Vodacom nawahama leo nimewachoka!

Vodacom nawahama leo nimewachoka!

wajanja tusharudi nyumbani kitaaambo, TTCL ndo geto langu nalala nalo naamka nalo.
 
Vodacom ni mtihani...

Screenshot_20190721-083503_Phone.jpg
 
Yaani shilingi elfu mbili unapata MB 512, Jamani Jamani vodacom, Halafu sasa ajabu na kweli ni kwamba katika kuwataarifu wateja wao juu ya mabadiliko hayo wametumia maneno ''tumeboresha''.....

Wakuu tupeane ushauri hapa tunahamia wapi... ?
Mimi nahama Voda walahi, ila sijui niende wapi kwenye ahueni ya bando la internet
Njoo tigo gb2 moja mchana moja uck kwa 1500 tu line ya chuo lkn
 
Karbu ttcl
Yaani shilingi elfu mbili unapata MB 512, Jamani Jamani vodacom, Halafu sasa ajabu na kweli ni kwamba katika kuwataarifu wateja wao juu ya mabadiliko hayo wametumia maneno ''tumeboresha''.....

Wakuu tupeane ushauri hapa tunahamia wapi... ?
Mimi nahama Voda walahi, ila sijui niende wapi kwenye ahueni ya bando la internet
 
Me voda. Imebaki kwajili ya mpesa na kupokea cm za wazazi basi
 
VODACOM MNATUZOEA VIBAYA WATEJA WENU, MNATUNYONYA!

VodaCom.......VodaCom....VodaCom....!
Vodacom Tanzania

Tafadhari sana Kampuni kumbwa kama nyinyi kila siku mnajinasibu kuwa ni kampuni na mtandao unaongoza Tanzania. Sasa kwenu nyinyi wakubwa uendeshaji wa kibiashara wa mtandao wenu hukoje???? Kwasababu Yaani badala ya kuwa wenye kujali wateja wenu kwa kuwadumisha waendelee kutumia huduma zenu kwa huduma zenye bei nafuu lakini imekuwa wakubwa mwenye wateja wengi ambao sasa Mnatunyonya wateja wenu. Sasa kila siku mnaongeza tu gharama za kutumia mtandao wenu Yaani kifupi hamueleweki nini mnatafuta. Kwasababu kama biashara mnafanya vizuri na wateja wengi mnao sasa kwanini mnashindwa kuwa “Customer-care Oriented” nyie mnakuwa tu “Profit-care oriented”. Yaani kifupi mnatunyonya sana wananchi wa kawaida kama sisi. Kwa mabadiliko haya mlioyafanya ya mabando ni wazi kuwa mnatunyonya hakuna kingine cha kusema zaidi ya unyonyaji huu.
*Ya kawaida mambo ya ajabu ni haya:
i). Tsh.5,000= 2GB (kwa masaa 48)
ii).Tsh.2,000= 1GB (kwa masaa 24)
*Ya UNI-OFFER ndio maajabu huko yaani ni unyonyaji mtupu:
i). Tsh.3,000= 1.2GB( kwa siku 7)
ii).Tsh. 2,000= 512GB (kwa siku 7)
iii).Tsh. 1000= 500GB(kwa siku 7)

MY TAKE:
Yaani nawashauri sanaa VodaCom-Tz Yaani kama mnashindwa kuendesha huu mtandao kwa gharama ambazo ni rahisi kama wenzenu wanavyotumia nawashauri muache kujinadi kuwa ni kampuni na mtandao unaongoza Tanzania, kwasababu ninawasiwasi hata kwa upangaji wa bei zenu za data zenu sizani kama mnatumia njia hizi kuu za uuzaji..1. COST-PLUS METHOD 2.COMPETITIVE COMPARING METHOD 3. WHAT MARKET WILL BEAR METHOD.

Kwasababu kama mngekuwa mnatumia hizo njia msinge tunyonya hivyo kwakuwa mngeweza kuwa sawa na wenzenu kama TTCL au makampuni mengine kwa mfano gharama za TTCL ni za chini kweli:
i). Tsh. 1,500 = GB 1(kwa siku 7)
ii). Tsh.2,500=. GB 2.2( kwa siku 7)

Najua TTCL ni ya serikali lakini hata kama nyinyi ni tofauti na hawa haiondoi uhalalali wa nyinyi kwenda kinyume na tofauti sanaa na Mitandao mengine. Yaani hapa kuna Tatizo.

MWISHO:
Tegemeeni kupoteza wateja wengi sana hasa wale tunaotumia mabando ya internet na ambao ni wengi zaidi kama Hamtabadilika.
 
Kwasasa tuwatafutie nao jina baya kama la tgo,tuwaite ebola au kimeta
 
tatizo mnaongea tu vitendo sifuri.

mimi nimeyaacha nina mwezi sasa,na nilikuwa mteja wao wa 30000 kwa mwezi.
 
Ukija halotel ndio utachoka, zamani jero tulikuwa tu napata mb 500 kwa wiki vifurushi vya chuo. Leo nmeshangaa wamevinyambua eti mb 250 na dakika za halotel 30, hivi nani ana shida na dakika za kupiga?
nunua mega bundle buku gb 1 kwa wiki
 
Saba saba ndio alikuwa mwisho wa kutumia huu mtandao wa Voda.
Kuna tabia ya kumwambia mteja hujazima data hii yote ni mianya
 
Njoo tigo gb2 moja mchana moja uck kwa 1500 tu line ya chuo lkn
Nimefika voda nikitokea tigo (nina laini za chuo za hawa wote), niliwahama baada ya kupunguza vifurushi vya chuo. Sijajua Kama wamesharudisha offer kwa kiwango hicho. Ngoja niangalie hapa.
 
Halotel 1000 gb1 line ya chuo
Hata line ya kawaida inapiga kazi nafikiri ila mpaka kwenye ununue kwenye Halopesa. Hawa jamaa wanamchezo mmoja mchafu sana. Hilo bando halitoboi siku 3 limeisha. Halotel wachenzi sana, bora niangalie Tigo japo spid yake ndogo lakini bundle linakaa.
 
Back
Top Bottom