Vodacom na CRDB wanavyoibia wateja!

Vodacom na CRDB wanavyoibia wateja!

Jaribu kuomba huduma ya CRDB SIM BANKING kupitia vidacom kwa wakati huu utajibiwa kuwa hakuna huduma.
sasa nenda kwenye salio lako la muda wa maongezi...unakuta limekatwa kiasi kisichopungua Tsh 20...sina hakika kama kuna senti iliyoingia Serikalini.
Asante kwa kutuelimisha. But, nashauri uzi huu uhamishiwe huko Habari na Hoja mchanganyiko. Sio humu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hawa voda ndio wahuni sio CRDB,
CRDB hawaruhusu mitandao mingine ya simu hususani Halotel kwenye Simu bank yao. Hivyo ni lazima kuna kitu kati yao na VodaCom kwenye wizi huo. Ni wakati sasa wakalazimishwa kutumia mtandao wetu wa TTCL na Halotel!
 
me pesa zangu zinakaa m.pesa nkitaka muda wa maongezi nanunulia hapo, nna kama mwaka cjawah nnua vocha.
 
CRDB eti ukicheki tu balance kwa Sim banking wanakata tshs 364.. Kila ukicheki balance wanakata hela hiyo.. Ni hatari sana huo ni wizi..!! Hivi kucheki balance kwa simbanking kwann wana chaji? Hela yangu, simu yangu, data yangu, hivi kweli hata kucheki balance unanichaji tshs 364..yaani kila ukicheki balance wanakata hiyo hela.. 😡😡😡😡
voda wezi hasa kipindi hiki rostam anataka kuuza hisa..ila kucheki salio si ni sawa na kuingiza atm card kwenye atm!!?..kama ndivyo nadhan kuingiza atm card wanakata hela hiyo
 
Jaribu kuomba huduma ya CRDB SIM BANKING kupitia vidacom kwa wakati huu utajibiwa kuwa hakuna huduma.
sasa nenda kwenye salio lako la muda wa maongezi...unakuta limekatwa kiasi kisichopungua Tsh 20...sina hakika kama kuna senti iliyoingia Serikalini.
kamshauli jiwe awakoromee wataacha wewe si fito ya ndani
 
Mimi kuna mtandao nauhifadhi, mpaka nipate uhakika kama wao ndio wananichezea ama ni simu yangu ndiyo inashida. Ni hivi,kila nikijiunga na kifurushi kiwe cha siku , wiki ama mwezi...laini yangu inapoteza mawimbi ya mtandao...inaniwekea ka alama kekundu ka eksi( x). Vifurushi vikiisha wala hako ka alama sijui kanapotelea wapi...nikiweka muda wa maongezibila kujiunga kifurushi yaani mtandao unakuwa full kiasi cha kushangaza.
=====
Nikirejea kwenye mada:
Sidhani kama ni wizi...maana unapobonyeza key kwenye simu yako, mitambo kuanzia minara ya simu, satelati, servers, nubs, routers, na maoperators( kama siyo automated) vina/ wanakuwa active kukujibu hitaji lako. Hapo...kuna li'algorithim' lakuchuja taarifa yako ...ambalo linaendeshwa kwa speed kubwa...kiasi cha kuhitaji matranzistar, kapasita, mikrokontrola na kadhalika yanayolibeba kupozwa kwa haraka zaidi. Kwa maelezo hayo...ukijaribu kupiga hesabu ya umeme unaotumika wa wewe kutuma ujumbe wa kuuliza salio kwenye mtambo huo...ukaongeza na mishahara ya kukarabati mitambo, ukaongeza riba za benki( hiyo mitambo mingi wamekopa)... unaweza kukuta unawahurumia hasa kipindi hiki ambacho udanganyifu wa kulipa kodi umedhibitiwa kwa kiasi kikubwa....( nawaza tu...namna hiyo mitandao ya simu inavyoweza kujitetea)
 
Pilitics again!!
Sio kila kitu kinajadiliwa au kuamuliwa kisiasa.
Tukiendelea kuendekeza siasa kiasi hiki tutakuwa nchi maskini sana.
Toa ushauri au mawazo yako nini kifanyike, ukiitaja CCM au chama chochote haiondoi ili tatizo la walaji(consumers) kudhulumiwa na watoa huduma(service providers).
Hahahaàa mkuu usijifanye huoni.
 
Jaribu kuomba huduma ya CRDB SIM BANKING kupitia vidacom kwa wakati huu utajibiwa kuwa hakuna huduma.
sasa nenda kwenye salio lako la muda wa maongezi...unakuta limekatwa kiasi kisichopungua Tsh 20...sina hakika kama kuna senti iliyoingia Serikalini.
pesa ya wizi haikatwi kodi.
 
Hili jambo mkuu ungelifanyia utafiti kwanza. CRDB umewatuhumu bure wanaokata ni VODACOM, kuondokana na hii kero mimi nilijiunga Simbanking kwa kutumia HALOTEL sikatwi hata sumni. Nasikia pia TIGO na hawakati.
Yeah ni kweli, mfano hata AMANA Bank ukiwa na sim banking services kwa halotel haukatwi chochote

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hili halijaanza leo ni suala la siku nyingi sana labda kama umeaanza kutumia huduma hii leo, na sio CRDB na VODA tu bali ni suala la mitandao yoote kwa namna tofauti tofauti na kuna maada nyingi sana humu toka 2010 zinalalamikia wizi huu aina nyingine ya wizi wa kwenye huduma za atm pale transaction inapokuwa cancelled. Upo pia wizi kwenye speed za mitandao, mtandao unasearch dk10-20, usiponunua kifurushi pia na ukaacha data on imekula kwako.. TUNAHITAJI KUAMKA KUWEKA MAMBO SAWA.
Ni uhuni unaotakiwa kukabiliwa
 
Back
Top Bottom