Vodacom mtandao usiomjali mteja

Vodacom mtandao usiomjali mteja

Nimewapigia jioni hii wanasema hela iko hewani haijafika kwao wala kwangu haipo hivyo niwe mpole
Ha ha haaa! Hata sisi mawakala ndo wanavyotwambiaga hivi! Hivi hela inakaa vipi hewani? Hela ni lazima ukae kwenye account! Kqma haipo kwenye account ya receiver basi imebaki kwenye account ya sender, otherwise ipo kwenye account ya Voda. Sasa inakuwaje hewani? Kwenye account ipi? Inaelea tu! Ha ha haaaaa! Matter core yao Vodacom!
 
Mm nikinunua double bundle huwa siipati hyo double,sijui ni kwangu tu ama.
 
Mara mbili nimepata shida na mpesa katika kununua LUKU na kulipia AzamTV. Ndipo nilipogundua selcom POS. Yaani hii ni moto mara moja.
 
pole yenu ambao bado mpo kwenye huo mtandao mimi sitaki hata kuwasikia,mimi nilishaiharibu kadi yao kwasababu ya hasira kila siku matukio hayaishi,hakuna siku inaisha bila ya voda kuniliza.ukituma pesa haifiki kwa wakati,ukitoa pesa sasa ndiyo kivumbi meseji hawakutumii mara unaambiwa imepotelea hewani ilimradi tu upoteze muda wako kufuatilia,njoo kwenye bando sasa ndiyo ulaghai mtupu GB1 inaisha kwa kuchati kwenye facebook,jiroge kwa kuweka vocha bila kujiunga kifurushi uone walivyokuwa na uchu wataitafuna ndani ya muda mfupi tu hatakama uliweka vocha ya shilingi elfu kumi,ukiwauliza sasa badala ya kukuuliza unatumia simu gani wao watakujibu pesa yako iliisha kwasababu uliweka data on,"nawekaje data on wakati simu yangu ni nokia jeneza".
 
Bora ww mkuu,mi dada angu aliweka mpesa mil 2 ili ipelekwe bank mana alikua na marejesho,cha kushangaza mpk leo hela haijafika bank toka tr23 ya mwez jun,kafatilia mpk kacho jibu la maana hawana,,na kule bank wataendelea kuhesabu penat kwa kua kachelesha rejesho,yaan hata hatujui tufanyeje
 
voda ni mtandao mzuri ila wameanza kuniudhi sasa, toka ijumaa nimeenda kurenew laini yangu ya kazi mpaka leo registration failed, au wanataka nihame mtandao
 
Kusema ukweli mimi hela niliyopoteza kupitia huduma za Vodacom haisemeki. ilimradi sasa nimegundua tupo wengi tunaokereka na mtandao huu. Nafikiri ufike wakati sasa tupige kampeni ya kuukimbia huu mtandao.
 
Bora ww mkuu,mi dada angu aliweka mpesa mil 2 ili ipelekwe bank mana alikua na marejesho,cha kushangaza mpk leo hela haijafika bank toka tr23 ya mwez jun,kafatilia mpk kacho jibu la maana hawana,,na kule bank wataendelea kuhesabu penat kwa kua kachelesha rejesho,yaan hata hatujui tufanyeje

Peleka mahakamani washike adabu
 
Mimi mpaka sasa nilimtumia mtu qa Airtel laki na 20 kutoka Mpesa nikiwafata ni porojo tuuuu! Na zaidi ya mwezi na nusu sasa imebidi line ya voda nitunze makumbusho
 
Back
Top Bottom