Imekaaje Serikali kuingia ubia na CCM kukarabati viwanja vya CCM?

Hismastersvoice

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
18,388
21,877
Hii imekaaje kwa Serikali kutumia pesa za umma kukarabati viwanja ambavyo CCM ilishirikiana na serikali kupora viwanja vya umma ambavyo ni wazi CCM wameshindwa kuvitunza na sasa CCM inataka kutumia pesa za umma kuvikarabati, haiingii akilini CCM ambayo kila mwezi inachukua mabilioni ya pesa za umma baada ya kujipa ushindi wa viti vyote vya wabunge na madiwani kutuambia haina uwezo kuvikarabati.

Hii haikubaliki ni hujuma.
 
Unajua maana ya ubia na Serikali

Viwanja hivyo vitasaidia Serikali kuongeza Mapato kupitia ubia
 
Imekaa hivi viwanja ni mali ya CCM ndio ilijenga CHADEMA hawajenga hata uwanja mmoja ofisi tu imewashinda kujenga ,pili Serikal inapata mapato asilimia flani inaenda kwenye mapato ya Serikali, tatu Serikali inataka AFCON ichezewe Tanzania, nne ni jukumu la Serikali kuboresha mazingira ya viwanja nchini.
 
Imekaa hiv viwanja ni mali ya ccm ndio ilijenga chadena hawajenga hata uwanja mmpja ofis tu imewashinda kujenga pili serikal inapata mapato asilimia flan inaenda kwenye mapato ya serikal tatu serikal inataka afcon ichezewe tanzania nne ni jukumu la serikal kuboresha mazingira ya viwanja nchin
TANU au CCM haijawahi kujenga Kiwanja chochote hapa Nchini Viwanja vimejengwa na Wananchi na Serikali Wananchi Wamechangishwa Mifugo mazao na Pesa CCM imejimilikisha kwa Nguvu Viwanja hivyo Busara Viwe vya Serikali au Halmashauri

Sent from my SM-J600F using JamiiForums mobile app
 
Unajua maana ya ubia na Serikali

Viwanja hivyo vitasaidia Serikali kuongeza Mapato kupitia ubia
Serikali ilikwisha acha kufanya biashara, serikali pia ina maslahi ndani ya CCM ndiyo sababu imejipa fedha kukarabati viwanja vyao badala ya kuvirudisha serikalini.
 
Imekaa hiv viwanja ni mali ya ccm ndio ilijenga chadena hawajenga hata uwanja mmpja ofis tu imewashinda kujenga pili serikal inapata mapato asilimia flan inaenda kwenye mapato ya serikal tatu serikal inataka afcon ichezewe tanzania nne ni jukumu la serikal kuboresha mazingira ya viwanja nchin
Wakati wananchi walipokuwa wanavijenga viwanja kwa ajili ya mzunguko wa sherehe za kitaifa za Sabasaba wewe haukuwepo duniani yaani ulikuwa haujazaliwa, sasa Chadema imeingiaje humo! Pia wakati tunapata Uhuru kila mji ulikuwa na viwanja vya mpira vya serikali ambavyo hivi sasa eti ni mali ya CCM.
 
Imekaa vzuri sana; UBIA (PPP) itasaidia kuboreshwa kwa viwanja vya michezo na hata kuongeza ukusanyaji wa mapato

Ni muda muafaka sasa
 
TANU au CCM haijawahi kujenga Kiwanja chochote hapa Nchini Viwanja vimejengwa na Wananchi na Serikali Wananchi Wamechangishwa Mifugo mazao na Pesa CCM imejimilikisha kwa Nguvu Viwanja hivyo Busara Viwe vya Serikali au Halmashauri

Sent from my SM-J600F using JamiiForums mobile app
Unaweza kutofautisha tanu na ccm ni shiling moja yenye pande mbili ukisema tanu wamejenga na sio ccm na wana tanu ndio walichangia pesa za kujenga uko sahihi tanu baadae ikawa ccm kwa kauli moja tuseme wanatanu ndio walichangia baadae ikaja ccm kwa hiyo tunakubaliana ni mali ya ccm ambayo zaman ilikua tanu.sawasawaa
 
Wakati wananchi walipokuwa wanavijenga viwanja kwa ajili ya mzunguko wa sherehe za kitaifa za Sabasaba wewe haukuwepo duniani yaani ulikuwa haujazaliwa, sasa Chadema imeingiaje humo! Pia wakati tunapata Uhuru kila mji ulikuwa na viwanja vya mpira vya serikali ambavyo hivi sasa eti ni mali ya CCM.
Tanu ndio walijenga na tanu ndio ikazaa ccm ni lugha flan hiv mpaka uwe na akili timamu ndio utaelewa kwanini ccm na tanu ni kitu kimoja chadema imeingia sababu ni moja ya chama cha siasa kinachopokea michango ming sana kila siku lakin hakimiliki hata jengo moja tafaut na tanu au ccm ambayo wamewaletea watanzania viwanja
 
Yule mzee alisema CCM ndio inaiambia serikali na sio serikali inaiambia CCM.

Kama majizi ya kura yalipitisha kura zilizokwishapigwa kwenye vikapu, hotpot ,mabegi na bahasha mchana kweupe na polisi waangalia unafikiri kuna kipya tena.?
 
Hii imekaaje kwa Serikali kutumia pesa za umma kukarabati viwanja ambavyo CCM ilishirikiana na serikali kupora viwanja vya umma ambavyo ni wazi CCM wameshindwa kuvitunza na sasa CCM inataka kutumia pesa za umma kuvikarabati, haiingii akilini CCM ambayo kila mwezi inachukua mabilioni ya pesa za umma baada ya kujipa ushindi wa viti vyote vya wabunge na madiwani kutuambia haina uwezo kuvikarabati.

Hii haikubaliki ni hujuma.
Kwani kuna shida?
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom