Vocha za simu zinatengenezwa wapi?

SUTAGI-

JF-Expert Member
Nov 9, 2018
269
511
Habari zenu wadau mnaotumia simu kwa matumizi mbalimbali. Mimi pia nawashukuru Wazungu kwa kuleta hii technolojia ya kuwasiliana kirahisi zaidi.

Pamoja na hayo najaribu kuwaza hizi vocha za simu zinatengenezwa wapi? Je, ni kama zinavyotengenezwa pesa kwamba sisi kama nchi (Tanzania) hatuwezi kutengeneza pesa zetu?

Ni teknolojia ipi inatumika kutengeneza vocha? Kuna historia yoyote ile ya kufoji vocha zikafanya vizuri au watu kubuni namba za vocha zikakubali kuingia kwenye simu?

Nawasilisha.
 
Kwenye hesabu kuna topic moja ina serials and sequence ukiisoma vizuri na kuielewa basi utaelewa vizuri,Kiufupi tu ni kwamba hauwezi kutengeneza wala kubuni zile tokeni,Wao wenyewe wenye kutengeneza izo vocha wao wenye wenyewe hawawezi kuchukua vocha hadi ziingizwe kwenye system
 
  • Thanks
Reactions: apk
Kumbe ni mpaka ziingizwe kwenye system! Ndiyo maana hakuna udukuzi. Maana wabongo wangekuwa washapiga pesa hapo.
Nashukuru kwa michango yenu
 
Sijui zinatengenezwa wapi, ila itakuwa ni hapa Tanzania maana miaka ya nyuma zile vocha za karatasi nyepesi zilikuwa zinajazwa kwa wizi kwenye sim card za wafanyakazi wa voda, wewe ukinunua vocha unaweka unaambiwa imetumika.
 
Zile wanaprint tu karatasi, sema no hadi iwe activated na wao ndo utaitumia
 
Back
Top Bottom