Vodacom Tanzania nini Hiki Mnafanya? Niwashitaki?

Vodacom Tanzania nini Hiki Mnafanya? Niwashitaki?

GenuineMan

JF-Expert Member
Joined
Jun 13, 2017
Posts
7,870
Reaction score
18,598
Vodacom Tanzania huu Ujumbe wenu mlionitumia leo asubuhi umeniumiza sana kihisia na kiakili. Mimi na maswala ya uchawi wapi na wapi?



Screenshot_20261025_092254_Messages.jpg

​
 
Vodacom Tanzania huu Ujumbe wenu mlionitumia leo asubuhi umeniumiza sana kihisia na kiakili.
Mimi na maswala ya uchawi wapi na wapi?​


View attachment 3698005
Mie walinipigia na no yenye tarakimu 6 za mwisho hizi.......505050 nikapokea, nikasikilizishwa tangazo la "Chemba " kwakuwa sikuwa na interest nalo nikakata simu.

Masaa 2 baadaye nashika simu , nikakuta ujumbe wa kunipongeza kujiunga na huduma za Chemba na tayari washakata salio, kisha wakanitumia ujumbe wa namna ya kujitoa kwenye huduma hiyo.
Kuanzia Siku hiyo, salio lilikatwa kila siku mpaka likaisha. Ni mwezi wa 5 sasa sijawahi kuongeza salio wala kutumia namba yangu kwenye m pesa japo line ipo hewani.
Wacha nikomee na mitandao mingine.
 
Mie walinipigia na no yenye tarakimu 6 za mwisho hizi.......505050 nikapokea, nikasikiliziahwa tangazo la "Chemba " kwakuwa sikuwa na interest nalo nikkakata simu.
Masaa 2 baadaye mashuka simu , nikakuta ujumbe wa kunipongeza kujiunga na huduma za Chemba na tayari wasakataji walio!, kisha wakitumia ujumbe wa namna ya kujitoa kwenye huduma hiyo.
Siku hiyo, salio lilikatwa kila siku mpaka likaisha, ni mwezi wa 5 sasa sijawahi kuongeza salio wala kutumia namba yangu kwenye m pesa japo line ipo hewani.
Wacha nikomee na mitandao mingine.
Chemba la choo au
 
SMS Marketing inahitaji udhibiti, imekuwa kero sana.
Sio sawa simu yangu kutumika kama ubao wa matangazo bila idhini ya mteja.

Inapaswa kuwe na makubaliano (tena mkataba wa muda mfupi) baina ya mteja na mtandao husika ukionyesha manufaa atakayopata mteja kutokana na usumbufu, kuingiliwa uhuru n.k.

Hii mtandao inaibia wateja kupitia huduma duni za ujanjaujanja na kuuza matangazo
 
Back
Top Bottom