Vodacom na bado mtafilisika kabisa

Vodacom na bado mtafilisika kabisa

Ciprofloxacin.

JF-Expert Member
Joined
Apr 15, 2015
Posts
1,583
Reaction score
2,702
Kampuni kubwa ya kimataifa haina mikakati ya kibiashara,mnachekesha mno,na kama hakuna MTU anayewahujumu basi pigeni chini management yote ya "Sales and Marketing".
yaani nyie mna tabia zote za kichawi, kila siku mnabuni mbinu za kuwakamua wateja wenu,matokeo yake mnapoteza zaidi ya mil 200 kila wiki,Mteja aliyekuwa akipata MB au vocha kwa sh 500 per week ,sasa hivi mmeweka eti sh 20,000 kwa mwezi,mnadhani pesa zinaokotwa?
kwa hiyo mmepoteza zaidi ya wateja 100,000 ambao mlikuwa mkipata zaidi ya mil 30 kwa siku faida tu,after tax payment, 100,000 x 300=30,000,000.
nawafahamu mno aina ya watu mliowaajiri,lazima mfilisike tu,sijui walisoma uchumi wapi,kwa tuliosoma uchumi tunatambua slogan hii " the less money,the more money, the more money, the less money".
 
Natoka Fb kusoma lalamiko, naingia JF nakuta lalamiko. Voda wajiangalie
Screenshot_2018-05-20-00-19-57.jpg
 
Nikiwa kama mtumiaji wa Voda nasema voda ndio mtandao wenye viwango nchi hii kama unataka MB 500 na unaish Dar kuna kifurushi cha Dar mb 500 instagram,whatsapp and facebook ni bure kwa sh 500
 
Voda wamebadilisha vifurushi vyao vya (ya kwako tu) bila kutazama vizuri uwezo wa wahusika, (watumiaji) mtu aliyekuwa anapata bundle la Gb 3 kwa tsh 2000 kwa siku 5 sasa anapata bundle hilo kwa 30,000.
Ni vema wangepunguza kiasi cha bundle kuliko kuongeza gharama.

Ukiwauliza katika page yao wanakujibu kama watoto wadogo hawana maelezo ya maana, na baada ya muda wanafuta maswali yote magumu kwao. Nimeachana nao mwezi wa tatu sasa.
 
Mara kadhaa nimekua nukipanga kuipiga chini line ya voda lakini naishia kuwapa nafasi nyingine, lakini safari hii ntafanya kweli.

Halafu siku hizi wameanza utapeli. Walianzisha promosheni ya TUSUA MAPENE. Utapeli mtupu. Tofauti na wenzao wa TIGO, washindi wao wa mara ya mwisho wanatokea mkoa wa Ruvuma hata kama kwa sasa wapo maeneo tofauti yaani Korogwe na Njombe.

Reaction ya washindi walipopigiwa simu ilimshtua Dada Materu aliyekuwa anawapigia washindi. Cha ajabu sana afisa kutoka Gamming Board of Tanzania alibaki anang'aa macho kama picha fulani hivi. Kilangila.
 
Nikiwa kama mtumiaji wa Voda nasema voda ndio mtandao wenye viwango nchi hii kama unataka MB 500 na unaish Dar kuna kifurushi cha Dar mb 500 instagram,whatsapp and facebook ni bure kwa sh 500

Mkuu umenicha njia panda ukivomalizia. Hiyo '..bure kwa sh 500' kama sijaielewa
 
Hawa Vodacom Tanzania nilishaacha kununua vifurushi vyao. Nimebaki natumia kwenye Mpesa tu.
Mara ya mwisho nimejiunga na kifurushi cha dar supa UNI wakanipa Data GB1 na madakika, ukiwasha data simu inasoma 4G ila huwez ku-browse website yoyote (hata gugo iligoma) nikahisi labda niko location mbaya nikaenda maeneo mengine pia mambo ni hayo hayo. Hadi wiki inaisha sikumaza hata MB 1. Nyie voda nyie Mungu anawaona
 
Back
Top Bottom