Vodacom kujitoa kudhamini miss tanzania......

only83

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
5,343
2,525
...Kuna taarifa zimeanza kusambaa kuwa VODACOM-Tanzania inaweza ikajitoa kudhamini Miss Tanzania muda si mrefu watatoa taarifa rasmi.Akiongea Meneja Masoko wa Vodacom ndugu George Rwehumbiza alisema tayari barua ya kuonyesha wazo lao la kutaka kujitoa wamekwisha liwakilisha kwa Mkurugenzi wa Rino Agency ndugu Hashim Lundenga.Pengine hii inaweza kuwa ni pigo kubwa kwa waandaaji wa shindano hili na inaweza kuwa ndio mwanzo wa Hashim Lundenga kupoteza sehemu ya mapato yake kwa kiasi kikubwa.Alipotafutwa ili kutoa maelezo juu ya hili hakuweza kukubali wala kukataa juu la hili zaidi ya kutoa maelezo marefu yasiyo jibu swala husika.

source:Mwananchi
 
kwani kabla ya vodacom wallikuwa wanadhaminiwa na nani? Hata hivyo mashindano yenyewe hayana tija. Rene Meza keshaliona hilo
 
Kwani mdhamini alikua vodacom peke yake? Sioni hata umuhimu wa shindano hili ilobaki basi tuu.
 
SIO TETESI NI KWELI...Rene Meza aliuliza.... Vodacom tuna sponsor v2 vipi? Binti Makamba akajibu... Ligi ya Bara,Miss TZ etc...
Shs.ngapi? Billion 1 kila event...
Rene Meza akajibu....Khaaa yaani kitu cha siku 1 tu shs.Billion 1 FUTA FUTA FUTA HIYO... LOL...
 
Mmh nahc ww ulikuwepo Mliman City cku ile...umecopy na kupaste km ilivyo.
SIO TETESI NI KWELI...Rene Meza aliuliza.... Vodacom tuna sponsor v2 vipi? Binti Makamba akajibu... Ligi ya Bara,Miss TZ etc...
Shs.ngapi? Billion 1 kila event...
Rene Meza akajibu....Khaaa yaani kitu cha siku 1 tu shs.Billion 1 FUTA FUTA FUTA HIYO... LOL...
 
Asante Mungu hayo mashindano ya Miss Tanzania hakuna cha maana zaidi ya ukahaba ni wakati mzuri serekali kupitia vyombo vyake wakayafutilia mbali mabinti wetu badala ya kutuvalia vichupi wakazane kupiga shule.
 
Hakyanani uncle Lundenga kama ni kweli Vodacom wanataka kukuharibia mradi wako lo!
 
Wakitoka voda poa tu tutapata wengine wadhamni wengi sana wanatafuta mileage na penetration!watajuta baaadae wakitutosa!!
 
Aaaaaah kwani wadhamini ni wao tu!!!!!!!!!!udhamini ni kama kiti cha daladala akishuka mwingine anapanda..
 
Hakuna cha Rene wala nini atachemsha tu maana kasi yake haina support na pia yuko pekeyake atachemsha tu
 
Back
Top Bottom