Napinga Hela za Umma kutumika kukarabati Viwanja vya Soka vya CCM

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,600
218,001
Waziri wa Sanaa na Michezo , Mh Mchengerwa wakati akiwasilisha hotuba ya Bajeti ya Wizara yake bungeni, pamoja na mambo mengine , amesema kwamba , SERIKALI IMETENGA ZAIDI YA SHILINGI BILIONI 10 KWA AJILI YA KUKARABATI VIWANJA VYA MICHEZO VINAVYOMILIKIWA NA CCM .

Miongoni mwa viwanja vitakavyofaidi hela hizo ZISIZO ZA HALALI , umo uwanja wa Sokoine ulioko Mkoani Mbeya , ulioharibiwa na Spika wa bunge la Tanzania Tulia Ackson , ambaye aliitisha Tamasha la Singeli na vigodoro wakati wa kampeni za ubunge za 2020 , jambo lililosababisha Uwanja huo kuwa Chanzo Kikuu cha Mafuriko Mjini Mbeya .

Napinga jambo hili kwa sababu , Viwanja vya ccm si viwanja vya Umma , ni mali ya Chama Chao , iko siku wanaweza kuamua kuvifunga ama kubadilisha matumizi , Wananchi wa Tanzania hawahusiki navyo , Kuchukua hela za watu wote milioni 70 kukarabati viwanja vya chama cha watu wasiozidi milioni 10 ( ikumbukwe kwamba wanaccm hawazidi mil 10 ) ni UHUJUMU UCHUMI , CCM kama chama cha siasa kinavyo vyanzo vya mapato yake , japo vingi ni vya dhuluma , lakini pia kinapata karibu ruzuku yote inayotolewa kwa vyama vya siasa baada ya kuhujumu uchaguzi wa 2020 , Itumie mapato ya chama chao kukarabati viwanja hivyo , lakini kutumia hela za umma ni ubabe wa Kishamba sana na utawagharimu wahusika wote , hata kama siyo leo .

Waziri Mchengerwa asipoondoa jambo hili NITAITISHA MAANDAMANO NCHI NZIMA KUPINGA WIZI HUU WA MCHANA ULIOPANGWA KISHAMBA KABISA .

Ni kweli Watanzania wanaweza kuwa Mabwege , Lakini si Mabwege wa kuwafananisha na Zumbukuku kwa kiwango hicho .

Naomba Kuwasilisha .
 
Kipindi cha JPm wana ChAdeMa wengi waliunga mkono juhudi za mwendazake na mabilioni yalitumika kuwanunua na kurudia na chaguzi.
 
Mbowe anasemaje kwanza!!?? Kabla ya yote!. Maana mmebaki mnatangatanga tu 😂😂😂😂😂
 
Back
Top Bottom