Vodacom tumewachoka

kwitandula

Member
May 24, 2020
30
35
Habari!

Hivi wakuu Vodocom mbona wanatuibia hivi, asubuhi nimenunua muda wa maongezi 1000 hawajakata nikaongezea 1500 ili niunge kifurushi cha wiki 2500 matokeo yake naambiwa sina salio la kutosha, kucheki salio ipo 2000 sh.500 wameikata na hakuna sms inayoonesha makato hayo.

Nimepiga customer care kwanza matangazo ni mengi mara nipige tafu, shangwe shangwena! Kha kwani hiyo customers care ni kwa ajili ya kutusikiliza na kutatua changamoto au matangazo! Haya, anakuja kupokea huyo Mtoa huduma anasema tu hiyo 500 ulikatwa kwasababu umejiunga na sport mapene sijui(sijawahi) namuuliza namna gani naweza jiondoa anajibu nakutoa mimi huku kwenye system inakera sana.

Kama kuna wadau wa voda mtapitia uzi huu tafadhali rekebisheni hivi vìpengele

1. Mpunguze kuongea tunapopiga no yenu ya customer care ili changamoto zetu zitatuliwe kwa haraka matangazo yenu tafuteni namna nyingine ya kuyafikisha

2. Mteja akilalamika kukatwa salio msijitetee kwa kusingizia kuwa kuna huduma uliyojiunga umekatwa ada na mimi mtumiaji sijawahi jiunga.

Asante!
 
Mtu anapopiga simu anataka aongee na mtoa huduma,kumuwekea matangazo mengi wala hayazingatii kwasababu akili yake ishavurugwa na changamoto anayotaka msaada huduma kwa wateja.

Kwa mfano,mtu anapiga simu kuzuia muamala wa pesa,alafu mnamuwekea maelezo meengi yasiyo na msaada kwake,hana muda wa kuzingatia matangazo ya promosheni yenu mnayomweleza ni kupoteza muda tu.
 
Kweli kabisa yani tena naona hata wanakiuka maadili TCRA waangalie ile ni huduma sio matangazo!!
 
Pia vifurushi vyao ni bei ya juu sana/ghali,na vinabadilishwa na kupandiahwa bei bila kumpa taalifa mteja.
Na wizi umeongezeka kwenye vifurushi tatizo ni mtandao ambao wengine watu wetu wengi wa karibu hasa watu wazima wanautumia lasivyo ningeuacha kabisa
 
Kwani umelazimishwa kuwa mteja wa Vodacom??
Hebu hamia mitandao "utopolo' mingine utuachie the superb and leading network in TANZANIA yetu
Sijalazimishwa na sihami ila kwenye ubovu lazima tuseme na sijasema kuwa mtandao ni mbaya may be wewe hujapata hizo changamoto
Kosoa kwenye tatizo sio kila kitu ndiyo mzee!!
 
Na mpigwe tu kummmke😂😂😂 kila siku mnalalamika tu si muhame. Kuna makampuni 5 yanayotoa huduma sawa na Vodacom. Ila mumeng'ang'ana tu kulia lia hovyo.

Jama wamefile loss katika mwaka 2019/2020 about 5.09 Billions! Hio hasara lazima nyie kenge wa maziwa mfidie!😂😂😂
 
Mnaweza kuwa na huduma nzuri upande wa data licha ya bei ghali mnazotoza ila meseji zenu za songesha, shangwena, soka letu nk zinakera, narudia tena zinakera... Mtu hajajiunga mnakomaa tu kutuma... Kwa stress hizi mtu anadhani sms ya maana akicheki anakuta songesha..

Sent from my HUAWEI SCL-U31 using JamiiForums mobile app
 
Kwani umelazimishwa kuwa mteja wa Vodacom??
Hebu hamia mitandao "utopolo' mingine utuachie the superb and leading network in TANZANIA yetu
Isifie tu, siku ukipigwa hutarudi hapa na mashairi ya kusifu na kuabudu Vodacom. Mie nilishaachana nao kitambo.
 
nawaza tusi la kukupa sema nafuta na kuandika nafuta tena aaagh maku...konyo
Tafuta pesa pimbi wewe acha kulia lia!!
Kuilisha tu simu yako na hivo vivocha unashindwa mwanaume mzima je kuilisha familia utaweza kweli??
Ninyi ndo mnaotelekezaga familia kisa changamoto ndogondogo Kama hizi za mleta mada.
 
Isifie tu, siku ukipigwa hutarudi hapa na mashairi ya kusifu na kuabudu Vodacom. Mie nilishaachana nao kitambo.
Suluhisho ndo hilo bwana, Kama huna pesa za kumudu kasi ya maendeleo ya mtandao wetu pendwa hamia tu mitandao mingine na sio kulia lia kipumbavu Kama mleta mada.
 
Back
Top Bottom