Socratic
JF-Expert Member
- Dec 18, 2014
- 568
- 308
Ndugu zangu hii imekaaje?
Nililipia kwa mpesa kifurushi cha Azam Tv. pamoja na kupata receipt ya malipo toka kwa selcom. Sikupata kifurushi wala salio halikuingia kwenye account yangu.
Niliwapigia Azam tv wakasema swala hilo linawahusu Vodacom. Nikawapigia Vodacom huduma kwa wateja wakadai swala hilo niwatafute Selcom. Selcom nimepiga sana huduma kwa wateja bila mafanikio.
Nimewauliza Vodacom huduma kwa wateja waniambie ofisi za selcom zilipo niwafuate wakajibu hawajui ofisi zilipo! Hii inawezekanaje? Kinachonitia hasira ni kuona nalazimika kufuatilia mwenyewe selcom wakati mi sina mkataba na selcom, jambo hili kwa mrazami wangu lilipaswa kushughulikiwa na Azam Tv wao ndio wanajua makubaliano yao na Vodacom au Selcom.
Tangu mwezi wa pili hadi leo nazungushwa sijarudishiwa pesa yangu.naombeni mawazo yenu namna ya kupata pesa yangu