Tigo huu ni wizi! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tigo huu ni wizi!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by JAYJAY, Jul 20, 2011.

 1. JAYJAY

  JAYJAY JF-Expert Member

  #1
  Jul 20, 2011
  Joined: Oct 31, 2008
  Messages: 2,495
  Likes Received: 824
  Trophy Points: 280
  Leo mchana nilikuwa sina salio kabisa kwenye simu ,nikamuomba jamaa yangu akanitumia 250, muda mfupi nikapokea sms kutoka namba 15556 ya msimu wa dhahabu na clouds Fm huku nikitaarifiwa na hiyo sms kuwa nitaendelea kutumiwa meseji zaidi msimu wa fiesta. Nikakumbuka juzi j3 ninilipokea sms inayohusiana na suala hilohilo lakini sikuijibu, kwa kuwa mwaka 2007 walikula sana salio langu kwa mtindo huo hivyo tangu wakati huo sijawahi kujibu tena sms za aina hiyo. Ikanibidi niangalie salio nikakuta imebaki 100, yaani wamekula 150, nikashangaa sana kwa sababu sijajiunga na huduma hiyo vipi wale salio langu. Kupiga customer care naambiwa kuongea na mhusika nitalipa sh. 50 kwa kila simu ikanibidi nipige maana nilikuwa na hasira sana, kupiga namba ambayo nilipewa simu inaita halafu inakuwa kama imepokelewa simu inahesabu muda lakini muhusika haongei, ikabidi nikate simu, kucheki salio imebaki 50. Jamaa mmoja akanishauri nitume neno "ondoa" kwenda ile namba iliyonitumia sms nikajibiwa na sms nyingine ya pushmobile kuwa nitaondolewa kwenye huduma hiyo baada ya masaa 24, yaani mpaka sasa naogopa kuweka salio kwa hofu kuwa jamaa wanaweza kunitumia sms nyingine na kuendelea kula salio langu. Hivi wandugu kuna namna naweza fanya hawa wezi warudishe salio langu? Na haiwezekani mamlaka husika kuzuia kutumiana matangazo ya aina hii au ndio vigezo na masharti yamezingatiwa mara tu unapojiunga na mtandao husika?
   
 2. COMPLICATOR2011

  COMPLICATOR2011 JF-Expert Member

  #2
  Jul 20, 2011
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 255
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 33
  Unazidi kuniongezea hasira make sio tigo tu, mimi vodacom wanakata hela kila siku eti wananiwekea redio ya mziki, wanaweza kukata 200 wakasema ni kwa siku 15, hlf utashangaa baada ya siku4 wanakukata tena eti umeunganishwa upya yaani mimi nina hasira na hawa watu ila basi tu maana ndo serikali yetu, juzi mbunge Azani Zungu kaliongea hili bungeni ya kuwa makampuni ya cm ni wezi but mpaka sasa TCRA hawajasema kitu, hawa dili ni moja. Kuna jamaa kanidokezea eti CCM wameshindwa kuwalipa hela walizotumia kuwapromote wakati wa kampeni kwa kusambaza msg za kumkashifu Dk. Slaa, sasa wameamua kujilipa wenyewe.
   
 3. Butho Mtenzi

  Butho Mtenzi JF-Expert Member

  #3
  Jul 20, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 328
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Haya ndo makampuni ya cm tz wao wanananga tu bila ata kujali pesa inapatikanaje
   
 4. pumbatupu

  pumbatupu JF-Expert Member

  #4
  Jul 20, 2011
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 258
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  sasa kama wanajilipa kwa stahili hii unadhani ni sahihi? kiukweli mie nilikoma nao ilibidi nibadilishe namba ndo ikawa suluhu..sitaki hata kuwasikia..
   
 5. mopaozi

  mopaozi JF-Expert Member

  #5
  Jul 20, 2011
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 3,290
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  wasipoiba watapata wapi faida wakati wateja wamebakia laki mbili tuuu na wengi wao ni wanafunzi wazee wa kubipu na kuomba salio!!!l:mad:;p>:>?::>@?
   
 6. kingxvi

  kingxvi JF-Expert Member

  #6
  Jul 20, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 883
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  mim voda sasa na miezi 4 siwatumii wapumbavu sana kila nkiweka hela wanantumia msg za yanga sc kwa 150 msg zingine hazina hata maana nshawapigia zaidi ya mara 5 wananipa maelekezo ila nkiyafata wapi?
   
 7. M

  Mike 1234 JF-Expert Member

  #7
  Jul 20, 2011
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 1,634
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mimi nilitupa line ya simu maana ilikuwa kero,nilitumiwa sms yakwamba nitatumiwa mistari mizuri ya bibilia nikakubali,jamani acheni nilitafunwa pesa kila siku,ikabidi niwapigie simu maana kuna no; yao ya simu waliweka hiyo simu ikawa haipatikani nika piga tigo wakaniambia andika neno ondoa kwenda no iliyoleta sms,nilifanya hivyo hakusaidia,kweli tunaibiwa sana
   
 8. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #8
  Jul 20, 2011
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,106
  Likes Received: 7,363
  Trophy Points: 280
  Mimi kitu pekee nachofaidi tigo ni huduma yao ya light siku ambayo kama hivi JF niko available anytime,
  But ishanipotezea dili kibao tu,
  Juzi kati jamaa yangu mmoja alipiga intavyuu kama 3 hivi, ya 4 ambayo ndo ilikua ya mwisho aliambiwa angepigia kujulishwa muda wa kwenda,
  wiki ikapita kimya, jamaa kuwapigia ili kuwauliza wakamjibu walimpigia but hakupatikana
   
Loading...