Viwanja vya Michezo twavitaka, lakini kutoa Bilioni 10 kukarabati viwanja vilivyoporwa na CCM ni wizi mwingine

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
39,803
71,229
Serikali imesema imetenga shilingi Bilioni 10 kwa ukarabati wa viwanja kadhaa vya michezo ambavyo kwa sasa vinamilikiwa na CCM.

Kiuhalisia viwanja hivyo vilijengwa na wananchi wakati wa chama kimoja kwa michango, makato kama ushuru na kodi mbalimbali kwenye Halmashauri zao lakini vikaporwa na CCM baada ya kuanza vyama vingi.

Sasa wameshindwa kuvihudumia lakini ndio wanakusanya mapato na leo wanataka hela za serikali zikakarabati viwanja hivyo na mapato bado yanaendelea kuchukuliwa na CCM.

Huu ni wizi wa mchana kabisa na sio wa kunyamaziwa. Kama wameshindwa kuvihudumia basi wavikabidhi kwenye council vilipo.
 
Kwan CCM sio wananchi?

Mbona Zitto Kabwe na Dr. Slaa hawadai mgao wowote CDM?

Walioondoka CCM baada ya kuanzishwa Kwa mfumo wa vyama vingi waliondoka Kwa hiyari Yao.
 
Serikali imesema imetenga shilingi Bilioni 10 kwa ukarabati wa viwanja kadhaa vya michezo ambavyo kwa sasa vinamilikiwa na CCM.

Kiuhalisia viwanja hivyo vilijengwa na wananchi wakati wa chama kimoja kwa michango, makato kama ushuru na kodi mbalimbali kwenye Halmashauri zao lakini vikaporwa na CCM baada ya kuanza vyama vingi.

Sasa wameshindwa kuvihudumia lakini ndio wanakusanya mapato na leo wanataka hela za serikali zikakarabati viwanja hivyo na mapato bado yanaendelea kuchukuliwa na CCM.

Huu ni wizi wa mchana kabisa na sio wa kunyamaziwa. Kama wameshindwa kuvihudumia basi wavikabidhi kwenye council vilipo.
Hivi viwanja ni mali ya umma, tukitaka virudi kwa umma CCM iondolewe madarakani.
 
Mbaya zaidi ni kuwa hawawezi kuvihudumia. Nenda mfano Ali Hassan Mwinyi Tabora, bila hata aibu kiwanja kimeoza huku wanachukua mapato yote wao. Na sio hicho tuu, karibu vyote.
 
Serikali imesema imetenga shilingi Bilioni 10 kwa ukarabati wa viwanja kadhaa vya michezo ambavyo kwa sasa vinamilikiwa na CCM.

Kiuhalisia viwanja hivyo vilijengwa na wananchi wakati wa chama kimoja kwa michango, makato kama ushuru na kodi mbalimbali kwenye Halmashauri zao lakini vikaporwa na CCM baada ya kuanza vyama vingi.

Sasa wameshindwa kuvihudumia lakini ndio wanakusanya mapato na leo wanataka hela za serikali zikakarabati viwanja hivyo na mapato bado yanaendelea kuchukuliwa na CCM.

Huu ni wizi wa mchana kabisa na sio wa kunyamaziwa. Kama wameshindwa kuvihudumia basi wavikabidhi kwenye council vilipo.
Upo sahihi
Sasa kama watakarabati kwa fedha za serikali basi vyama vingine viruhusiwe kufanya mikutano ya hadhara viwanjani humo.
 
Back
Top Bottom