa Kenya. Kiwango hiki ni kikubwa mno kulinganisha na bei ya kwenye Maduka ya fedha (Bureau de Changes). Mfano nikitaka kutuma KES 100,000 basi kwa kutumia Mpesa nitahitajika kutumia Tshs 2,376,000/= wakati kwenye maduka ya fedha ambako nanunua KES 1 kwa Tshs 21.5 ningelipa Tshs 2,150,000/= (hasara 226,000/=). Hii ni zaidi ya Faida nayoipata kwa mzigo naoulipia hizi hela.

Na serikali hapa pia inapoteza hela nyingi sana, maana ki ukweli hii ni biashara ya Bureau De Change "bubu" wanafanya hawa Vodacom. Ukiacha fact kwamba wanatuibia kwa kutukata rate kubwa, pia wanaiibia serikali kwa kufanya biashara ya Bureau de Change Bila Kibali.

Naomba mamlaka zinazohusika na mambo haya ziangalie hili swala, tulipishwe kwa rate ya Soko, pia Hawa Voda ikiwezekana wasajiliwe kama Bureau de Change nao walipe kodi pia kwenye sekta hiyo
Mkuu huibiwi hata exchange ya dola iko juu kwenye online exchange kuliko kwenye maduka ya kubadilishia fedha
 
Ngorunde

Platinum Member
Nov 17, 2006
2,302
2,000
Kaka,
wajua ilivyo rahisi kwa simu kuliko kwa Benki,
Ila ahsante kwa ushauri, nitaangalia huduma za kibenki kwa transactions zangu kama itapunguza cots
Kutumia bank ndio suluhisho. Utapata usumbufu kidogo wa harakati za kibank lakini ni nafuu. Ila ujue kila jambo ni gharama, uharaka unaoupata kwa kutumia mtandao ni lazima ulipe zaidi.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom