Vodacom wameniibia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vodacom wameniibia

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Ndetirima, Oct 5, 2011.

 1. Ndetirima

  Ndetirima JF-Expert Member

  #1
  Oct 5, 2011
  Joined: Oct 4, 2011
  Messages: 898
  Likes Received: 172
  Trophy Points: 60
  Jana mchana nineingiza salio kwenye simu yangu line ya Vodacom TZS 1,000/= baada ya saa moja nikatumiwa ujumbe wa simu kuwa nimeingizwa kwenye bahati nasibu ya TZS 11,000,000/= na wakakata TZS 550/= toka kwenye salio langu ili hali sijatuma ujumbe wowote wa kuhitaji kucheza bahati nasibu yao hiyo. Jamani huo si wizi? Iliniuma sana.
   
 2. m

  mayai New Member

  #2
  Oct 5, 2011
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  You have to sue them, that's apparently daytime robbery.
   
 3. mysteryman

  mysteryman JF-Expert Member

  #3
  Oct 5, 2011
  Joined: Aug 4, 2011
  Messages: 986
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Jamani kila siku tupige kelele tu ebu hamieni huku kwetu mbona mambo mazuri tu...hamia airtel wewe ndugu jamaa na marafiki...
   
 4. HARRY POTTER

  HARRY POTTER Member

  #4
  Oct 5, 2011
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hata mimi walishanifanyia hivyo na walishaniibia takribani 30,000/=.nilipowapigia mara ya kwanza wakaniambia andikaneno ''ondoa" nikafanya vile na nikajibiwa hutakaa upate tena sms za promotion ya voda.
  Kesho yake nikaweka 5000/= nikatwa tena then nikawajia juu wale staff wa customer care.ndiyo mmoja wao akaniambia nipunguze jazba ila tuma neno 'toka' kwenda 15544, nikafanya vile,nikajibiwa tangu leo umeondolewa kwenye promotion ya voda 11million.so since then sijawahi kukatwa tena.
  chakufanya tuma neno "toka" kwa herufi kubwa kwenda namba 15544.
   
Loading...