Vodacom Tanzania: wanalijua hili? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vodacom Tanzania: wanalijua hili?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Hofstede, Jan 7, 2009.

 1. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #1
  Jan 7, 2009
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Nimekuwa na kawaida kila siku kuwasiliana na ndugu na jamaa kupitia international calls. Cha ajabu leo siku ya pili jamaa zangu wote walio katika mtandao wa Vodacom nimekuwa siwapati. Nilidhani tatizo labda ni kwa Tanzania lakini wa mitandao mingine kama, Tigo, Zain na TTCL nawapata pasi na tatizo. Nina watu kama 20 wenye namba za Vodacom hakuna mawasiliano kabisa kutokea nje ya Tanzania. Swali ni je Vodacom wameamua kuachana na simu zote zinazotoka nje ya Tanzania na hasa zile zinazotumia kadi maalum za International call au mitambo yao ina matatizo?.
   
 2. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #2
  Jan 8, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Pole sana Hofs, tatizo la mtandao wa Vodacom ni la muda sasa. Hata sisi tulio hapa Tz tunapata shida sana na mtandao huu. Sijui nini kimewasibu ila ni kama mwezi sasa mtandao wao unasuasua. Ni vigumu sana kuwa na mtandao wenye nguvu muda wote. Wakati mwingine unapiga simu kwa mtu ambaye uko naye mji mmoja ila hapatikani. Mitambo inakueleza kuwa hakuna huduma. Lakini linalokera zaidi kuhusu huu mtandao wa Voda ni bei. Yaani bei zao ziko juu kuliko mitandao mingine. Na jambo jingine linalonikera ni kuwa hivi hawa wenye kutoa huduma za simu kwa nini wanang'ang'ania promotions badala ya kupunguza gharama za huduma kikaeleweka? Promo nyingine zimekaa kimtego fulani hivi. Na pia hilo linavutia utapeli kwenye hii biashara.
   
  Last edited: Jan 8, 2009
 3. S

  Silas A.K JF-Expert Member

  #3
  Jan 8, 2009
  Joined: Apr 23, 2008
  Messages: 807
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Hofstede,

  Vodacom Tanzania wamekuwa wakitumia Gateway ya Zantel na TTCL kwa muda mrefu kwaajili kama carrier wao wa international calls.lakini hivi karibuni Vodacom group imenunua gateway yao na hivyo wanaacha utegemezi wa zantel na TTCL kwa shughuli hiyo.sasa nafikiri katika transition hapa walikuwa hawajajipanga vizuri lakini nafikiri hilo ndiyo tatizo kubwa.soon mawasiliano na ndugu zako kupitia vodacom yatarejea katika hali ya kawaida.pole kwa usumbufu ulioupata na nafikiri vodacom wenyewe (mimi si mfanyakazi wao) wana regret kwa usumbufu unaowapata watu kama nyinyi.

  Asante.
   
 4. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #4
  Jan 8, 2009
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,793
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145

  .......MMmmmmm?? You could have easly passed for their PR! teh teh
   
 5. S

  Silas A.K JF-Expert Member

  #5
  Jan 8, 2009
  Joined: Apr 23, 2008
  Messages: 807
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Lol,I think PR would have been better for me! unfortunately sikumajor kwenye PR.
   
 6. KiuyaJibu

  KiuyaJibu JF-Expert Member

  #6
  Jan 8, 2009
  Joined: Aug 29, 2007
  Messages: 769
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 45
  TCRA waliwashauri makampuni yote ya simu ya-share miundombinu ya mawasiliano pamoja lakini muafaka haukupatikana nafikiri madhara yake ndiyo kama haya;kwasababu umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu.
  Hata hivyo mimi nasubiri hiyo June,2009 ifike ili nijione urahisi,uharaka na wepesi wa teknolojia ya kisasa ya mawasiliano kwa kutumia optic fibre backbone.
   
 7. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #7
  Jan 8, 2009
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Wamenunua facilities zao lakini bado watatumia Gateway ya TTCL kutolea mawasiliano ya nje. Kumbuka earth station ni moja na ni kwa ajili ya kuwa na monitoring mechanism ya data.
   
 8. E

  Egongos Member

  #8
  Jan 8, 2009
  Joined: Nov 5, 2007
  Messages: 39
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 13
  Nafikiri kwa issue ya Vodacom Kununua Gateway yao hiyo itakuwa kwa outgoing calls only kwa ajili ya incoming calls hawawezi kutumia gateway yao. Kumbuka katika mawasiliano nchi ina country code (International Signalling Point Code-ISPC) moja tu kulingata na Taratibu za ITU-T na hiyo iko assigned kwa gateway ya TTCL. Sasa kama wamenunua gateway yao ambayo hawataweza kutumia then hilo ni tatizo lao na wataalam wao.
   
 9. Kapinga

  Kapinga JF-Expert Member

  #9
  Jan 8, 2009
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 728
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0

  kama TCRA as a national regulatory authority walishauri basi wanashangaza sana..huku ulaya its passed in the telecoms regulations kwamba lazma watu washare facilities.. (from minara to gateways.....especially kwa new entrants in the game..) kama ni kweli unayoyasema basi TCRA wanabangaiza tuu...back to the issue of international calls..kweli hata mimi yamenitokea sana napojaribu kupigia ndugu wenye line ya voda ..na celtel ile issue ya kutuma sms mbili mbili internationally especially uk naona bado inaendelea...tatizo ni nini??
   
 10. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #10
  Jan 8, 2009
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0

  Mkuu Kapinga hapo umeongea, Unapokuja kwenye suala la mawasiliano linakuwa si only business interest but public interest, Kitendo cha kutokuwa na mawasiliano ya uhakika miongoni mwa wateja ni kuwanyima haki muhimu sana, umefika wakati sasa viongozi wetu wawe hata wanajifunza toka kwa wenzetu si kwenye vijiwe vya kahawa. Hawa jamaa wamenikatisha mawasiliano kabisa na ndugu na jamaa nafikiri TCRA sasa iwe kwa ajili ya Public interest si hawa wasanii wanaoshindana. Promotion nyingi huduma duni. VODACOM kama wameshindwa wasiwarubuni watu wengi kujiunga nao kwani ni utapeli sasa, Inabidi watu wawe na line mbili au tatu which is expensive sana. Imebidi niwashauri jamaa zangu wawe na alternative line si kutegemea VODACOM ambao mpaka leo mtu ukipiga kutoka nje ya Tanzania inakuwa kimyaa, hamna unalolisikia.
  Au kwenye promotion zao waweke wazi ni kwa mawasiliano ya ndani tu ili watu wenye jamaa zao nje waepukane nao.
   
Loading...