Vodacom Premier League (VPL) Simba SC dhidi ya Biashara United, Uwanja wa Taifa

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Patashika ya Ligi Kuu ya Tanzania Vodacom Premier League VPL, kuendelea kusukumwa leo February 22, 2020 ambapo Wekundu wa Msimbazi, Mnyama Mkali, Simba SC wanawakabili Biashara United kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Simba SC ambayo ndo vinara wa Ligi Kuu, kwa kuwa na alama 59, kwa michezo 23, wanaingia uwanjani wakiwa na rekodi ya kuvutia msimu huu ya kuandikisha ushindi kwa asilimia 99% ambapo leo wana kazi moja tu kupata ushindi na kuweza kukusanya alama tatu muhimu ili kuzidi kujikita kileleni mwa VPL.

Nao Biashara United, wakiwa nafasi ya 9 kwa alama 32 kwa michezo 23, wanaingia uwanjani wakiwa na kumbukumbu ya kuchapwa mabao mawili bila majibu kwenye mzunguko wa kwanza wa VPL, katika uwanja wa Karume mjini Musoma ambapo leo wataendelea kugawa alama au watajituma na kuzuia ushindi dhidi ya Simba SC?

Yote haya ni mwisho wa dakika 90 kukamilika. Usikose Ukaambiwa.

Kumbuka kipute ni kuanzia saa 1: 00 Usiku.

STARTING XI:

Aishi Manula, Shomari Kapombe, Mohamed Hussein, Pascal Wawa, Erasto Nyoni, Jonas Mkude, Clatuos Chama, Luis Miquissone, Maddie Kagere, John Bocco, Francis Kahata.

SUB:

Beno Kakolanya, Gadiel Michael, Kennedy Juma, Grason Fraga, Sharaf Shiboub, Deo Kanda, Hassan Dilunga.


•••===============••••••

Klabu ya Simba imeendelea kujikita kileleni mwa ligi kuu Tanzania, baada ya kuibuka na ushindi wa mabao matatu kwa moja dhidi ya Biashara Utd

Ikicheza kandanda safi na kuvutia huku wakitawala mchezo kwa muda wote, Simba walianza kuhesabu bao la kwanza likifungwa na kiungo mshambuliaji Luis Miquissone, akiachia kombora kali lililomshinda golikipa wa Biashara katika dakika ya 35'

Mabao mengine yalifungwa na Meddie Kagere 68' na Francis Kahata 88' huku la kufutia machozi kwa Biashara likifungwa na Novatus Dismas 71'

Kwa matokeo hayo Simba imefikisha alama 62 kwa michezo 24 huku Biashara Utd ikibaki na alama 32 kwa michezo 24'

VPL, FT; Simba SC 3-1 Biashara Utd

......Ghazwat...

85176956_132061764976912_3611153242060934894_n.jpeg
84977521_514081432627433_1302693593900409069_n.jpeg
 
Kwa Simba hii ya kiwango cha CAF, leo anapiga Biashara kama alivyopiga waliotangulia
 
Back
Top Bottom