Wadau napenda kupata maoni kuhusu WIZI wa dhahiri kabisa unaofanywa na vodacom kupitia MPESA. hawa jamaa nashindwa kuwaelewa pale wanapokukata sh. 200 unapochukua (sio kununua) muda wa maongezi toka kwenye akaunti yako ya MPESA. Hivi hii ni haki? Ukinunua sh 500, inabidi uwe na 700 ili ukatwe 200. Hawa jamaa naona wananufaika na kupata super profit kutokana na mbinu zao za ujanja ujanja na wizi wizi tu.