Vodacom wadaiwa kuanza kupunguza wafanyakazi, ubaguzi wahusishwa

dubu

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
3,496
3,461
Heshima kwenu wakuu,

Kumekuwa na Malalamiko kwamba, kampuni ya simu ya Vodacom imekuwa ikipunguza wafanyakazi kimya kimya kila idara.

Tatizo kubwa ni kwamba anaondolewa Mtanzania na kuingizwa Mgeni kutoka nje ya nchi na anafanya kazi zile watanzania ambazo wana uwezo wa kuzifanya na wamekuwa wakizifanya.

Hivyo wafanyakazi wa Vodacom wamekuwa wakifanya kazi kwa uoga kwani hawajui kesho ni zamu ya nani kupigwa ‘ridandasi’.

Naamini Serikali itaingilia kati suala hili ili tujue ukweli ni upi kwani Serikali imekuwa ikisisitiza asiajiliwe mgeni kwenye kazi ambayo Mtanzania anaweza fanya.

Haki itendeke kwenye hili suala.
 
Kauli mbovu haitokani na utaifa wala unini, ni mtu mwenye binafsi, kwani hao wageni wenyewe huko watokako hakuna kauli mbovu?
Kauli mbovu ni mtu binafsi siyo taifa.
 
vodacom tumewanyima kibali cha ceo mkenya sababu watanzania wanaweza.. walivyo wahuni wakaajiri mmisri.. halafu serikali imepigwa chenga..

nafasi ya mtanzania kapewa mgeni tena
Yule Mkenya alipigwa chini kwa kukosa sifa stahiki pia alikuwa na kesi nzito iliyomalizwa kimya kimya.
 
ndo maana siku hizi makato yanaongezeka kila kukicha ktk ada zao m-pesa, wanatukata gharama kubwa ili wapate pesa za kuwalipa hawa waajiriwa wageni(nahisi hawa wa kuja wanataka mishahara mikubwa zaidi)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom