Vodacom Premier League (VPL) Azam FC dhidi ya Simba SC, Uwanja wa Taifa

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Hello Tanzania na Duniani Kote

Patashika ya Ligi Kuu Tanzania, Vodacom Premier League (VPL), kuendelea kuvurumishwa leo Jumatano ya March 4, 2020, ambapo Wana Lambalamba Azam FC, wanawakabili Wekundu wa Msimbazi, Mabingwa wa Nchi, Simba SC kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Mchezo unatarajiwa kuwa mkali na kusisimua kwa muda wote wa dakika 90 kutokana na ubora wa vikosi vya timu hizo, ambazo zimesheheni nyota kadhaa wakali na wa kigeni.

Azam FC wanasaka ushindi na alama tatu muhimu kwa ajili ya kufuta unyonge wa kufungwa mara kwa mara, vile vile kujiweka sawa katika mbio za kuifukuza Simba katika kuwania taji la VPL.

Kocha wa Azam FC Aristica Cioaba amesema hatakubali kupoteza mchezo wa leo kwa kuwa mipango yake ni kuifukuzia Simba mpaka mwisho, hivyo amefanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza katika michezo iliyopita hasa umaliziaji.

Simba SC inaingia uwanjani ikijivunia rekodi ya msimu huu kuifunga Azam FC mabao 4-2 kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii, huku wakichapwa bao 1-0 kwenye Ligi Kuu mzunguko wa kwanza.

Kocha wa Simba Sven Vanderbroeck amesema mchezo utakuwa mgumu kutokana na kila mmoja kuwa katika nafasi za juu kwenye mbio za kuwania ubingwa, lakini amewahakikishia Wanasimba kuwa wanakwenda kupambana kuendeleza ushindi ili kufikia lengo la kutetea ubingwa wa VPL.

Ni game ya kukata na shoka, ambapo dakika 90 zitaamua. Kumbuka mchezo ni kuanzia saa 1:00 usiku.

Msimulizi wenu ni Ghazwat pamoja na WanaJF..Kulipewa Mwana Kulitaka Mwana.

FB_IMG_1583315385537.jpeg
FB_IMG_1583315559671.jpeg
FB_IMG_1583315443857.jpeg
 
Taarifa Muhimu;

Leo hakuna kusalimia kwa kupeana mikono kwa viongozi wa soka na wachezaji uwanjani hivyo salamu itakuwa kwa ishara, ikiwa ni hadhari ya kujikinga na virusi hatari vya Corona
FB_IMG_1583321650108.jpeg
 
Back
Top Bottom